Waziri Mwigulu Nchemba jiuzulu; ulilazimisha wananchi wanyonywe kupitia tozo kubwa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Uliwadharau Watanzania na ukatoa kauli za kebehi kuwa hii ni sheria ya bunge hivyo kila mtanzania anatakiwa kulipa tozo za kizalendo ili kujenga shule, zahanati na vituo vya afya.

Watanzania wakakuona hufai maana ulibuni chanzo cha mapato kisichofaa na kinachowanyonya watanzania wanyonge. Maana kama ni vyanzo vya mapato vipo vingi na kama mchumi ulitakiwa usiwakabe na kuwanyonya wanyonge.

Nini kimekufanya urekebishe kanuni? Malalamiko ya watanzania?

Wewe hufai kuwa waziri wa fedha maana hauna huruma na raia ambao hata kupata mlo ni shida, ila wewe ulipiga mayowe wakamuliwe kana kambwa wanaokota pesa.

Jiuzuru kulinda heshima yako.
 


 
Mi wananiudhi wanaposema kodi ya tozo inarudi kwetu!!! Kwani kodi zote tunazolipa zinaenda wapi? Waziondoe basi ibaki hii ya tozo!!!
Unaponunua kitu huwa unadai risiti? Kama hudai basi unaikosesha serikali mapato, kwa hiyo ukiuza na kununua dai risiti
 
Kama kweli pesa itatumika kwa maendeleo ya nchi,ni ubunifu mzuri. Wale akina"unanijua mimi ni nani" hawapo, hivyo pesa itaenda kujenga taifa.
 
Bado makato ni makubwa sana waondoe ibaki kama zamani, kumbuka makato ya zamani kodi ipo ndani yake
 
Unaponunua kitu huwa unadai risiti? Kama hudai basi unaikosesha serikali mapato, kwa hiyo ukiuza na kununua dai risiti
Mbona mada yako siielewi? Tunazungumzia tozo siyo ukwepaji wa kulipa kodi. Ukwepaji wa kodi si jukumu langu kuhakikisha serikali inalipwa. Mimi nalipa kwa manunuzi na serikali ifanye wajibu wake wa kuhakikisha hao wanaoikusanya kwa niaba yao wanaiwakilisha kunakositahili. mimi sehemu yangu nimeshafanya na serikali ifanye sehemu yake.
 
Back
Top Bottom