Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak naye aishia kutua Tel Aviv. Awatakia ushindi Israel

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,191
10,925
Huku ikielezwa umebaki muda mfupi jeshi la Israel lianze kujingia Gaza kupigana mitaani na wapalestina,waziri mkuu wa Uiengereza naye ametua uwanja wa Ben Gurion kuonana na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Hiyo ni siku moja tu tangu kumalizika kwa aibu kwa ziara ya rais wa Marekani, Joe Biden ambaye nchi za kiarabu zilikataa kuonana naye.

Katika mazungumzo ya Sunak na Netanyahu, waziri mkuu huyo wa UK aliwaambia Israel kuwa amekwenda ili kuwaonesha kuwa Uiengereza iko pamoja nao na kwamba anawatakia ushindi katika vita vyao.

UK stands with Israel after ‘horrific act of terrorism’, says Sunak

1697716027482.png
 
Naye amekusudia kuitumbukiza Israel shimoni.
Tunaomba Hamasi waachie mateka hao ili kuepusha umwagaji damu pale Palestine, nchi za kiarabu ndo maana mnakosa sapoti ya nchi za Magharibi, huwezi kutetea eti Palestine wanaonewa na wakati Hamas ameshikilia mateka, na ndo ameanza mashambulizi. Israel hawezi kutishwa na ujanja ujanja na propaganda, anajua akiwachekea hamasi na kuogopa ndo mwanzo wa kuangamia Kwa wayahudi pale Israel, kesho tena watashambulia na kwenda kujificha kwenye hospital, shule, makanisa na misikiti, akishambulia tu lawama.
 
Tunaomba Hamasi waachie mateka hao ili kuepusha umwagaji damu pale Palestine, nchi za kiarabu ndo maana mnakosa sapoti ya nchi za Magharibi, huwezi kutetea eti Palestine wanaonewa na wakati Hamas ameshikilia mateka, na ndo ameanza mashambulizi. Israel hawezi kutishwa na ujanja ujanja na propaganda, anajua akiwachekea hamasi na kuogopa ndo mwanzo wa kuangamia Kwa wayahudi pale Israel, kesho tena watashambulia na kwenda kujificha kwenye hospital, shule, makanisa na misikiti, akishambulia tu lawama.
Vita gani ya kushambulia watoa huduma za afya,waandishi wa habari na watoto acheni ukafiri.
 
Jana Kuna Profesa wa USA amesema Israel itashinda Vita Ila itapoteza eneo la Gaza,huyu sio Muislamu Ni kafir wa kutupwa.

Lakini Maandiko ya Allah anasema hakitasimama kiama mpaka Muislamu amuue myahudi,weka akilini kwamba Myahudi lazima atapoteza tu kwa mpalestina hata Kama sio leo.
Hizi elimu zenu za madrasa na stori zenu mnazodanganyana redio imani

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
 
watu wanafikiri ushindi utakwenda kwa Israel na Marekani na Uk ili baada ya hapo wapate kibri zaidi za kufanya kufru.
Huu ni mtihani mdogo tu kwa mataifa ya kiislamu ambapo kushindwa kwao kuonesha umoja wa kweli na Palestina wala hakutapelekea Allah s.w kuwapa ushindi wanyonge wanaoonewa kwa namna azijuwazo mwenyewe.Silaha kama makombora na nyuklia ni vitu vidogo sana kwake na ameviumba kama mtihani kwa wanadamu
 
Restless Hustler

Myahudi gani mwenye uwezo huo kijana wa hovyo?

Hao jamaa zenu walipendwa Sana na Allah na akawapa upendeleo zaidi kuliko watu wengine lakini hakutaka kushukuru neema walizopewa na Allah,Nabii Mussa aliwaokoa kutoka kwa farao hiyo Ni neema ya Allah kuwatoa kwenye mateso Makali.

Allah aliwashushia chakula moja kwa moja kutoka mbinguni lakini walikufuru wakaanza kukidharau na kukashifu wakaomba mateso walime wenyewe.

Baada ya kuamini Mussa akawaacha na haruni...wakatengeneza sanamu na Ndama wakaanza kumuabudu.

Hawa jamaa ndio watu walioshushiwa mitume wengi kuwaonya Tabia zao mbovu lakini hawakubadilika Mwisho wake Allah akawalaani mpaka leo.

Jiulize Kama sio laana Ni Nini....Israel inavyosifika kwa Mambo ya Teknolojia,kilimo,afya,ujenzi n.k kwa Nini Ni Taifa ambalo huwezi kusikia linavuma midomoni mwa watu Kama lipo?
Hawana umaarufu wa kuzungumzwa hata Kama wanayo Mambo makubwa wanayo yafanya.....laana imewafifiza Kama vile hawapo.
 
Kombora la Islamic jihads lilifeli kwenda Israel likaangukia Hospital ya Gaza sasa mnamsukumia lawama Israel wafia dini acheni uwongo na unafiki kutafuta huruma

Sent from my Infinix X663 using JamiiForums mobile app
Hiyo habari umepika mzee,wewe na vyombo vya kimagharibi vinavyo ripoti mubashara Nani mkweli?

Vita ya kushambulia hospitali,waandishi wa habari,watoto kweli Ni Vita?
 
Mdogo mdogo hii ndo naona vita ya 3 ya dunia inanukia, siyo ile ya Russia na Ukraine. Au la sivyo itakuwa Vita ya mauaji ya kutisha.
 
Waziri mkuu wa Uingereza Rish Sunak amemuomba Waziri mkuu wa Israel mh Netanyahu aruhusu kuingia Gaza Misaada ya kibinadamu

Netanyahu amesema dunia inapitia zama za giza

Source BBC news
 
Hamas kaua raia 1300 wa Israel, wewe unaona huo siyo ukafiri?
Israel kauwa wapalestina wangapi Tangu unapata kufahamu mgogoro wa mashabiki ya Kati?

Ukipiga hesabu mpaka leo Kati ya waisrael na wapalestina wangapi wameuwa wengi utaacha kuwatete hao Walaaniwa na Mungu.

Robo Tatu ya vifo Ni watoto Sasa hapo Kuna Vita?
 
Back
Top Bottom