Waziri Mkuu, stendi ya Songea inawalipa wengi

D2050

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
1,901
1,063
Waziri Mkuu naomba nikumbushe suala la stendi mpya.

Mara ya mwisho unafika Songea ulikuta mgogoro wa stendi mpya iliyojengwa kilo mita 20 mbali na mji.

Ulipokuwa Songea uliagiza mkuu wa mkoa na watendaji wa serikali wakae na wadau wa usafirishaji wajadili changamoto na waweze kuzitatua.

Naomba nikupe taarifa maagizo hayo hayajatekelezwa hadi leo hii.

Wafanyabiashara wa manispaa ya songea wameona wafanye mgomo wa kutofungwa maduka na wasafirishaji kuto toa huduma za usafiri hadi hapo serikali itakapo kaa na wadau kujadili matatizo yanayowakabili.

Leo 22/2/2021 maduka yote yamefungwa katika manispaa ya songea na daladala zote zimesimama hazitoi huduma.magari yote yaendayo pembezoni mwa manispaa hayatoi huduma.

Je, baada ya kuwachagua madiwani na wabunge wa CCM hamuoni umuhimu wa kuwatetea wananchi wenu? au hadi Rais aje ndio atatue suala hili?

Waziri Mkuu agizo lako lilikuwa la siasa tu maana hadi leo halitekelezeki.
 
aisee niliwah kufika kule nilishangaa sana.kuiona stend inayoitwa ya zaman ya mabus ya mikoan na hio inayoitwa mpya.
ya zaman ipo vizur inaonesha ilikua imechangamsha mji
hio ya mpya yan matope matupu giza
Afazali ingekua ya matope ipo kidogo mjin iyo mpya ipo mbali uko porini ili watanue mji eti
 
Ili kupanua mji ni sawa hizo 20 km
Kukiwa na ongezeko steady la watu ni sawa.. ila kama population inaongezeka kwa kusuasua.. move kama hii inaua Mji.. shughuli za usafirishaji ndizo zinachangamsha miji mingi midogo na ya kati.

Ukiondoa transportation node.. Mji unazima na biashara zinapwaya... Kabla ya move kama hizi lazima kuwe na study kupima impact yake.

Tatizo wakurugenzi wengi wanakimbilia unafuu wa ardhi ya kulipa fidia.. na hawaoni umuhimu wa kuboresha huduma hizi kwa maeneo zilipo kwa sasa..

Wenzetu nje huko huduma hazihami HOVYO HOVYO... Maana zinimpact kubwa kwenye spatial development pattern ambayo inaathiri gharama za kuishi ndani ya mji na kuathiri uwekezaji mwingine wowote uliofanya kwa kuzingatia uwepo wa huduma kama stand.
 
Songea hakuna ongezeko wala population kubwa, nashangaa sana stand kupelekwa mbali vile, halafu sasa abiria anayetoka njia ya Dar, analazimika kushuka pale then achukue usafiri mwingne had town centre, tena km ni usku tabu tupu.

Serikali iliangalie hili kwa jicho pana, wanaoumia ni wananchi wa kawaida.
 
Ni changamoto maeneo mengi sana... Miji inapanuliwa bila umuhimu wowote..
 
Huu mtindo wa hovyo mno , hii nchi ina watu wenye akili matope Sana , unapeleka stend 20km away kwenye mji kama Songea ??? Hvi viongozi wanafkr Kwa kutumia matako au makalio .... Stendi ni sehemu ya kushusha na kupakia abiria , sio lazima uwe na stend moja unaweza kuwa na stend hata tatu kulingana na mji unavyoingilika kupitia njia kuu... Kama ilivyo Mwanza , wafanyabiashara huko inabid mkaze mwanzo mwenga.. nothing to loose , ikibidi wenye mabas pia mzingue vile vile
 
Ulikua na ujumbe muzuri kulinga na usumbufu unao jitokeza kwa abilia na wafanya biadhara,lakini umeniuudhi kudanganya klmt 20 kwa wasio pajua watapata picha gani,upo kupotosha jamii natamani kukutukana mungu anisamehe tu,au kwa akiri yako unazani hapa jf niwewe tu unaepajua hapo songea,kama umeamua kutoa taarifa zingatia ukweri wa jambo, kutoka songea mjini kwenda shule ya tanga ilipo hiyo stend ni klmt 20.
 
Shida mtu anae ishi ruhuwiko akitaka kusafiri kwenda dar anatakiwa alipe nauli asubuhi ya pikipiki 15000 ili afike stendi iliyopo shule ya tanga, maana stendi nyingine zote hawaruhusiwi kupakia
Labda nikupe ushauli siku ukitaka kusafiri nenda alfajiri stend ya zamani hua kuna vigari vidodogo nauri 3000 mpaka 4000.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom