Waziri Magufuli apata PhD

Waziri Magufuli apata PhD

Watu wengi hapa JF wamemsifu sana Magufuli kwa kupata Phd hapo UDSM.
Kwa hiyo Mhe Nchimbi akipata Phd toka Mzumbe say,tushishangae sana.Naona kuna hypocricy hapa ,ni sawa kigogo kupata Phd Udsm lakini kuna watu watachallenge kigogo kupata Phd toka Mzumbe.

Thread yangu ni obectivity ya Phd ya Magufuli.labda mnaomjua zaidi huyu Mhe mtudokezee :
1.any standard Phd toka top class university ni 3 yrs for full time,na 5-6 yr for
for part time.Tunasikia Magufuli alichukua 3 yrs kumaliza tunaassume,alikuwa full time.Wote tunajua kipindi hiki alikuwa waziri !full time maana yake mwaka wa kwanza darasani,miaka 2 ni research na kupresent papers mbali mbali,au kuwa Tutorial assistant.
2.tunasikia supervise wake aliuwa classmate wake.je hapa kuna uhalali?
kwa sababu ni waizri mnategemea nani angesema ana walakini na research yake?


Hii trend imeanza kwa mawaziri kufanya Phd vyuoni!Kama Nchimbi na wenzake
wakipata Phd za Mzumbe watu wa UDSM msilalamike,maana trend imeanzishwa
na akina Magufuli.Miaka yote alikuwa wapi,mpaka awe waziri ndio awe na Phd?
Au ni kuwa sambamba na akina nagu,makogoro,matayo,dialo etc

wewe unachanganya mambo kinachomtofautisha Dr Magufuli na hao wa Mzumbe ni reseach yake aliyofanya ( alifanya utafiti na akagundua kitu ambacho kilikuwa hakijulikani) hapa ndo tunamsifia, ukumbuke uvumbuzi wake ni sifa hata kwa UDSM, sasa nakushangaa unapolinganisha PHD za Mzumbe na ya huyu bwana kwanza walimu kibao wa Mzumbe walikuwa na PHD feki naamini walichukuliwa hatua na TCU, wengine phd zao zilikuwa recategorized,Kwa nchi kama TZ usomi tunaouangalia ni ule ambao unaweza badilisha maisha ya mtanzania maskini, kumbuka finding ya dr magufuli tayari imeshaongeza value ya Korosho, mkulima ataweza uza korosho pamoja na maganda yake, kitu ambacho kilikuwa hakijulikani kabisa, sasa ndo unalinganisha na hizo za kina nchimbi na nagu ambazo hata title zao hazijulikani na hazina impact yeyote katika jamii???TUBADILIKE WABONGO NA TUACHE WIVU
 
Tumesikia supervisor wake alikuwa ni dr Nkunya!ni kweli ?kama kweli huyu mayunga ni wa TCU?sasa huyu atawezezaje ku sort out fake au political motivated Phd za wabunge na mawaziri?
 
ukumbuke uvumbuzi wake ni sifa hata kwa UDSM, ........, kumbuka finding ya dr magufuli tayari imeshaongeza value ya Korosho, mkulima ataweza uza korosho pamoja na maganda yake, kitu ambacho kilikuwa hakijulikani kabisa, sasa ndo unalinganisha na hizo za kina nchimbi na nagu ambazo hata title zao hazijulikani na hazina impact yeyote katika jamii???TUBADILIKE WABONGO NA TUACHE WIVU

Mkuu,

Unaweza ukatupasha habari zaidi juu ya uvumbuzi wa jamaa? Mbona hii sijaiona?

Mwaga hapa habari zake ili Ngosha asifiwe kwa kazi yake......
 
Sina wivu,tunataka integrity ya Phd tanzania!hujajibu hoja,ni Phd gani unasoma within 3 ,wakati wewe ni full time employee mwenye majukumu ?ukiwauliza watu wengi waliosoma Phd za uhakika toka top Uni duniani ,utaambiwa mwaka wa kwanza lazima usome full time.

Kama una maana kukaa lab mpaka saa saba ya usiku weekend(questionable) ndio full time ,basi hii ni bongo tu.
 
Hii trend imeanza kwa mawaziri kufanya Phd vyuoni!Kama Nchimbi na wenzake
wakipata Phd za Mzumbe watu wa UDSM msilalamike,maana trend imeanzishwa
na akina Magufuli.Miaka yote alikuwa wapi,mpaka awe waziri ndio awe na Phd?
Au ni kuwa sambamba na akina nagu,makogoro,matayo,dialo etc

Well; badala ya kuanza kuponda na kuuliza alikuwa wapi; Tumpongeze awe ameitoa Mzumbe ; UDSM jamani tuwapongeze ikiwa kweli vyuo vimetuthibitishia kuwa wamesomea hapo! Nchi hii ina wasomi wachache na ikifika mahali watu calibre hii wanasoma ni jambo la busara! Tache ushakunaku na tuone kuwa jambo jema ikiwa limeenda katika misingi ianyokubalika.
 
Umeme ukikosekana kwenye Train ya kati, lazima TANESCO ilaumiwe.... tetetetee 🙂

Sawa, hongera Dr. Kwani tofauti ya Docta na Prof ni ipi? Tuwape tu wote u-Prof na kijulikane kimoja. Prof. Kikwete, Magufuli, Mwakyembe, Makinda, Makongoro, Malecela, Makamba, Nchimbi, nk na wale wote wasiofundisha sasa kama Mwandosya, Sarungi,........................

SIKONGE
Udaktari ni cheo mtu anachotunukiwa baada ya kumaliza PHD yake, na PHD inachukua zaidi ya miaka MITATU kusomea, Kumbuka kabla ya kutunukiwa unatakiwa uitetee mbele ya JOPO la wataalamu waliobobea katika hilo eneo ulilostudy kumbuka unaweza ukawa umeandika vizuri na kufanya research ukishindwa kuitetea umekwenda na maji,,,,U professor kaka ni cheo, kama mtu anafanya kazi nje ya academic institution hawezi akawa professor, kwenye academi institution baada ya kupata PHD mtu unatakiwa UANDIKE academic papers, vitabu na presentaion kwenye mikutano mbali mabli from there wanatumia vigezo kukupandisha cheo kuanzia senior DR, Assocaiate Professor mpaka full professor, ambacho kwa Academic Institution ndo cheo cha mwisho kabisa, kwa taasisi nyingine kama una phd unapandishwa cheo kutokana na taratibu za taasisi au serekali, ukiwaona maprofessor ambao wako labda serekalini au kwenye taasisi au bunge jua kwamba wametoka vyuoni ndo wakaenda huko kama wakina Ndulu magembe nk

hope umenipata
 
Mkuu,

Unaweza ukatupasha habari zaidi juu ya uvumbuzi wa jamaa? Mbona hii sijaiona?

Mwaga hapa habari zake ili Ngosha asifiwe kwa kazi yake......


SIKONGE kama kuna sehemu nimegusia huo uvumbuzi wake, na hata ukienda pale UDSM Library ukiomba chapisho lake PHD thesis ya dr Magufuli ipo

Alichokivumbua ni namna gani Maganda ya Korosho yanaweza tumika kuondoa tatizo la KUTU. Ukimbuke Kutu na tatizo kubwa saana kwa nchi za ulimwengu wa kwanza hasa marekani,na kikubwa ni kwamba hayo maganda yakianza kutumika tayari mkulima wa kurosho atakuwa anauza korosho pamoja na maganda yake, so atapata faida mara mbili, Kumbuka yeye aliweza kuprove kabisa kwamba kisayansi kwamba maganda yakorosho yanaweza kutumika kuondoa hilo tatizo

ni swala la kujivunia na kumpongeza na sana saana UDSM hususani idara ya kemia wanatakiwa wapongezwe kwa kuweza kumwongoza vyema akaweza maliza utafiti wake ontime
 
zitto Kabwe anafanya Phd wapi?

Namnukuu Zitto kutoka huko ughaibuni

cleardot.gif
Zitto Zuberi Kabwe to wanabidii


s

Naomba nisahihishe tafadhali.

I am currently writing a PHD proposal and my admission depends on my the submission of it by May 2010 at WHU-Otto Beisheim School of Management. I am not a PHD candidate yet. At the time i am doing a second post graduate on Law and Business at Bucerius Law School in Hamburg and expecting to write on Fiscal stability clauses in mining agreements.

My PHD proposal so far is on Why Tanzania is yet to benefit from 10 years extraction of its mineral resouresces - testing the backward linakages (energy, transport and agri sectors).

So bado sana kujiita mwanafunzi wa PHD. Nanoa bongo tu kwa sasa!
 
