Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,290
- 8,511
Hivi ni kweli sura yako ilivyo ndiyo roho yako ilivyo? jinsi sura inavyo kuwa mbaya na roho...sijui mambo ya saikolojia, lakini watu wenye sura mbaya hujihisi inferior, na kuhisi wako less regarded katika jamii, hivyo maamuzi hua ni ya chuki..."WApigeni tu mpaka wakome".
Hapa kuna ukweli mkubwa, wewe nenda tu hospitali ama benki. ukitaka kuhudumiwa haraka mtafute tu dada mwenye sura nzuri, msalimie na umwombe kuwa una haraka halafu utuletee jibu.
Nilishafanya hii kitu karibu mara 4. NMB magomeni mara 2 nilikuwa na haraka, nahitaji kutoa hela kupitia kaunta. Foleni ilikuwa balaa. Sasa nilichofanya ni kumfuata dada mmoja mrembo, japo alikuwa ana pete ya ndoa, nikamwomba anichukulia hela nina haraka, akachukua slip ndani ya dakika 5 nikashika pesa mkononi. Siku nyingine nikapata msaada wa dada mwingine mrembo palepale NMB Magomeni. Pia Ifakara hospitali (ST. FRANCIS) nikiwa natibiwa mimi mwenyewe miaka ya mwaka 1998. Nililazwa, akiingia nesi mmoja mrembo ananihudumia kwa ukarimu wa hali ya juu kweli kweli. Lakini wacha waingie wenye sura za MAGAMBA, utaona mziki wake. Shinyanga Hospitali ya mkoa, nilimpeleka mama yangu yangu. Nikaenda maabara nikakuta foleni kubwa, nikamwita dada mmoja Mrembo, nikamwelezea. Ndani ya nusu saa majibu yakatoka.
Kwa hiyo mkuu kuna ukweli flnai ndani yake