Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,041
- 103,472
Bora umeung'amua huo usanii wa kiutendaji. Siku zote ukiona tatizo la kiutendaji linatatuliwa kwenye makamera, usitegemee ufumbuzi hapo zaidi ya kusaka kick. Halafu huwezi kuamini, subiri itokee huyo waziri Mkuu abadilike aje mwingine, utashangaa na yeye atakuta tatizo ni hilo hilo, na usishangae na yeye akitumia mbinu hiyo hiyo ya kick.Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu. Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.
Amandla...