Waziri mwingine aihujumu CHADEMA

Waziri mwingine aihujumu CHADEMA

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,463
BAADA ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira kutajwa kuwa nyuma ya mkakati wa kukihujumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waziri mwingine ametajwa kufadhili kundi la vijana wasaliti wa chama hicho. Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa kigogo huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni naibu waziri wa wizara moja nyeti, juzi alifadhili kikao cha kutathimini athari za tamko la aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa wa Baraza la Vijana la CHADEMA Taifa (BAVICHA) aliyefukuzwa, Juliana Shonza. Naibu huyo pia anadaiwa kutumia siasa za ukanda na ukabila kuwarubuni vijana waliofukuzwa uanachama wa BAVICHA.Baadhi ya vijana hao waliofukuzwa uanachama na kuungwa mkono na naibu waziri huyo, ni Shonza, Mtella Mwampamba aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki 2010 na Habib Mchange aliyegombea Kibaha Mjini.

Vijana hao walivuliwa uanachama baada ya BAVICHA kujiridhisha kuwa walikuwa wakitumiwa na CCM pamoja na baadhi ya viongozi wawili ndani ya CHADEMA ili kutoa matusi kwa viongozi waandamizi wa chama na kuwazushia uongo. BAVICHA pia iliwataja Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigella na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba, kuwa nyuma ya mkakati huo. Mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho juzi usiku, alisema kuwa watatathmini kazi aliyokuwa amepewa Shonza. Alisema kuwa Shonza alipewa kazi ya kutoa tamko la kuwatukana viongozi wakuu wa CHADEMA, kukishambulia chama na kuwashambulia baadhi ya viongozi wa BAVICHA, hasa mwenyekiti wake, John Heche.

"Tulikutana pale Mikocheni kwenye nyumba moja, tukajadili kwa mapana mkutano wa Shonza na waandishi wa habari baada ya kufukuzwa. Sikujua nyumba ni ya nani, lakini aliyekuwa mwenyeji zaidi ni Shigela," alisema.

Aliwataja wengine waliohudhuria kikao hicho kuwa ni Mwampamba, Tambwe Hiza, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Salumu Hapi pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, Wareni Kamnyoge. "Katika mkutano ule, Shigella alimuuliza Shonza anaendeleaje baada ya kutoa tamko na athari zake kwa jamii. Shonza alijieleza na baadaye wajumbe wakamsifu kwa kusema CHADEMA ni chama cha Wachaga na cha ukanda," aliongeza. Aliongeza kuwa Shigella alisema kuwa; "Hapa kwenye ukanda na ukabila, nakwambia Juliana umetufurahisha. Maana sasa, tutakuwa tumefanikiwa sana. Tutatembea na agenda hii hadi mwaka 2015."

Shigela hakupatikana kuthibitisha madai hayo, lakini Tambwe aliliambia gazeti hili kwa ufupi kuwa; "Mikakati ya kuwatumia vijana wa CHADEMA inaendelea vizuri." Akizungumza kwa kujiamini, Tambwe alisema juzi hakwenda Kinondoni hasa Mikocheni, lakini akathibitisha kuwa; "unachokisema cha kuwatumia vijana wa CHADEMA ni kweli maana mikakati ni ushindi katika uchaguzi mkuu 2015." Kuhusu kuwapokea CCM vijana hao, Tambwe alisema hayo mengine ya kutumika au kupokelewa waulizwe viongozi maana hao ndiyo wasemaji.

Shonza hakupatikana ili kuzungumzia madai hayo, ingawa kuna taarifa kuwa wameahidiwa kazi kulingana na elimu zao. Shonza inadaiwa kuwa ataajiriwa kwenye kazi za ustawi wa jamii, Mwampamba ameahidiwa ualimu.

Chanzo hicho kinaongeza kuwa, kwa mujibu wa mkakati huo, Shonza na kundi lake, wamepanga kufanya ziara mikoani, wakianzia Mbeya, Iringa na baaye Mwanza. Naibu waziri anayedaiwa kuwafadhili inasemekana anatumia ukabila na ukanda akisema kuwa waliofukuzwa ni vijana wa Mbeya, na hivyo anataka kuwatumia kuivuruga CHADEMA mkoani humo hasa Jimbo la Mbeya Mjini analojitapa kutaka kulirejesha CCM.

 
Kama gazeti limeweza kuyataja majina ya washiriki wengine kwa nini linapata kigugumizi kulitaja jina na naibu waziri au wizara anayoisimamia.

Huu unakuwa ni uandishi wa habari katika mazingira ya kufikilika na siyo katika habari kamilifu.

Haya ndiyo magazeti ya Tanzania. No investigative journalism. Udaku tupu.
 
Bado wizi mtupu,Kichwa cha habari kimeanza na waziri halafu ndani jina kapuni!Nyie ni Mamulugo tu!
 
Hapa anaongelewa Mlugo? Maana ndiye aliyetamba kutaka kulirudisha jimbo la mbeya mjini mikononi mwa CCM!

Umefika wakati CHADEMA itabidi wafanye kazi ya ziada katika kupanua huduma ya utoaji wa taarifa kwa jamii. Maana habari kama hizi kamwe haziwezi kuandikwa na magazeti ya mwananchi, wala habari leo. Sasa itawabidi CHADEMA wasiendelee kulitegemea gazeti la Tanzania daima tu, bali waangalie uwezekano wa kuwa na gazeti la chama, na pia kuwa na redio plus television ya chama.

Nashangaa sana ni kwa vipi CHADEMA wanashindwa kufanya hili. Kwa ruzuku wanayopata, wakijipanga vizuri wanaweza kabisa kuwa na hivi vitu. Kitendo cha kukosa vyombo vyake vya habari, kutaiwezesha CCM kusambaza propaganda zake kirahisi na kuuhadaa umma wa watanzania, matokeo yake tutajikuta na 2015, tunashindwa kuchukua nchi.
 
Hivi Tanzania Daima ni gazeti la Chadema au la Mwanachadema?
Mbowe mjanja sana Kazima mikakati ya Kuanzisha Gazeti la chama na sasa Gazeti lake linatumiwa na chama kwenye Propaganda but Faida yote inakwenda Free Media( kwa mbowe) hizo ni habari za kushtua 'makamanda' wanunuwe gazeti kwa wingi kumbe wanatunisha mfuko wa Dj! Kapu la mjanja anaetia mkono ni Mwerevu pekee!
 
mKAKATI HUU UPO!... mIMI NINA TAARIFA YA MULUGO KUWAPA SAPOTI HAWA VIJANA!.. hELA WANAYOPEWA KIDOGO KIDOGO INAWEZA KUWAFIKISHA MAHALI POPOTE HAPA NCHINI LAKINI SI KUWATOA KIMAISHA!... bAADHI YA MASISIEM WANAOWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MASALIA NI NCHEMBA, SHIGELA, TAMBWE HIZA, NA MWENEZI WA MAGAMBA... hIVI SASA HAWA JAMAA HAWAAMINI MTU!... WANAMASHAKA KUWA WANAREKODIWA, WANAHOFU KUPELELEZWA KUPITIA SIMU ZAO!.. kIUFUPI HAWAJIAMINI!
 
Hivi Tanzania Daima ni gazeti la Chadema au la Mwanachadema?
Mbowe mjanja sana Kazima mikakati ya Kuanzisha Gazeti la chama na sasa Gazeti lake linatumiwa na chama kwenye Propaganda but Faida yote inakwenda Free Media( kwa mbowe) hizo ni habari za kushtua 'makamanda' wanunuwe gazeti kwa wingi kumbe wanatunisha mfuko wa Dj! Kapu la mjanja anaetia mkono ni Mwerevu pekee!

mAJINI YABUBUJIKA!
 
mKAKATI HUU UPO!... mIMI NINA TAARIFA YA MULUGO KUWAPA SAPOTI HAWA VIJANA!.. hELA WANAYOPEWA KIDOGO KIDOGO INAWEZA KUWAFIKISHA MAHALI POPOTE HAPA NCHINI LAKINI SI KUWATOA KIMAISHA!... bAADHI YA MASISIEM WANAOWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MASALIA NI NCHEMBA, SHIGELA, TAMBWE HIZA, NA MWENEZI WA MAGAMBA... hIVI SASA HAWA JAMAA HAWAAMINI MTU!... WANAMASHAKA KUWA WANAREKODIWA, WANAHOFU KUPELELEZWA KUPITIA SIMU ZAO!.. kIUFUPI HAWAJIAMINI!
umaskini mbaya kaka ndo mana BABU anajichotea mil 7 kwa mwezi
 
Mkuu Ritz
Chadema badala ya kumaliza matatizo yao wanakimbilia habari za kutunga kama hii; ni mtu pimbi ndiye atakayekubaliana na hili.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
JULIAS sHENZ, eDDA MWAMALALA, MTERA MWAMPAMBA, NA HABIBA MCHANGE HELA ZA KUZUNGUKA MAHOTELI MNAZIPATA WAPI?!!!.......
kama nyie mnaakili na demokrasia hao akina mamuya na saanane mbona mmewaacha??? hakika hamtachukua kamwe madaraka ya nchi hii
 
Mkuu Ritz
Chadema badala ya kumaliza matatizo yao wanakimbilia habari za kutunga kama hii; ni mtu pimbi ndiye atakayekubaliana na hili.

Chama
Gongo la mboto DSM
tatizo lao wameona umaarufu wao umeshuka ndo mana wanakimbilia kuleta hoja za kitoto
 
hili ni jukwaa la grat thinkers acha kujadili ujinga

kweli unaitwa nikanyagwe hata kiingereza umeamua kukanyagakanyaga tu, siku nyingine andika great.
kwa taarifa yako great thinker huwa akurupuki kurupuki kama hapo juu.

kuna dictionary za kiswahili - english mitaani zitumie kupunguza ujinga, kama huna hela nitakusaidia

note: Jina linaumba

 
Back
Top Bottom