Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
- Thread starter
- #941
- Obasanjo kuwafukuza kazi mawaziri wake haina maana yoyote kwetu Tanzania, kwanza yeye mwenyewe Obasanjo ni corrupt, the ishu hapa ni je Masha alikutana na Sagem Geneva au hapana? Na je Sagem ni kampuni yenye rushwa au hapana? Na je waziri wetu alijua mapema au hakujua?
- Swali ni je waziri alikutana na sagem huko Geneva au hapana? Wewe umeleta ushahidi wa google na ukadai kwamba kwa sababu uko hiyo wewe uko sayayri nyingine sasa ninakuuliza hivi serikali yetu itumie huu ushahidi wa google kumfukuza kazi waziri? Huu ushahidi wako wa google hata huko Nigeria umeshindwa kuwa-convict watuhumiwa sasa tutaufanyia nini?
- Ya power-breakfast ndio hayo, limeshindwa bunge letu la taifa sasa nani mwingine tena ataweza? Ninaomba kurudia tena kwamba kenye hili la vitambulisho waziri amelipangua tayari, akishakataa Spika tu ujue basi. Kosa lililofanyika ni papara za kutaka kumpata waziri na makosa, I hope litakuwa fundisho in the future kwamba ishu zingine zinahitaji kuachiwa mpaka zifike mwisho kwanza ndio uwapate wanaoshuka kwenye hili kuna mtu aliyekosea na kuwafanya wahusika washituke mapema, halafu ni lazima tuwe makini na hizi barua za ku-leak, maana in this case zilizkuwa zinalikishwa na wale wale wahusika tena kwa makusudi, matokeo ndio haya hakuna kinachoeleweka, yaani form a suspect to a victim, sasa hiii safisha safisha jina sio yeye anayeifanya ila kuna kikundi behind kinachomuongoza, yaani Kingunge, Almeir na Makamba na the boss ni the man Lowassa, akisaidiana na Nchimbi.
Tanzania tumefikaje huku maana hapa mbele ni giza tupu, hatuwezi kuwashupalia watangazaji wa Clouds hivi tulitegemea wafanye nini maskini wa Mungu wanaojaribu tu kutafuta riziki zao ambacho bunge limeshindwa kukifanya?
Umesomeka vizuri sana. But natoa angalizo: safari ya Masha ilianzia wapi? na kwanini alianzia huko? Majina uliyoyataja Mkuu yana maana kubwa kuliko wengi wanavyoyasoma katika maandishi, na kijana anapita juu ya "zulia jekundu" lililoandaliwa na usingetegemea lolote pale Clouds. Lakini kuna jambo moja tu, katika Presss Conf alisema hawafahamu kabisa SAGEM na hajawahi kukutana nao, leo anasema alikutana nao lakini si katika hoteli iliyoandikwa katika magazeti.
Angalizo lingine ni tuzitizame hizi kampuni kwa jicho makini zaidi:
Unisys ya Afrika Kusini, Giesecke & Devrient Fze ya Dubai, Iris Corporation Berhad ya Malaysia, Madras Security Printers ya India, Maruben Corporation ikishirikiana na Zetes na Nec ya Japan, Tata Consultancy Services ikishirikiana na Ontrack Innovations Ltd ya India.