Waziri Mkuu wa India M. Singh kuanza Ziara Tanzania Alhamisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu wa India M. Singh kuanza Ziara Tanzania Alhamisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 23, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa India kuanza ziara Tanzania Alhamisi

  [​IMG] (FikraPevu) Waziri Mkuu wa India Bw. Manmohan Singh anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi wiki hii kuanza ziara rasmi ya kiserikali kwa muda wa siku tatu akiwa mgeni wa Rais Jakaya Kikwete. Bw. Singh atakuwa anaingia nchini akitokea Ethiopia ambako atashirikia Mkutano wa pamoja wa Biashara kati ya India na Afrika. Ziara yake ya Ethiopia anaifanya kwa mara ya kwanza tangu ashike madaraka. Ziara yake katika Afrika itachukua siku sita.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Dar-es-Salaam Bw. Singh anakuja nchini kuitikia mwaliko ambao ulitolewa na Rais Kikwete kwa Waziri Mkuu huyo wa taifa ambalo linapiga kasi zaidi ya maendeleo na ambalo lina nguvu ya Nyuklia. “Mheshimiwa Singh amekubali mwaliko huo katika barua yake aliyomwandikia Rais Kikwete na iliyokabidhiwa kwake na Balozi wa India katika Tanzania, Mheshimiwa K.V. Bhagirah wakati Balozi huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete leo, Alhamisi, Mei 19, 2011, Ikulu, Dar es Salaam.” imeseta taarifa hiyo iliyosainiwa na Ikulu bila kusainiwa na mtu yeyote.


  Akijibu mwaliko huo Bw. Sing amesema kuwa “Nakushukuru kwa barua ya kunilialika kuitembelea nchi yako nzuri. Itakuwa ni heshima kwangu kuitembelea Tanzania na naukubali mwaliko huo kwa furaha kubwa” na kuwa “Nina ari kubwa kukutana nawe na marafiki wengine wa Tanzania wakati wa ziara hiyo na kujadili njia ya kuuinua uhusiano kati ya nchi zetu kwenye ngazi mpya kwa manufaa ya wananchi wa nchi zetu mbili”


  Ziara ya Bw. Singh nchini imekuja wakati ambapo taifa hilo la India likizidi kututumua nguvu zake za kiuchumi na ushawishi hasa katika eneo la Afrika na kuonekana ikiingia katika ushindani wa ushawishi kati ya na China pamoja na nchi za Magharibi ambazo zimekuwa na nafasi ya pekee katika bara la Afrika kwa muda mrefu.


  Kabla hajaanza ziara yake hiyo ndefu leo Jumatatu Bw. Singh alielezea siku ya Jumapili mwelekeo wa ziara yake hiyo kuwa uhusiano kati ya India na Afrika utahusisha zaidi ni “kuipa uwezo Afrika na kubadilishana ujuzi, biashara na ujenzi wa miundombinu”. Bw. Singh amesema kuwa “uwepo wa watu wengi wenye asili ya India katika kila kona ya Afrika ni ushahidi wa wazi wa mahusiano yetu ya kihistoria.”


  Soma Zaidi tovuti Dada ya JamiiForums -Fikrapevu.com
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  huyo naye ni mwizi kama mijizi mingine inayonyemela maliasili zetu tu. ingekuwa nchi za wenzetu angepokelewa kwa mabango ya 'hatukutaki mwizi', lakini kwa unafiki wetu na kuabudu ngozi nyeupe, tutapanga foleni na kuvikwa skafu za bendera za india kumpokea.
   
 3. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  naona anakuja kuchukua chuma chetu, haya bwana endeleeni kugawa mali zetu
   
 4. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wacha kutukana huu ni wakati wa utandawazi na kushirikiana na nchi kama India ni kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili yaani mutual benefit na hata Mwalimu Nyerere alisisitiza sana ushirikiano wa nchi za kusini na zisizofungamana na upande wowote hivyo kumtusi Waziri Mkuu wa India ni kumvunjia heshima na ni sisi ndio tuliomualika kufanya ziara nchini mwetu jazba na hamaki za kisiasa tuziache pembeni tuweke maslahi ya nchi yetu mbele kwanza.
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mgeni njoo wenyeji tupone!! :A S thumbs_up:
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Huyu ni kichwa cha Uchumi,Mchango wake ni mkubwa sana kwa Taifa hilo tangu akiwa waziri wa fedha.Sasa kichwa hicho kikikutana na hawa wenzetu wasio na uzalendo kwa Taifa wanaishia kusaini mikataba ya kinyonyaji tu na kuuza nchi kwa bei chee.
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  ndiyo unafiki wenyewe huo.

  rushwa, mgawo, epa, matrekta ya kilimo kwanza, rada(vithlani) na mambo mengine yenye sura ya ufisadi na rushwa, ukichunguza sana utakuta wahusika ni hao mabaniani.
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa nyie vijana wadogo mliosoma shule za vidatu , huyu waziri mkuu wa India Singh sio mgeni wa kuja hapa Tanzania; aliwahi kufanya kazi kwa karibu sana na hayati mwalimu Nyerere kwenye SOUTH COMMISSION iliyokuwa na ofisi zake hapa Dar na Geneva. Kutokana na kazi yao hiyo ndio kitabu kiitwacho THE CHALLENGE TO THE SOUTH kiliandikwa. Ni advocate mkubwa wa ushirikiano wa nchi zinazoendelea.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hili ni kweli lakini anakuja akiwa na wingu kubwa la ufisadi katika serikali yake kama lilivyo wingu la ufisadi kwenye serikali ya Kikwete.
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Anakuja kuangalia zile 30mil us d walizotoa mkopo nafuu wa ma trekta mengi sana zimefikia wapi???maana ndio yale matrekta pale mwenge jkt wanayapamba pale kama picha badala kwenda kuuza kwa strategy mikoani huko kuwakopesha kwa bei nzuri na installments wakulima wao wameyapanga tu....mengine hayajatoka yapo bandarini karibu mwaka sasa!!!!!aibu sana maana msaada serikali inataka india walipe hadi ushuuru wa bandari!!!
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  India's growing interests in Africa!!!!!!!!!!!!!!!
  china's growing interests in Africa!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  American's growing interests in Africa!!!!!!!!!!!!!
  Europe's growing interests in Africa!!!!!!!!!!!!!!

  your all mother****errs​
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  At the same time husikii kama Waafrika wenyewe wana growing interest in Afrika. Ukoloni haujaisha.
   
 13. C

  Claxane Senior Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaja kuwekeza kwenye umeme.
   
 14. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Du nikifikiria foleni zitakavyokua kesho nakosa amani. Hivi kuna anayejua ule mpango wa kumnunulia Raisi Helkopta ili aruke foleni yeye na wageni wake wakitoka na kwenda airport umeishia wapi?
   
 15. w

  wera New Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anakuja kuwaandalia wahindi ili wazidi kutunyonyua zaidi
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  you have noticed....
   
 17. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa wa nje waje wasije siyo tatizo kubwa kwetu - KIINI CHA MATATIZO YETU KIPO NDANI, Asipokuja huyu atakuja mwingine ila ukweli utabaki watanzania hatutanufaika na rasilimali zetu mpaka tutakapofumbua kitendawili cha UFISADI.
   
 18. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Inakuwaja nchi zenye uchumi mkubwa kama Marekani inajitaidi sana kubana idadi ya dhifa za kitaifa, wakati nchi masikini kama Tanzania zinatolewa kama njugu; kwa mfano, inasemekana tangu rais Obama aingie madarakani ni dhifa tano yu za kiserikali ambazo ameishatoa hadi sasa.
   
Loading...