Waziri Masauni: Mpaka kufikia 'March' mwakani wananchi wote mtakuwa mmepata kadi za NIDA

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,828
Waziri wa mambo ya ndani, Hamadi Masauni amesema kabla ya kufikia mwezi wa tatu mwaka 2023 wananchi wote watakuwa wamepata kadi zao za NIDA na haitazidi hapo, Masauni kasema inaweza kuwa hata Disemba mwaka huu.

Pia Masauni amesema wananchi ambao hawajapata vitambulisho lakini wana namba za utambulisho hakuwazuii kupata huduma na ametoa wito kwa taasisi hasa za umma kutowanyima huduma wananchi kwa kosa ambalo sio lao hivyo waendelee kutoa huduma kwa wananchi wenye namba za utambulisho.

Masauni amesema pesa yote ambayo ilitengwa katika bajeti, bilioni 42.5 Rais Samia ameshaitoa na imeshalipwa kwa mkandarasi. Masauni amesema karibu timu kutoka wizara ya mambo ya ndani ikiongozwa na naibu waziri ilienda kiwandani kushuhudia kadi zikizalishwa na zimeanza kupokelewa.

Pia, soma=> Serikali: Watanzania wote wenye sifa watapewa vitambulisho vya Taifa kufikia Disemba 31, 2021
 
safi sana serikali iko macho haswa
Hapa ilikuwa imelala!!??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom