tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,153
- 27,729
Akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara huko wilayani mbozi, waziri Mulugo alionekana akiwa na kiroba kilichojaa mabulungutu ya noti huku akigawa mafungu ya noti hizo kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo kwa kisingizio kwamba anawezesha VICOBA.
Haikufahamika mara moja kwa nini aliamua kugawa fedha taslimu kwa watu binafsi badala ya kuziweka kwenye akaunti ya VICOBA. Hii inachukuliwa kuwa mbinu ya kujipanga kuwaweka wapiga kura wake sawa kisaikolojia kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2014 na 2015.
Source: TBC1