Sanaa ya siasa: Mbinu za Rais Magufuli katika medani hii

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Nimefuatilia siasa za Tanzania kwa muda mrefu, nimefuatilia haiba, mienendo ya kisiasa ya watu mbalimbali maarufu nchini. Miongoni mwa hao, nimefuatilia namna ambavyo raisi Magufuli hufanya siasa zake. Ufuatao ni uchambuzi wa mbinu na tekniki amazo raisi Magufuli hutumia ili kufikia malengo yake ya kisiasa.

1. Mbinu ya wagawe uwatawale
Kama kuna mbinu kubwa ambayo raisi Magufuli huitumia katika kukidhi malengo yake ya kisiasa ni mbinu hii ya wagawe uwatawale, mbinu hii ameitumia sana na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri basi bila shaka umeshang'amua mara kadhaa ambapo raisi Magufuli ameitumia hii mbinu, nitaeleza chache:

(a) Baada ya kutoa ile kauli yake ya "wanawashwawashwa" ambayo ni dhahiri aliwalenga viongozi wastaafu walioanza kukosoa baadhi ya mambo nchini, alitafuta audience na viongozi wastaafu wa mhimili mwingine wa dola wastaafu, yaani Majaji wastaafu, kisha katika kuzungumza rais akawasifu wale Majaji kuwa "Nyie mmestaafu lakini hamsemisemi", na wakati mwingine akamsifu Waziri Mkuu Mstaafu Mzingo Pinda, kuwa "Mzee Pinda amestaafu na wala huwezi kumsikia akisemasema". Mbinu hii inawagawa hawa dhidi ya wale, kwamba hawa ni wazuri wale ni wabaya, hii hutuma meseji kwa wahusika kuwa hapendi kauli zao na hupelekea wale wenye nia ya kukosoakosoa serikali yake haswa wale ambao ni watu wazito kujistukia na hivyo kukaa kimya.

(b) Wakati mwingine alimualika Mzee Lowasa kwenye Uzinduzi wa Library mpya chuo kikuu, Wakati huo Lowasa alikuwa bado Chadema, katika hadhara hiyo Magufuli akamsifu sana Lowasa kuwa ni mtu aliyepikwa kiuongozi akapikika, akasema huwezi kumsikia Lowasa akitukana wala kukashifu, kisha akamwambia akawafundishe Chadema namna ya kufanya siasa nzuri. Ukisoma between the lines ni dhahiri hapa Rais Magufuli alikuwa anatumia mbinu ya kuwagawa wanachadema, Upande Mmoja yupo mtu mzuri Lowasa, Upande wa Pili wale wengine wabaya yaani akina Mbowe.

(c) Mbinu hii pia huitumia dhidi ya makundi ya dini, Nyakati ambazo Jumuia za Makanisa zikimkalia kooni, humsifu sheikh mkuu mara kwa mara.

(d) Au juzi hapa anamsamehe Kinana, huku Membe akifukuzwa uanachama, lengo hapa ni kupitisha wedge kati ya watu hao wawili na makundi ndani ya Chama yaliyokuwa yanasapoti hawa watu, kwa hiyo sasa hivi Mkorofi ni Membe na waliobaki sasa ni watu safi

2. Mbinu ya mtumbue mtu, kisha mpe nafasi nyingine ili awe mtiifu zaidi kwako
Mara kadhaa Rais Magufuli amewatumbua watu kwa sababu tofauti tofauti lakini baada ya muda fulani huwarejesha katika system na ukifuatilia mienendo ya hawa waliotumbuliwa, basi wakirudi huwa watiifu na wengine huwa waimba sifa kwa Magufuli kuliko kipimo.

(a) Amewahi kumtumbua Simbachawene kutoka kwenye uwaziri wa madini, baadae Simbachawene akawa mtetea serikali mzuri bungeni, alipoona amenyooka akamrudishia uwaziri wa mambo ya ndani, Sasa hivi Simbachawene ukimsikiliza ni mtiifu mno.

(b) Alimtumbua Charles Kichere kutoka TRA, Sasa hivi kamteua CAG

(c) Alimtumbua Diwani Athumani baadaye akamteua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

(c) Alimtumbua Andengenye kwa Ufisadi, baadae akamsamehe sasa hivi Andengenye kapelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, na kazi ya utiifu kwa Magufuli ameianza kwa nguvu kubwa kupita kiasi maana ameanza kuingilia uhuru wa wananchi kujumuika kwa kufuta kijiwe kikubwa cha kahawa amabcho wananchi hujadili siasa na mambo mbalimbali, na pia ameanza kusumbua Chama cha ACT Wazalendo kisifanye shughuli zake halali za kisiasa kupitia mikutano ya ndani. Hii yote ni dhahiri kwa kufanya hivyo anadhani anarudisha asante kwa bwana mkubwa wakati anavunja sheria na haki za wananchi.

(d) Mwigulu Nchemba, huyu alipotumbuliwa uwaziri, kisha akarudishiwa, miongoni mwa vitu vya kwanza kufanya ni kutamka waziwazi kuwa Mgombea urais wa CCM mwaka huu lazima awe ni Rais Magufuli.

3. Mbinu ya Usamaria mwema
Pita njiani huku na kule, gawa fedha, Mara kibao tumeona Raisi Magufuli akipita njiani na kugawa fedha waziwazi, Mbinu hii binafsi sijawahi kuiona watangulizi wake kuanzia Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete wakiitumia. Picha zipo mitandaoni rais akigawa Mabulungutu. Bila shaka mbinu hii inalenga "kununua" imani ya wananchi kuwa anajali shida za watu n.k

4. Mbinu ya kuonyesha Mamlaka ya Kidola
Rais Magufuli anapotaka kuongea na Taifa kuhusu jambo kubwa, hupenda iwepo hadhara ya viongozi wakubwa wa majeshi yetu, kuanzia wakati ule wa sakata la madini, hadi wakati wa kutoa hotuba kwa Taifa juu ya muelekeo wa Korona nchini huko Chato. Nadhani Rais hupenda mbinu hii ama kuonyesha kuwa yeye ndiye yko incharge na hivyo kila mtu amsikilize yeye, au kutuma meseji kuwa hilo ni suala very serious na lichukuliwe hivyo. Au kuwafanya wale wakosoaji hususan wanasiasa wafikirie mara mbilimbili juu ya ukosoaji wao maana ukikosoa utakuwa kinyume na hao waliohudhuria. Sasa huwa hakuna mwanaisiasa apendaye kwenda kinyume na vyombo vya dola ambavyo kimsingi huwa anapambana kisiasa ili siku moja aweze kuviongoza.

5. Rais Magufuli anatambua Star Power ya viongozi wastaafu na anaitumia kiakili
Mara kadhaa, Raisi Magufuli amejitahidi kuwaweka karibu sana viongozi wastaafu, Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Anajua wazi Viongozi wastaafu wana heshima kubwa mno mbele ya umma. Mara nyingi katika shughuli zake mbalimbali amewaita na kuwa nao karibu sana, na hii naamini haikuja by chance. Mimi hii naitafsiri kama mbinu ya kutumia kiakili sana kusafiria nyota za wastaafu wetu.

Naamini kuanzia lile vuguvugu la waraka wa akina kinana mpaka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kisiasa siamini kama Raisi Magufuli angeweza kuhimili ipasavyo mpasuko wa chama bila sapoti ya maraisi wastaafu, Maji yangekorogeka kwelikweli. Uongo mbaya. Kikwete anapendwa sana na umma, hata Magufuli analijua hilo, Mkapa anaheshimwa na wananchi na Mzee Mwinyi anahusudiwa na wananchi, bila kuwaweka hawa wazee karibu kama Magufuli alivyojitahidi angepata tabu sana kisiasa.

6. Mbinu ya Charm offensive
Hii inafanana sana na ile ya kwanza ya wagawe uwatawale, kwenye mbinu hii ili raisi Magufuli apate sapoti ya baadhi ya watu au makundi ya jamii basi huanza kuyamwagia sifa, kwa mfano anaweza kummwagia sifa askofu fulani, au shehe mkuu au mwanasiasa fulani (kafanya hivyo mara kadhaa kwa Mbatia, Loawasa alipokuwa Chadema), au kiongozi wa makundi fulani ya kijamii anayetafuta uungwaji mkono wake.

7. Kuteua watu ili kushawishi wengine nao wawe loyal au waunge mkono juhudi
Nimezisoma baadhi ya teuzi za rais Magufuli na nyingine zimekaa kimkakati sana, kwa mfano kuteua wapinzani akina Waitara, Katambi na Kafulira kulipelekea wimbi kubwa la Wapinzani wengine "kushawishiwa" kuunga mkono juhudi wakiamini kuwa kuwa nao huenda wakalamba ulaji pindi wakiiunga mkono juhudi.

Ninaweza kusema kwamba, mbinu hii ya kumuonyesha fisi fupa, imesaidia sana kuwavuta wanansiasa waroho wa madaraka walioko upinzani kuuza imani yao ya wananchi na kukimbilia huko kwenye fupa la madaraka. Hii mbinu pia imetumika kuwafanya wana CCM na wenyewe wabehave, maana wamegundua kuwa ukiwa upande wa Magufuli na ukawa muimba sifa na mapambio basi chance za kupewa fupa ni kubwa.

Bashe aliponda waraka wa Kinana baada ya siku chache akalamba unaibu waziri, Mollel alisifu namna ambavyo serikali inapambana na korona masiku machache baadae akalamba uteuzi, Mwigulu aliponda sana upinzani bungeni na aksifu mkakati wa serikali inavyopambana na Korona, haikupita mwezi akarudishwa kundini, Hii inatuma meseji gani, Raisi Magufuli anatuma meseji ya Wagawe Watawale.

8. Mbinu ya joho la Uchamungu
Raisi Magufuli anajua kuwa Watanzania waliowengi ni watu wa Imani na wanampenda Mungu, Hata kama watu ni watenda madhambi lakini wengi wetu ni watu wa Imani, Mara nyingi rais akitaka kupata uungwaji mkono wa watu au sympathy ya umma basi hutumia kauli za kidini kama vile "Mtangulizeni Mungu Mbele, Nampenda Yesu, Niombeeni", Hili naamini hulitumia ili kupunguza resistance ya jamii kwa baadhi ya maamuzi yake. Anajua akitanguliza Jina la Mungu basi atapata hadhira ya kusikilizwa na kuonekana kuwa ni mtu genuine, mwenye nia njema, mwenye malengo mema n.k. Sijui level ya Imani ya Rais Magufuli kwa Mungu, lakini naamini mara nyingi amelitumia jina la Mungu kisiasa ili kulainisha mioyo ya watu ikubaliane naye kwenye namna anavyoendesha mambo.

Hitimisho:
Hizo ni baadhi ya mbinu katika playbook ya kisiasa ya rais Magufuli. Nyingine nimeziacha kwa sababu si medani za kisiasa per se bali ni rafu zaidi kuliko uanasiasa, vitu kama kuwaweka ndani wapinzani au kauli zinazoshadadia mfumo dume kama vile zile za utani unaoelekezwa zaidi kwa wanawake hizo nimeziacha, au kumpiga kiatu cha kisiasa Membe
Ila ninachotaka kusema ni kwamba, kisiasa Rais Magufuli increasingly ameanza kuulewa mchezo huu wa kisiasa na ameanza kuonyesha onyesha ufundi fulanifulani katika hiyo gemu ya kisiasa, sivyo kama alivyokuwa hapo awali mwanzoni mwa utawala wake.
 
3. Mbinu ya Usamaria mwema
Pita njiani huku na kule, gawa fedha, Mara kibao tumeona Raisi Magufuli akipita njiani na kugawa fedha waziwazi, Mbinu hii binafsi sijawahi kuiona watangulizi wake kuanzia Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete wakiitumia. Picha zipo mitandaoni rais akigawa Mabulungutu. Bila shaka mbinu hii inalenga "kununua" imani ya wananchi kuwa anajali shida za watu n.k.

IMG_20200606_235613.jpg
IMG_20200606_235601.jpg
IMG_20200606_235552.jpg
 
Ni kweli ulichoandika hapo juu, hizo sifa zote anazo, lakini mwisho wa siku anakuja kutambulishwa zaidi kwa ubabe, asiependa kupokea ushauri wa wengine, na anatumia vitisho kwa maslahi yake kisiasa.

Binafsi naamini angebaki na mbinu ulizoorodhesha hapo juu bado angefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye utawala wake kutokana na aina ya makundi ya watu kwenye jamii anayoiongoza, kwani wengi wanapenda kujipendekeza, wanafiki, na wanaopenda kuweka maslahi yao binafsi mbele, hawa watu Magufuli angewapata kirahisi sana hata bila ukali na vitisho.
 
Nimefuatilia siasa za Tanzania kwa muda mrefu, nimefuatilia haiba, mienendo ya kisiasa ya watu mbalimbali maarufu nchini. Miongoni mwa hao, nimefuatilia namna ambavyo raisi Magufuli hufanya siasa zake. Ufuatao ni uchambuzi wa mbinu na tekniki amazo raisi Magufuli hutumia ili kufikia malengo yake ya kisiasa.

1. Mbinu ya wagawe uwatawale
Kama kuna mbinu kubwa ambayo raisi Magufuli huitumia katika kukidhi malengo yake ya kisiasa ni mbinu hii ya wagawe uwatawale, mbinu hii ameitumia sana na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri basi bila shaka umeshang'amua mara kadhaa ambapo raisi Magufuli ameitumia hii mbinu, nitaeleza chache:

(a) Baada ya kutoa ile kauli yake ya "wanawashwawashwa" ambayo ni dhahiri aliwalenga viongozi wastaafu walioanza kukosoa baadhi ya mambo nchini, alitafuta audience na viongozi wastaafu wa mhimili mwingine wa dola wastaafu, yaani Majaji wastaafu, kisha katika kuzungumza rais akawasifu wale Majaji kuwa "Nyie mmestaafu lakini hamsemisemi", na wakati mwingine akamsifu Waziri Mkuu Mstaafu Mzingo Pinda, kuwa "Mzee Pinda amestaafu na wala huwezi kumsikia akisemasema". Mbinu hii inawagawa hawa dhidi ya wale, kwamba hawa ni wazuri wale ni wabaya.

(b) Wakati mwingine alimualika Mzee Lowasa kwenye Uzinduzi wa Library mpya chuo kikuu, Wakati huo Lowasa alikuwa bado Chadema, katika hadhara hiyo Magufuli akamsifu sana Lowasa kuwa ni mtu aliyepikwa kiuongozi akapikika, akasema huwezi kumsikia Lowasa akitukana wala kukashifu, kisha akamwambia akawafundishe Chadema namna ya kufanya siasa nzuri. Ukisoma between the lines ni dhahiri hapa Rais Magufuli alikuwa anatumia mbinu ya kuwagawa wanachadema, Upande Mmoja yupo mtu mzuri Lowasa, Upande wa Pili wale wengine wabaya yaani akina Mbowe.

(c) Mbinu hii pia huitumia dhidi ya makundi ya dini, Nyakati ambazo Jumuia za Makanisa zikimkalia kooni, humsifu sheikh mkuu mara kwa mara.

(d) Au juzi hapa anamsamehe Kinana, huku Membe akifukuzwa uanachama, lengo hapa ni kupitisha wedge kati ya watu hao wawili na makundi ndani ya Chama yaliyokuwa yanasapoti hawa watu, kwa hiyo sasa hivi Mkorofi ni Membe na waliobaki sasa ni watu safi

2. Mbinu ya mtumbue mtu, kisha mpe nafasi nyingine ili awe mtiifu zaidi kwako
Mara kadhaa Rais Magufuli amewatumbua watu kwa sababu tofauti tofauti lakini baada ya muda fulani huwarejesha katika system na ukifuatilia mienendo ya hawa waliotumbuliwa, basi wakirudi huwa watiifu na wengine huwa waimba sifa kwa Magufuli kuliko kipimo.

(a) Amewahi kumtumbua Simbachawene kutoka kwenye uwaziri wa madini, baadae Simbachawene akawa mtetea serikali mzuri bungeni, alipoona amenyooka akamrudishia uwaziri wa mambo ya ndani, Sasa hivi Simbachawene ukimsikiliza ni mtiifu mno.

(b) Alimtumbua Charles Kichere kutoka TRA, Sasa hivi kamteua CAG

(c) Alimtumbua Diwani Athumani baadaye akamteua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

(c) Alimtumbua Andengenye kwa Ufisadi, baadae akamsamehe sasa hivi Andengenye kapelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, na kazi ya utiifu kwa Magufuli ameianza kwa nguvu kubwa kupita kiasi maana ameanza kuingilia uhuru wa wananchi kujumuika kwa kufuta kijiwe kikubwa cha kahawa amabcho wananchi hujadili siasa na mambo mbalimbali, na pia ameanza kusumbua Chama cha ACT Wazalendo kisifanye shughuli zake halali za kisiasa kupitia mikutano ya ndani. Hii yote ni dhahiri kwa kufanya hivyo anadhani anarudisha asante kwa bwana mkubwa wakati anavunja sheria na haki za wananchi.

(d) Mwigulu Nchemba, huyu alipotumbuliwa uwaziri, kisha akarudishiwa, miongoni mwa vitu vya kwanza kufanya ni kutamka waziwazi kuwa Mgombea urais wa CCM mwaka huu lazima awe ni Rais Magufuli.

3. Mbinu ya Usamaria mwema
Pita njiani huku na kule, gawa fedha, Mara kibao tumeona Raisi Magufuli akipita njiani na kugawa fedha waziwazi, Mbinu hii binafsi sijawahi kuiona watangulizi wake kuanzia Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete wakiitumia. Picha zipo mitandaoni rais akigawa Mabulungutu. Bila shaka mbinu hii inalenga "kununua" imani ya wananchi kuwa anajali shida za watu n.k

4. Mbinu ya kuonyesha Mamlaka ya Kidola
Rais Magufuli anapotaka kuongea na Taifa kuhusu jambo kubwa, hupenda iwepo hadhara ya viongozi wakubwa wa majeshi yetu, kuanzia wakati ule wa sakata la madini, hadi wakati wa kutoa hotuba kwa Taifa juu ya muelekeo wa Korona nchini huko Chato. Nadhani Rais hupenda mbinu hii ama kuonyesha kuwa yeye ndiye yko incharge na hivyo kila mtu amsikilize yeye, au kutuma meseji kuwa hilo ni suala very serious na lichukuliwe hivyo. Au kuwafanya wale wakosoaji hususan wanasiasa wafikirie mara mbilimbili juu ya ukosoaji wao maana ukikosoa utakuwa kinyume na hao waliohudhuria. Sasa huwa hakuna mwanaisiasa apendaye kwenda kinyume na vyombo vya dola ambavyo kimsingi huwa anapambana kisiasa ili siku moja aweze kuviongoza.

5. Rais Magufuli anatambua Star Power ya viongozi wastaafu na anaitumia kiakili
Mara kadhaa, Raisi Magufuli amejitahidi kuwaweka karibu sana viongozi wastaafu, Mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Anajua wazi Viongozi wastaafu wana heshima kubwa mno mbele ya umma. Mara nyingi katika shughuli zake mbalimbali amewaita na kuwa nao karibu sana, na hii naamini haikuja by chance. Mimi hii naitafsiri kama mbinu ya kutumia kiakili sana nyota ya wastaafu wetu.

Naamini kuanzia lile vuguvugu la waraka wa akina kinana mpaka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kisiasa siamini kama Raisi Magufuli angeweza kuhimili ipasavyo mpasuko wa chama bila sapoti ya maraisi wastaafu, Maji yangekorogeka kwelikweli. Uongo mbaya. Kikwete anapendwa sana na umma, hata Magufuli analijua hilo, Mkapa anaheshimwa na wananchi na Mzee Mwinyi anahusudiwa na wananchi, bila kuwaweka hawa wazee karibu kama Magufuli alivyojitahidi angepata tabu sana kisiasa.

6. Mbinu ya Charm offensive
Hii inafanana sana na ile ya kwanza ya wagawe uwatawale, kwenye mbinu hii ili raisi Magufuli apate sapoti ya baadhi ya watu au makundi ya jamii basi huanza kuyamwagia sifa, kwa mfano anaweza kummwagia sifa askofu fulani, au shehe mkuu au mwanasiasa fulani (kafanya hivyo mara kadhaa kwa Mbatia, Loawasa alipokuwa Chadema), au kiongozi wa makundi fulani ya kijamii etc

7. Kuteua watu ili kushawishi wengine nao wawe loyal au waunge mkono juhudi
Nimezisoma baadhi ya teuzi za rais Magufuli na nyingine zimekaa kimkakati sana, kwa mfano kuteua wapinzani akina Waitara, Katambi na Kafulira kulipelekea wimbi kubwa la Wapinzani wengine "kushawishiwa" kuunga mkono juhudi wakiamini kuwa kuwa nao huenda wakalamba ulaji pindi wakiiunga mkono juhudi.

Ninaweza kusema kwamba, mbinu hii ya kumuonyesha fisi fupa, imesaidia sana kuwavuta wanansiasa waroho wa madaraka walioko upinzani kuuza imani yao ya wananchi na kukimbilia huko kwenye fupa la madaraka. Hii mbinu pia imetumika kuwafanya wana CCM na wenyewe wabehave, maana wamegundua kuwa ukiwa upande wa Magufuli na ukawa muimba sifa na mapambio basi chance za kupewa fupa ni kubwa.

Bashe aliponda waraka wa Kinana baada ya siku chache akalamba unaibu waziri, Mollel alisifu namna ambavyo serikali inapambana na korona masiku machache baadae akalamba uteuzi, Mwigulu aliponda sana upinzani bungeni na aksifu mkakati wa serikali inavyopambana na Korona, haikupita mwezi akarudishwa kundini, Hii inatuma meseji gani, Raisi Magufuli anatuma meseji ya Wagawe Watawale

Hitimisho:
Hizo ni baadhi ya mbinu katika playbook ya kisiasa ya rais Magufuli. Nyingine nimeziacha kwa sababu si medani za kisiasa per se bali ni rafu zaidi kuliko uanasiasa, vitu kama kuwaweka ndani wapinzani au kauli zinazoshadadia mfumo dume kama vile zile za utani unaoelekezwa zaidi kwa wanawake hizo nimeziacha, au kumpiga kiatu cha kisiasa Membe
Ila ninachotaka kusema ni kwamba, kisiasa Rais Magufuli increasingly ameanza kuulewa mchezo huu wa kisiasa na ameanza kuonyesha onyesha ufundi fulanifulani katika hiyo gemu ya kisiasa, sivyo kama alivyokuwa hapo awali mwanzoni mwa utawala wake.
Waache watafunane walidhani wanamkomoa Mbowe.
 
Mbabe, mbinafsi mkabila na mkanda kun watu anawabagua waziwazi na ameshaligawa taifa vipande vipande.......Watu ni watulivu tu ila hawana amani kabisa maana hawaijui kesho yao
 
Na wateule wake nao wamefanikiwa sana kutumia mbinu moja kabambi UNAFIKI! Na inawasaidia sana huku wananchi wakiambulia HEWA.
 
Mkuu uko vizuri kiufafanuzi ila Uvccm watakushambulia
 
Ni kweli ulichoandika hapo juu, hizo sifa zote anazo, lakini mwisho wa siku anakuja kutambulishwa zaidi kwa ubabe, asiependa kupokea ushauri wa wengine, na anatumia vitisho kwa maslahi yake kisiasa.

Binafsi naamini angebaki na mbinu ulizoorodhesha hapo juu bado angefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye utawala wake kutokana na aina ya makundi ya watu kwenye jamii anayoiongoza, kwani wengi wanapenda kujipendekeza, wanafiki, na wanaopenda kuweka maslahi yao binafsi mbele, hawa watu Magufuli angewapata kirahisi sana hata bila ukali na vitisho.
Kila nyakati na majira yake!
sifa yake ndio hiyo, imemsaidia kutokuwa na marafiki wa kudumu ili pia imsaidie katika kupambana umimi mimi!!

mimi mtoto wa Fulani, Mimi ni Nani n.k imemsaidia,ingawa Kwa sehemu pia imempa maadui waliojificha mno, na hiyo yoote si Kwa ajiri yake yeye, ni Kwa ajiri ya Tz na watu wake

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom