Profesa Kitila Mkumbo: Wawekezaji wengi SGR imewavutia

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Waziri Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema haya kuhusu uzinduzi wa treni ya mwendokasi

Jana tumefanya majaribio ya treni ya umeme kutoka Dar es salaam hadi Morogoro jambo kubwa ni kwamba wawekezaji wengi kwa sasa wanatamani kuwekeza maeneo ambayo Reli ya umeme ya SGR imepita, hivyo miongoni mwa sababu zinazowavutia wengi kuja kuwekeza Tanzania ni uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji.

Tumefanya maboresho 665 ya kisera, kisheria na kikanuni kwa miaka mitano iliyopita ambapo katika maboresho hayo zaidi ya maboresho 416 yalilenga kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara hii inaonyesha kuwa nchi yetu kwa sasa ina mazingira mazuri ya Biashara na uwekezaji.
 
Ufanisi wa reli ya sgr, unategemea mambo kadhaa, achilia mbali ukweli kwamba, haijakamilika na wala haijulikani itakamilika lini. Hivyo hakuna mwekezaji atakayevutiwa na kitu ambacho hakipo.
Ikitokea imekamilika, mwekezaji atavutiwa na huduma ya sgr (kama kuna mlolongo wa mambo na watendaji wenyewe mpaka wasukumwe na rushwa, hakuna mwekezaji atakayejisumbua nayo), unafuu wa gharama za matumizi na uokoaji muda na zaidi ni umeme wa uhakika wa kulisukuma hilo treni.
Na kama mlolongo wa usafiri unaanzia bandarini, basi, hata utendaji wa bandari nao unakuwa ni kigezo cha kumvuta mwekezaji.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom