Waziri Mkuu, taarifa zinadai idara na Wizara nyingi zinafunga mwaka na wakubwa wanagawana fedha za funga mwaka

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
462
1,000
Mhe. Waziri Mkuu tunalojukumu lakukushirikisha wasemavyo Watumishi wa umma hasa waliopo wizarani na kwenye Idara za serikali, naamini ninachokiandika hapa unakifahamu ila najaribu kukirudia ukiweke kwenye mpango kazi wako.

Nianze kukupongeza kwa kazi kubwa uliyofanya Wizara ya fedha, hongera sana. Pili niombe kukushirikisha kinachoendelea serikalini kwa kipindi hiki cha Mei na June.

1. Wakuu wengi wa taasisi wanazunguka zunguka nchini kujustfy malipo bila kazi ya msingi,fedha ya funga mwaka.

2. Fedha zinatoka hazina kwenda kwenye taasisi na idara za serikali kwa mafungu makubwa na zinalamishwa kutumika kabla ya mwaka mpya wa fedha, hapa kinachofanyika zinatengenezewa stakabadhi feki, risiti za kughushi pamoja retirement zakuonyesha zimetumika vyema. Wahusika wakuu ni wakaguzi wa ndani na nje, wahasibu wakuu na viongozi waandamizi. Fuatilia fedha zilitoka na zinazotoka utabaini mabilioni yanaliwa na kuwekewa taaarifa za uongo zinazobarikiwa na watawala na wakaguzi.

3. Fuatilia activities zilizoombewa fedha against Watendaji waliolipwa fedha hizo utabaini watu wa mipango, utumishi, ukaguzi(auditing) na uhasibu wamejilipa fedha as if Hawa ofisini. Fuatilia akaunti zao za simu na hata benk utabaini wateule wako au hata wa Rais na Watendaji waliopo chini yao wameneemeka huku watumishi walio mbali na ofisi za juu wakiwa na malimbikizo ya madai yasiyolipika.

4. Upo utamaduni umeibuka wakukipana mamilioni ya fedha kwa ajili ya vikao vyakushughulikia mashauri ya nidhamu kila sekta. Hapa nikuombe upate taarifa ya vikao vya kushughulika mashauri vilivyokaa,vilikaa wapi, waliwajadili wakina Nani, waliojadiliwa maamuzi yaliyotolewa na mashauri mangapi Bado?

Kinachofanyika nikuhitisha vikao kwa kupanga safari za kwenda kusikiliza, mfano mashauri ya Wizara ya Utalii ambayo wajumbe wa kamati wote wapo Dodoma sehemu yakupanda daladala wakakutana ofisi moja wakawasikiliza watuhumiwa utashangaa wanatoka Dodoma kwenda kwenye vikao Arusha au mkoa wanaodhani unafaha kujustfy matumizi. Hapa serikali inapigwa kwelikweli. Mulika kesi zilizorundikana kwa wakuu wa taasisi miaka hazisikilizwi zikaisha just kwa sababu watu wanataka walipane posho za vikao. Ila wakati huo waliosimamishwa wanalipwa bila kufanya kazi.

5. Kwanini hazina utoa fedha nyingi mwisho wa mwaka? Je hii siyo njia yao yakula? Trilion zinatoka ndani ya mqezi mmoja kama siyo kutengeneza na kualalisha ubadhirifu? Nchi zote zilizoendelea huu utaratibu haupo, hazina waelekezwe kuachana na mfumo huu wa kukwangua hazina yetu kwa kisingizio funga mwaka.

Nakukabidhi maeneo ya utafiti ukiyasimamia before end of June utabaini ulichokuta Wizara ya fedha ndicho kilichopo wizara zote na idara zote.

Hii ni alert kwa wakuu wa taasisi rudisheni mlizokwisha jilipa kinyemela la sivyo mtakumbuka uzi huu.

Mwinyi kasema tuseme nakukosoa huku tukitoa way forward. Niwaombe Makatibu wakuu, wakurugenzi, wenyeviti, makamishna na wote mlioteuliwa na Mhe. Rais "take this seriously, mnagawana au kuidhinisha ugawanaji wa fedha za walipa kodi isivyo mpendeza Mwenyenzi Mungu na msipobadilika tutawaombea mtumbuliwe kupitia special audit.

Niwatakie utafiti mwema nikisubiri kuona matokeo
 

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
3,884
2,000
Enzi za mwendazake mlipiga sana kelele kuwa pesa imebanwa

Leo tena mnakuja sema watu wanatumia pesa ovyo.
Haya yaliendelea hata kipindi cha mwenda zake, tena yalizidi sana kwani walikuwa wanatenga fungu kidogo linarudi hazina wakisema halikutumika halafu mkwanja unaobaki wanautafuna wote.

Hapa tupate katiba iliyo bora ili tukate mzizi wa ushenzi huu wote.
 

Fund man

JF-Expert Member
Feb 24, 2021
686
1,000
Wanakula Bila kunawa mikono? Daah! Ila Wana wezesha mzunguko wa fedha mtaani(kwa wananchi).
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,394
2,000
Huku chiiiiini kabisa ngazi ya Zahanati ya Kijiji pia kuna Fungu limekuja naona mganga mfawidhi na mhasibu wamejifungia eti wanarekebisha taarifa za MTUHA, wanaandika dodoso, wanajilipa (hawa naomba tuwache tu maana per diem ni sh. 30,000 tu kila mmoja alafu yalivyo majinga yanajifungia mawili tu siku likibuma wakauliza wenzao hawajuhi kama kuna fungu la fedha lilitumiwa!) komaa na hao wa Hazina!
 

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
506
1,000
Kama Kuna kipindi fedha za serikali upigwa na watu wachache ni kipindi Cha funga mwaka, yaani wateule uacha kurelease fedha July to April nakusubiri Mei to Juni wamwage fedha kwenye taasisi ili waanze mwaka mpya na bajeti mpya. Nini ufanyika;

Wanakutumia bilioni moja wanakuambia fanya ufanyavyo rejesha milioni mia tatu kwao, au kwenye Mikoa acc anatumiwa milion hamsini anarejesha ishirini.

Hiki ni kipindi ambacho mafuta ya magari, vipuri na matengenezo ufanyika sana. Manunuzi yasiyo na tija na malipo ya ovyo ufanywa na Kama ulivyosema, wanaobariki wizi huu ni Auditors kwa sababu wao ni sehemu ya mgao huu.

Wakimulika ili eneo wataachana na utaratibu wakukaa na fedha hazina nakuzitoa mwisho wa mwezi. Na hapa katibu Mkuu hazina na Waziri wanahusika maana wanashuhudia mchezo huu mbaya
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,128
2,000
Mkuu upo sahihi kwamba hizi posho zimekuwa kama vichaka vya upigaji na mara nyingi zinawanufaisha wakubwa na wale ambao wapo jikoni. Sasa nini kifanyike, mishahara na marupurupu iboreshwe kwa watumishi wote na posho ziidhinishwe na wakuu wa taasisi kwa safari na shughuli muhimu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom