Waziri Mulugo agawa rushwa hadharani

Waziri Mulugo agawa rushwa hadharani

Akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara huko wilayani mbozi, waziri Mulugo alionekana akiwa na kiroba kilichojaa mabulungutu ya noti huku akigawa mafungu ya noti hizo kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo kwa kisingizio kwamba anawezesha VICOBA.

Haikufahamika mara moja kwa nini aliamua kugawa fedha taslimu kwa watu binafsi badala ya kuziweka kwenye akaunti ya VICOBA. Hii inachukuliwa kuwa mbinu ya kujipanga kuwaweka wapiga kura wake sawa kisaikolojia kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2014 na 2015.

Source: TBC1

Kwani jimbo lake ni la Mbozi?
 
Lukosi komenti zako nyingine ni za kipumbavu sana! kwa hiyo unakubaliana na Mlugo kugawa rushwa? Mwingine anakusanya maaskofu huko Mwanza na kuanza kampeni za uraisi kwa rushwa, mwingine anagawa rushwa kwa nafasi ya ubunge 2015. ccm vipi, hamjiamini? Mpaka mwisho wa 2014 tutasikia mengi tu!!

Hata mi huyu lukosi sijui huwa ana mapepo anaropoka sana..! Au ndo anakingia kifua ccm? Hapon mtu kwa nguvu ya umma
 
Km nikilaza kwann .alipewa uwaziri lzma kunakitu alimfanyia mkuu
 
.....waheshimu Baba na mama (Wakubwa , wapakwa mafuta) upate miaka mingi na kheri Duniani .....na Usiseme uongo kabisa .....
 
url
url
yoweri-museveni-ronald-kibuule.jpg
Yoweri-Museveni-604x259.jpg
url
bro1.jpg
 
wanasiasa wa afrika huwachukulia wananchi (wapigakura) kama mbwa wa mwindaji. mbwa humsaidia mwindaji kukamata wanyama lakini huishia kulishwa mifupa huku bwana (mwindaji) akila minofu yote peke yake.

vivo hivyo, wananchi hujenga uchumi wa mabilioni ya shilingi lakini sehemu kubwa ya uchumi hufaidiwa na wanasiasa huku wananchi wakigawiwa makombo hadharani kwenye mikutano ya siasa.
 
Back
Top Bottom