Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
ufanisi? Ni ule uliosababisha serikali kulipa fidia ya bilioni 3 kwa kubomoa petrol station jijini mwanza kwa madai kuwa imejengwa katika hifadhi ya barabara au upi?
Jatropher usilete chuki zako kuhalalisha upuuuzi kama huo!, usihadae wana jf kwa kurejea kesi ambazo serikali ilipoteza! Nani hajui kama ''law'' ni ''art''? Mbona mkataba dowans ulisitishwa kihalali lakini kesi tukapoteza?, nani hajui kama Zombe na wenzake waliua lakini wako mtaani wanakula kuku?, nani hajui kama babu seya na wanae hawakubaka lakini wako wanaendelea kunyea debe?, sheria ni sanaa na hapa tanzania inaongozwa na rushwa, na kama ujuavyo serikali haitoi rushwa kwa hiyo haishindi kesi nyingi!, hilo unalijua. Magufuli ni mchapa kazi na anafuata sheria. Sio ndugu yako huyo anakurupuka kusema wanaoua arubino wauawe halafu analia mwenyewe! PM AMECHEMKA, usitetee ujinga eti kisa magufuli aligusa interest zako! Koma
MENGINE YOTE ULIYOSEMA YANA BENEFIT OF DOUBT LAKINI LA MAGAFULI KUFUATA SHERIA NALIPINGA KABISA KWA SABABU MAGUFULI NI MMOJA WA WABUNGE WALIOKUWA KATIKA BUNGE LILILOPITISHA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NA 5 YA 1999, HIVYO ANAFAHAMU FIKA KUWA VIFUNGU NAMBA 15 NA 16 VINAWALINDA WATU WALIOGAWIWA ARDHI KATIKA OPERESHENI VIJIJI (SOMA KIAMBATANISHO). ILIKUWAJE MWAKA 2001 TENA BILA KUSHIRIKISHA NAGZI ZA MKOA. WILAYA, MANISPAA NA SERIKALI ZA MITAA AKAMWAGIZA MKANDARASI WA WIZARA KUINGIA MITA 120 NDANI YA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI PANDE ZOTE MBILI ZA BARABARA KWA KUTUMIA KANUNI ZA SHERIA YA BARABARA YA MWAKA 1967, AMBAZO KIMSINGI KUTOKEA 1999 HAZIWEZI KUFANYA KAZI MAHALI POPOTE PALIPOKUWA NA ARDHI YA VIJIJI?
IKIZINGATIWA KUWA MWAKA 2001, WAKATI ANAAGIZA ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI KUINGILIWA, ILIKUWA NI MIAKA MIWILI TU KUTOKEA KUPITISHWA KWA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NA 5 YA 1999; NA KAMA ILIVYO ADA SHERIA HIYO ILIKUWA HAIJACHAPISHWA, KUSAMBAZWA NA WANANCHI KUPATIWA ELIMU YA SHERIA HIYO. HIVYO WAKATI HUO WANANCHI WALIKUWA HAWAJUI HAKI ZAO NDIO MAANA AKAWABURUZA KWA KUWAPANDIA MAWE NA MABANGO YA KUONYESHA MWISHO WA HIFADHI YA BARABARA KATIKA ARDHI NA MAKZI YAO ISIVYO HALALI?
WATANZANIA NI LAZIMA TUJIFUNZE KUWA WAKWELI, HUYU MTU ALIWAFANYIA WANANCHI HAWA HILA. NA AMEWAATHIRI SANA KIJAMII NA KIUCHUMI, WATU WAMESHINDWA KUENDELEZA ARDHI NA MAKAZI YAO, MABENKI YAKASHINDWA KUTOA MIKOPO N.K. NDIO MAANA KATI YA UBUNGO HADI KIRUVIA HAUWEZI KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI WALA ATM KAMA ILIVYO MBAGALA KATIK ABARABARA YA KILWA AU TEGETE, BUNJU N.K KATIKA BARABARA YA BAGAMOYO.
KUCHAGUA SHERIA ZA KUFUATA NA KUWAFANYIWA WANANCHI HILA NDIO UNAKUUITA KUFUATA SHERIA?