‪Waziri Manyanya: Mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania wanaweza kula kwakuwa soko si zuri‬

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Dodoma: Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.

Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.

Akijibu swali hilo naibuwaziri wa viwanda na biashara, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.

Eng. Stella amesema mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania wanaweza kula badala ya kuwategemea watu wa maeneo mengine. Amesema biashara ni ushindani na kila watu wanahakikisha wanakidhi soko lao la ndani, upande wa Tanzania wanaendelea kutafuta soko lakini wakati huo huo wanaendelea kusisitiza watu wapende kutumia mbaazi.

Amesema Dodoma Mbaazi inauzwa mpaka 1,800 kwa kilo na soko la Dar es Salaam kwenye supermarket inauzwa mpaka 2,400 hivyo tusitegemee soko mpaka kutoka nje kwani hata ndani ya nchi bado kuna watu wanaweza kula mbaazi yeye akiwa mmojawapo pia inategemewa hata mashule yanaweza kutumia wakati masoko yanaendelea kutafutwa.

Nimecheka sana alivyojibu huyu mama...ni sawa na MTU aulize nyama ya mbuzi inafaida gani katika mwili ,alafu mama anjibu kuwa kuna mbuzi wa Rangi 2 mweupe na mweusi..
Huyu manyanya hamna kitu kabisa anajiita engineer kwa cheti cha Technical college halafu namkumbuka sana case ya ulimboka aliposema alitekwa na chadema baadaye akapandishwa cheo na jk
 
jibu zuri lkn lilihitaji ufafanuzi wa kina.
kwa nini soko limepotea ghafla?
je tutegemee likurudi lini?
serikali inafanya nini na imefikia wapi?
je utafiti wa ulaji wa mbaazi tanzania unasemaje, kwa nini wali maharage na sio wali mbaazi mezani kwa mtz?
je, jitihada gani inafanywa kutufanya tule, maana mfano mimi kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe nimekula mwaka jana?

jibu zuri lkn limekuwa na mapana mafinyu.
 
Kwakweli tuna Serikali ya Ajabu haijawahi KUTOKEA! Majibu ya HOVYO SANA HAYA! Acheni USHAMBA MMESHAKUJA MJINI! Kuathirika kwa soko la Mbaazi Ni kutokana na UJUAJI wa wanaojifanya Wana akili kumbe zinawatosha kubangulia maganda ya Korosho tu. Miaka yote soko letu lilikuwa India, iweje Mwaka Jana tu ndo India ipate mvua za kuwatosheleza KUVUNA Mbaazi ZINAZOWATOSHA?

HAYA MAJIBU MNAYAANDAA WAKATI MNAJISAIDIA HAJA KUBWA AU NDOGO? Mnawaumiza Wakulima for no good reason, mnakosa Kodi kwa mauzo ya Nje kwa sababu ya USHAMBA, mnakosa fedha za kutimiza Bajeti kuu kwa Serikali kila Mwaka kwa sababu ya SIASA za kishamba za danganya toto! Serkali ya CCM Nani kawaloga?

MH. Rais, wasaidizi wako hawakusaidii kutatua kero za Wananchi, sanasana wanapika majungu na majibu ya Hovyohovyo tu!
 
Hii sasa ni dharau iliyopitiliza aisee hivi hawa mawaziri wanajivunia nini hasa kwa kutoa majibu ya hovyo?

tapatalk_1519073600276.jpeg
 
duh kazi kweli kweli.......waziri anatoa majibu mepesi
nakumbuka nape aliuza umuhimu wa bombardier ,mwenyekiti wa chama tawala alitoa povu balaa
 
Kama anajua Watanzania Wanazipenda saaana Kwanini waliahidi Bungeni??
 
Jibu nililopewa mie. Kukosekana kwa soka ilitokana na zao hilo kuwa na mnunuzi mmoja, alipopata misukosuko haikuwaathiri Yanga tu hata sie wakulima. Sitalima zao tena lenye mnunuzi mmoja. Mwaka jana nililima eka tano Gairo, lakini sikuingia shambani kuvuna niliogapa kuongeza hasara ya kuwalipa vibarua.

Dodoma: Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita matatizo ya soko kushusha bei kutoka Tshs 2,000 mpaka 150. Amesema serikali iliahidi Bungeni kuwa itahakikisha inahangaika kupata soko la kuaminika la zao hilo.

Nape amesema sasa ni msimu wa kilimo hicho, kama bado hali haieleweki wananchi washauriwe waachane na mbaazi na badala yake wajikite kwenye mazao mengine ambayo yana soko la uhakika.

Akijibu swali hilo naibuwaziri wa kilimo, Eng. Stella Manyanya amemjibu kuwa ni kweli hakukuwa na hali inayoridhisha kwenye soko la mbaazi na ni kutokana na wadau waliokuwa wanategemewa sana ilikuwa ni India.

Eng. Stella amesema mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania wanaweza kula badala ya kuwategemea watu wa maeneo mengine. Amesema biashara ni ushindani na kila watu wanahakikisha wanakidhi soko lao la ndani, upande wa Tanzania wanaendelea kutafuta soko lakini wakati huo huo wanaendelea kusisitiza watu wapende kutumia mbaazi.

Amesema Dodoma Mbaazi inauzwa mpaka 1,800 kwa kilo na soko la Dar es Salaam kwenye supermarket inauzwa mpaka 2,400 hivyo tusitegemee soko mpaka kutoka nje kwani hata ndani ya nchi bado kuna watu wanaweza kula mbaazi yeye akiwa mmojawapo pia inategemewa hata mashule yanaweza kutumia wakati masoko yanaendelea kutafutwa.
 
MAJIBU YA MZAHA HAYA

DODOMA: Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza serikali imefikia wapi kutafuta soko la Mbaazi baada ya msimu uliopita bei kushuka kutoka Tshs 2,000 mpaka 150

- Naibu waziri wa Kilimo, Eng. Manyanya amemjibu mbaazi ni chakula kizuri chenye protini na watanzania wanaweza kula wakati soko linatafutwa.
 
Back
Top Bottom