Waziri Mkuu Pinda Apangua Hoja Kuwa Yeye ni Mzigo!. Kinana Anasubiriwa Kufafanua!.

Anayeweza kusema kuwa pinda hafai atakuwa na matatizo binafsi serikali chini ya uongozi wa pinda imetulia kweli watu wanafanya kazi kwa umakini mkubwa mapungufu ni sehemu ya utendaji.
 
Waziri Mkuu Pinda aliambia bunge hivi punde; Rais na Bunge vyaweza kumvua wadhifa; ikithibitika yeye ni mzigo asema yupo tayari kuwekwa kitimoto.
 
Ulikunywa nini kabla ya kuandika hiki ulichokiandika hapa?
Kwenye bajaj yangu ninayotembelea wakati ambapo situmii boda boda, kuna 3 za hard drinks, Black Lebel chupa kubwa, Red Label size ya kati na Jack Daniels size ya kasichana ka konyagi!, lakini jana nimelalia maji!, na asubuhi hii, asubuhi bado sijaiona!.
Pasco
 
Wabongo banaaaaaa!

Seriously jana kwenye gumzo watu wakadai LIVE ti bora LOWAHASA ARUDI TU au SALIM uliko huyu liyamba lya mfipa! Wabongo hamna jema haki vileeeee!
Wee Lara, usilitaje tena hilo jina humu jf usije kuniharibia bure hii thread!, kuna watu wakilisikia jina hilo wanapagawa na kuishia kulalama humu kutwa nzima!.
Pasco
 
Pasco kuwa mkweli. Kama yeye mwenyewe anakili kuwa majukumu mengine ni magumu hata kushukuru kama akisimamishwa ina maan kuwa ni dalili za kushindwa kazi. Binafsi nilishamskia kwa masikio yangu kwenye ziara moja abroad akisema kuwa kuongoza nchi ni kazi ngumu ........... maneno kama hayo hayastahili kusemwa kwa wananchi. kama ni ngumu waachie wenye uwezo waifanye. Kwa ujumla napingana na wewe kuwa huyu bwana anaweza kuwa Rais bora Tanzania. Mtu aliyewahi kusema kuwa wakiwakamata wala rushwa nchi itayumba leo unasema anaweza kuwa Rais bora?? Tatizo kubwa la nchi yetu ni rushwa, sasa kama anaogopa kuifight atawezaje kutupeleka kwenye ile ndoto yetu ..... ya nchi ya asli na maziwa!!?? Jamaa ni mziogo. Period!!

mbowe amekaliliwa akisema kuwa kuongoza chama cha siasa ni jambo gumu sana ni mzigo ambao kuubeba yataka moyo hata yeye hapendi kukatalia madarakani hili nalo unasemaje.
 
Tangu lini Pinda akawa bora kiasi hicho umsifie kuwa anafaa kuwa raisi. Pinda kateuliwa na mtu dhaifu kwa hiyo lazima na yeye awe dhaifu kusimamia wizara zake.
 
Inaonesha we wala huji kazi ya JF.Mtu mathalani yuko na simu anakuwekea taarifa mpya ili kujulisha wengine,wewe hata hicho kidogo alicholeta unalalama! akina Maxence Melo wangetegemea mambo ya kulipwa kwanza wala hata JF isingekuwepo! coment kama hizi kama yako Nicas Mtei inaonesha ni kwa nini taifa hili linasafari ndefu ya kufikia maendeleo.! post ya kijinga sana hii! we ilibidi uombe upatiwe ufafanuzi siyo suala la kulipwa.Ningekuwa mod ningekupiga ban tu!
Mkuu Rutunga, we have a serious problem ya kukosa just a little appreciation!.

Wana jf, tuwe na shukrani katika madogo ili tujaaliwe makubwa!.
Pasco
 
suala la kusema anafaa kuwa rais bora tuwaachie wananchi
wewe mara lowassa mara pinda hata hueleweki
mwandishi makini huwezi kuja na hitimisho kama hili
we toa mada tuachie sisi tutoe analysis...
Pasco punguza njaa.zingatia maadili ya uandishi.
 
Msimsingizie Kinana hakumtaja Pinda kuwa ni Waziri mzigo ila aliwataja mawaziri wa Kilimo.
 
Asiyeona kuwa Pinda ni mzigo naye ni mzigo. Hamkumbuki issue ya Jairo? Hamkumbuki "piga tu"? Hamkumbuki alivyosema mafisadi wakikamatwa nchi inatikisika?
Tatizo tuna PM na rais mizigo kwa wakati mmoja! Nani atatupangulia nafasi ya rais?
 
Tangu lini Pinda akawa bora kiasi hicho umsifie kuwa anafaa kuwa raisi. Pinda kateuliwa na mtu dhaifu kwa hiyo lazima na yeye awe dhaifu kusimamia wizara zake.
Mkuu Nitonye, hii sii kweli!. Dhaifu sawa lakini kuna wengi wazuri tuu aliowateua!. Kwani lile "jembe la Kaskazi" liliteuliwa na nani?!. Namaanisha lile "jiwe walilolikataa waashi!".
Pasco
 
Nimetokea kumfahamu the real Mizengo Kayanza Peter Pinda in reality, he is one of the very few Tanzanzanians that can make the best president this nation has ever had!. Kwa vile ndani ya CCM hakuna utaratibu to pick the best, then there is no chance this country will ever have the best president in foreseeable new future!, tena kule upande wa pili ndio msiseme kabisa!, ni majanga tupu!.
Pasco
.....na Lowassa akiwamo?
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda apangua hoja kuwa yeye ni mzigo!.

Upanguzi huo umefanyika bungeni leo asubuhi wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambapo aliulizwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana amenukuliwa na media akisema baadhi ya mawaziri akiwemo Mhe. Pinda ni mzigo!, jee yeye anazichukuliaje kauli hizo?.

Pinda alijibu kuwa na yeye amesikia kwenye media na kwa sasa Kinana bado yuko safarini akirejea watakaa naye na kumuuliza alimaanisha nini?.

Ila akesema Waziri Mkuu amesema yeye anasimamia wizara zaidi ya 20, inapotokea wizara 2 ndizo hazifanyi vizuri, sio kumtendea haki Waziri Mkuu kumuita ni mzigo kwa makosa ya wizara mbili huku nyingine nyingi zikifanya vizuri!.

Ila pia amekiri baadhi ya hoja ni mitazamo binafsi dhidi ya Pinda, alitegemea kama kuna hoja za msingi wangekaa naye na kumweleza mapungufu yake ni haya haya na haya, kudai tuu kuwa Waziri Mkuu ni mzigo sio kumtendea haki!, na yeye ni binadamu tuu kama wengine udhaifu ni ubinaadamu!.

Pia amesisitiza kuwa nafasi hiyo hakuomba, ameangaliwa akaonekana anafaa!. Iwapo alionekana anafaa lakini utendaji wake ukawa ni kweli hauridhishi, mamlaka yake ya uteuzi ukijiridhisha hafai, atampumzisha na kusema ukweli majukumu mengine ni mazito ukipumzishwa unashukuru Mungu!.

My Take.
Kwa maoni yangu, Mizengo Pinda anaonewa bure!. Kosa lake kubwa kuwa humble na down to earth!. Watu walimtaraji aonyeshe utendaji kwa kasi zaidi ya mtangulizi wake. Yaani watu walitaraji aonyeshe utendaji zaidi ya Edward Lowassa anything less than Lowassaism then anaonekana anapwaya!. Huku sio kumtendea haki hata kidogo!.

Nimetokea kumfahamu the real Mizengo Kayanza Peter Pinda in reality, he is one of the very few Tanzanzanians that can make the best president this nation has ever had!. Kwa vile ndani ya CCM hakuna utaratibu to pick the best, then there is no chance this country will ever have the best president in foreseeable new future!, tena kule upande wa pili ndio msiseme kabisa!, ni majanga tupu!.
Pasco

Sikutegemea coment kama hiyo kutoka kwako Pasco! Ni kusahau au nini? Unakumbuka kesi ya Dr. Ulimboka? Mabomu Arusha initiator ni nani? Kuuwa watu wanaotaka kushiriki siasa? Humble kivipi?Huyo hajui atendalo kwa kisingizio cha kutunza amani, we didnt have before, hapo wahusika ni panoja na Pm, Mkuu wa usalama na mkuu wa polisi, usihengeshe mkuu!
 
Hili ndilo kosa nililolizungumzia usimhukumu kwa kumlinganisha na mtangulizi wake!.
Pasco

Ndugu PASCO toka alivyotutoka Moringe Tanzania haijawahi pata Waziri mkuu bali kila tukiokota basi ni magarasha na sidhani hapo kama kuna kushinda
 
Mkuu Nitonye, hii sii kweli!. Dhaifu sawa lakini kuna wengi wazuri tuu aliowateua!. Kwani lile "jembe la Kaskazi" liliteuliwa na nani?!. Namaanisha lile "jiwe walilolikataa waashi!".
Pasco

Dhaifu ni dhaifu Pasco hata angeteua majembe mangapi maana utendaji wao unategemea maamuzi ya dhaifu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom