Waziri Mkuu Pinda Apangua Hoja Kuwa Yeye ni Mzigo!. Kinana Anasubiriwa Kufafanua!.

Watu walimtaraji aonyeshe utendaji kwa kasi zaidi ya mtangulizi wake. Yaani watu walitaraji aonyeshe utendaji zaidi ya Edward Lowassa anything less than Lowassaism then anaonekana anapwaya!.
Pasco

Pinda wanamuonea kwakweli, makosa ya mawaziri yeye abebe? mbona kabla ya Mama Ghasia, Hata mama Kombani alichemsha? lile wizara limeguke kwa Waziri Mkuu liwe wizara kamili apewe Mh Mwakyembe watanyooka hawa Wakurugenzi maana ndo waleta shida zote hizi..

BTW Mkuu Pasco mimi na wawe tunajulikana tuko upande gani ndani ya chama chetu!! tuko Monduli na nafasi zinazidi kujazwa maana hata ya mpigapicha wa Rais imeishachukuliwa! ahahha
 
Kaka Pasco unatumia kweli kichwa chako vizuri.........maana watu huwa wakimwandama mtu hawataki hata kuangalia upande wa pili.....Ushabiki Maandazi....Wewe Umesema ya ukweli leo....
 
basically WAZIRI MKUU ANATAKIWA AWE MTENDAJI MKUU WA SEREKALI ILA KWA SASA NINA WASI!!

Mtendaji mkuu wa serikali ni rais tu. Usifananishe waziri mkuu wa Tz na wa Uingereza au Ethiopia. Mifumo ni tofauti....
 
Wabongo banaaaaaa!

Seriously jana kwenye gumzo watu wakadai LIVE ti bora LOWAHASA ARUDI TU au SALIM uliko huyu liyamba lya mfipa! Wabongo hamna jema haki vileeeee!

Lara1 huku utakula ban rudi kule
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda ametamka bungeni yakuwa uwaziri mkuu ni msalaba,Amesema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwake muda mfupi uliopita.Nikufuatia kuulizwa Juu ya kauli za wabunge wa chama chake na upinzani kuwa amekuwa mzigo hvyo anapaswa kujiuzulu.Pinda amesema kuwa wabunge au rais wanauwezo wakumtoa na yeye
atapumua.

Ajiu uzulu kama msalaba!!
Chezea posho na shikamoo mzee kutoka kwa baby zake!!!
Maneno matupu hayo!!!!
Arudi kulima yeye si mtoto wa mkulima!!!!
A achane na siasa!!!
 
Waziri mkuu amekuwa mzigo kwa kuwa anaonekana ameshika makali na kuna mtu kashika mpini!!
Hana maamuzi wala kauli!!
Wana mcontrol kwa remote!!!
Cheo chake hakifanyii kazi ipasavyo!!
I salute Lowassa
Sorry for thinking loud!!!
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda apangua hoja kuwa yeye ni mzigo!.

Upanguzi huo umefanyika bungeni leo asubuhi wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambapo aliulizwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana amenukuliwa na media akisema baadhi ya mawaziri akiwemo Mhe. Pinda ni mzigo!, jee yeye anazichukuliaje kauli hizo?.

Pinda alijibu kuwa na yeye amesikia kwenye media na kwa sasa Kinana bado yuko safarini akirejea watakaa naye na kumuuliza alimaanisha nini?.

Ila akesema Waziri Mkuu amesema yeye anasimamia wizara zaidi ya 20, inapotokea wizara 2 ndizo hazifanyi vizuri, sio kumtendea haki Waziri Mkuu kumuita ni mzigo kwa makosa ya wizara mbili huku nyingine nyingi zikifanya vizuri!.

Ila pia amekiri baadhi ya hoja ni mitazamo binafsi dhidi ya Pinda, alitegemea kama kuna hoja za msingi wangekaa naye na kumweleza mapungufu yake ni haya haya na haya, kudai tuu kuwa Waziri Mkuu ni mzigo sio kumtendea haki!, na yeye ni binadamu tuu kama wengine udhaifu ni ubinaadamu!.

Pia amesisitiza kuwa nafasi hiyo hakuomba, ameangaliwa akaonekana anafaa!. Iwapo alionekana anafaa lakini utendaji wake ukawa ni kweli hauridhishi, mamlaka yake ya uteuzi ukijiridhisha hafai, atampumzisha na kusema ukweli majukumu mengine ni mazito ukipumzishwa unashukuru Mungu!.

My Take.
Kwa maoni yangu, Mizengo Pinda anaonewa bure!. Kosa lake kubwa kuwa humble na down to earth!. Watu walimtaraji aonyeshe utendaji kwa kasi zaidi ya mtangulizi wake. Yaani watu walitaraji aonyeshe utendaji zaidi ya Edward Lowassa anything less than Lowassaism then anaonekana anapwaya!. Huku sio kumtendea haki hata kidogo!.

Nimetokea kumfahamu the real Mizengo Kayanza Peter Pinda in reality, he is one of the very few Tanzanzanians that can make the best president this nation has ever had!. Kwa vile ndani ya CCM hakuna utaratibu to pick the best, then there is no chance this country will ever have the best president in foreseeable new future!, tena kule upande wa pili ndio msiseme kabisa!, ni majanga tupu!.
Pasco
Nasikitika sana vigezo vyako vya kuangalia eti the best candidate kwa ajili ya urais! Hivi umeshawahi kufikiri mtu anaesema liwalo na liwe mbali na matamko mengine tata halafu kesho yake mtu anatekwa na kupigwa nusura ya kufa? Hata kama alikuwa anajua mpango mzima ile statement pale palikuwa mahali sahihi? Embu kuwa sincere
 
Sina wasiwasi na Mh:pinda ni mwanasiasa makini na mtu SAFI lakini katika serekali hii kunabaadhi ya watu yeye hawezi kuwawajibisha.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Kaka Pasco unatumia kweli kichwa chako vizuri.........maana watu huwa wakimwandama mtu hawataki hata kuangalia upande wa pili.....Ushabiki Maandazi....Wewe Umesema ya ukweli leo....
Upande wa pili ndio upi mkuu?
 
...apigwe tu hata akilia lia bungeni apigwe tu maana tumechoka sasa na mizigo...
 
Ila pia amekiri baadhi ya hoja ni mitazamo binafsi dhidi ya Pinda, alitegemea kama kuna hoja za msingi wangekaa naye na kumweleza mapungufu yake ni haya haya na haya, kudai tuu kuwa Waziri Mkuu ni mzigo sio kumtendea haki!, na yeye ni binadamu tuu kama wengine udhaifu ni ubinaadamu!.
Kama anajua kunako mapungufu ni muhimu kuelezena wenyewe kwa wenyewe kwanza kwanini yeye, kila mara huwa anaongea tofauti na sera za mawaziri wake isitoshe akiwa kama bosi wao.

Si angeanza yeye kuwauliza wenzie hayo maamuzi wamefikiaje kuliko kutoa kauli tata mara kwa mara ambazo kinyume na agenda za wenzake, sasa huyo bosi gani kama sio mzigo tu kwa wenzie, labda tatizo ni mfumo wa kuchagua tu bila ya watu kuwa na interest in the first place.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom