samilakadunda
JF-Expert Member
- Oct 13, 2011
- 1,780
- 360
MBUNGE wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi (CHADEMA),
amemuumbua Naibu
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Philip
Mulugo, akidai hatishwi na
kauli zake kwani ana
elimu ya kuungaunga
akiwa ametumia jina la
mtu mwingine.
Kauli ya Mbilinyi maarufu
kama Sugu, inakuja siku
chache tangu Mulugo
atangaze kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM),
kitayarejesha majimbo
yaliyoko mikononi mwa
CHADEMA mkoani Mbeya,
likiwemo la Mbeya Mjini.
Akizungumza jana kwa
simu na Tanzania Daima,
Mbilinyi alisema
anamshangaa Mulugo kwa
kauli hiyo wakati akiwa na
hali mbaya kisiasa jimboni
kwake Songwe, kiasi cha
walimu kulalamika kukosa
hata chaki shuleni.
Mimi Mulugo hanitishi
hata kidogo maana
mambo yake yote ni ya
kuungaunga, kuanzia
elimu yake hadi siasa
jimboni. Huyu nimesoma
naye Sekondari ya Mbeya
Day nikiwa namtangulia,
na jina lake alikuwa
akiitwa Amim si hili la
Philip Mulugo, alisema.
Mbilinyi aliongeza kuwa
amefanya ziara jimboni
kwa Mulugo na kuelezwa
matatizo mengi
yanayowakabili wapiga
kura wake, na kwamba
alishangazwa na hatua ya
kuona walimu
wakilalamika kukosa chaki
wakati mbunge wao ni
naibu waziri wa elimu.
Haya mambo hatuyasemi
kwa sababu ya
kuwachukia CCM, bali
wanatuletea wenyewe
malalamiko wakitaka
tuwasaidie kusema. Sasa
Mulugo kashindwa kwake
anakuja Mbeya Mjini
kujitapa kuwa
wataningoa, alisema.
Aliongeza kuwa, kutokana
na ubabaishaji wa Mulugo,
kuanzia sasa ataanza
kumuita jina lake halali la
Amim ili watu wafahamu
kuwa hata kweli elimu
aliunga licha ya kuteuliwa
kuwa naibu waziri.
Kila mtu anakuwa na
ndoto, haikataliwi, hata
yeye alipotoka hadi kuwa
Naibu Waziri wa Elimu ni
ndoto pia, hakutegemea
kutokana na kusoma kwa
kuungaunga kwa kutumia
jina na cheti cha mtu,
hakuwa na uwezo,
alisema.
Mbilinyi alifafanua kuwa
Mulugo amemchokoza
mwenyewe na kumtaka
atambue kuwa yeye si wa
kuchezea wala chama
chake cha CHADEMA, na
kwamba chama hicho
chini yake au mtu
mwingine kuliacha Jimbo
la Mbeya Mjini ni baada ya
miaka 25 ijayo.
Alisema kutokana na
kupendwa na watu na
kuwapa changamoto
katika halmashauri licha
ya kwamba CCM wana
madiwani 22 na CHADEMA
14, anaamini kabisa kwa
sasa atajipanga kugombea
umeya badala ya ubunge.
Yaani Mulugo
amechemsha, hakuna
namna ya kumtoa Sugu
wala chama chake, na sasa
itafika wakati nitakuwa
meya, tena pale ndio
wamechemsha kabisa
kumweka mwenyekiti
asiyekubalika, na sasa
wakifanya mikutano yao
hawapati watu.
Mulugo ndiyo maana
hata historia ya nchi haijui
kwa kuwa elimu yake
yenyewe ina utata, aanze
kuchunguzwa,
mtaniambia kafanya
jambo la ajabu sana,
mwenzake alifaulu, lakini
kutokana na kutokuwa na
uwezo wa kuendelea na
shule yeye akanunua jina
lake, alisema.
Mbilinyi alisema kama
Mulugo anahitaji
kuendelea na siasa, basi
aende Mbeya Mjini ili
wamfundishe jinsi ya
kuishi na watu jimboni
kwake na kujua kero zao.
Hata hivyo, Mulugo
alipotafutwa kufafanua
madai hayo, alikwepa
kulisemea sakata la
kutumia jina lingine
wakati akisoma sekondari,
akisema kuna vitu ni stori,
lakini fitina hizo za kisiasa
ni majungu ya mtu na
mtu.
Aliongeza kuwa, Mbilinyi
aliwahi kwenda jimboni
kwake Songwe na kusema
madai hayo pamoja na
kumtukana, lakini
wananchi walimzomea
wakisema wao ndio
wanamfahamu mbunge
wao kuanzia elimu ya
msingi mpaka shahada.
Matusi yale yalisababisha
vurugu mpaka CHADEMA
wakapata kura 19 dhidi ya
kura 365 za CCM.
Nilichokisema kwenye
mkutano wa Mbeya ni
jambo la kawaida kwa
mwanasiasa yeyote aliye
makini, tena mjumbe wa
NEC.
Nilisema majimbo yote
ya CHADEMA Mkoa wa
Mbeya tutayarudisha. Sasa
kwani mbona wao kila
siku wanasema
watachukua majimbo yote
ya Mkoa wa Mbeya?
alisema Mulugo kupitia
ujumbe mfupi wa sms.
mh mulugo elezea kuhusu Jina na cheti chako basi??