Du!!
Kwa sasa bongo kila mwana siasa ni DR. kuna Dr JK,Magufuli mara mtasikia Lyatonga nae DR. wakati wenyewe wanaosota na machaki/projector/reseach kila siku kwa miaka 3 hadi 5 apo UDSM awapati kupewa DR.
Bongo kila kitu ni siasa ukitaka uwe na elimu kama DR kuwa mwana siasa,ukitaka hueshimiwe watu wakupishe kwenye ATM kuwa mwana siasa kama Ngeleja,ukitaka usishitakiwe kuwa mwana siasa kama Dito,ukitaka kuzulumu watu magari kuwa mwanasiasa kama Manaaaara. na mengine.
 
Hivi kama mtu hufundishi, kwa nini unajiita Dr?

Hivi ataanza kuandika vitabu na takataka nyingine ili kui-keep hiyo Dr au inabaki jina tu?

Hizi Tittle sasa zimekuwa za kwenda kuchumia uyoga msituni (bunsolele)...

Sikonge,
Kuwa Dr. Si lazima ufundishe. Dr. maana yake mtu amesoma, akafanya research na kupata PhD na unaweza kufanyakazi yoyote unayoipenda tokana na fani yako uliyosomea. Ila sasa ukitaka kuwa academician ndo sasa inabidi ufundishe na lazima uendelee kufanya utafiti na ku-publish tafiti zako hadi unafikia rank ya kuitwa Professor.
 
hahahaha
hahaha
hahahahaha...e bwana mkuu umenifurahisha sana!
kwamba dr. kikwete,dr.karume, dr.sofia simba, dr.mkapa..wakati hawa watu wengi wao wana certificates tu kina karume..lakini wanatunukiwa dr.;amazing!!!
safi sana magufuli,hata rais japokuwa huwa hakupendi ila anakukubali kimoyo moyo..wewe ni kichwa cha kutoka kanda ya ziwa..upo serious na kazi..hutaki longolongo kama za kina mawaziri wengine! hata kusoma reports tu kwenye media hawawezi..yaani simply kudessa inakuwa ni issue!!!wamepewa madaraka ki uswahiba tu
 
Wazee Magufuli ni kchwa na hilo ukilipinga hata samaki, ng'ombe na barabara zitapiga kelele na kusema acheni kuachama na kupayuka maneno ya hovyo hovyo.John is doing to his best.
 
thats goood, waooooooo! you'll never miss it even there so many kanjanjas in your way to success your whole life and your nation too through what you'v got
 
SIKONGE kama kuna sehemu nimegusia huo uvumbuzi wake, na hata ukienda pale UDSM Library ukiomba chapisho lake PHD thesis ya dr Magufuli ipo

Alichokivumbua ni namna gani Maganda ya Korosho yanaweza tumika kuondoa tatizo la KUTU. Ukimbuke Kutu na tatizo kubwa saana kwa nchi za ulimwengu wa kwanza hasa marekani,na kikubwa ni kwamba hayo maganda yakianza kutumika tayari mkulima wa kurosho atakuwa anauza korosho pamoja na maganda yake, so atapata faida mara mbili, Kumbuka yeye aliweza kuprove kabisa kwamba kisayansi kwamba maganda yakorosho yanaweza kutumika kuondoa hilo tatizo

ni swala la kujivunia na kumpongeza na sana saana UDSM hususani idara ya kemia wanatakiwa wapongezwe kwa kuweza kumwongoza vyema akaweza maliza utafiti wake ontime

Mkuu,
Mbona hili halitangazwi? Kwa nini asifanyiwe mahojiano na yakawekwa kwenye YOUTUBE ili kila mtu aone nini jamaa kakifanya na INCOME gani sasa Tanzania inaweza kuwa inapata?

Ni kweli tatizo la kutu ni kubwa sana. Sikuwa nafahamu kama jamaa alifanya ugunduzi huu. Ndiyo maana nikaomba uniwekee. Ingelikuwa vema utafiti wake uwekwe walau kwa muhtasari ONLINE ili tuwe tunampandishia chat jamaa.

MAGUFULI, kwa hili ngoja niungane na wengine kukupa HONGERA.

Ya kuitwa au kutokuitwa Dr. hili inategemea kama unafuata system za Kiingereza au laah. Wale jamaa kama hufundishi au hufanyi kazi za kitafiti, basi huwezi ukajiita Dr au Prof. Ndiyo maana mama Angela Merkel au Condoleese Rise au hata mtu kama Obama, hawajiiti Dr au Prof. kwa sababu hiyo. Ila sisi mwendo mmoja. Anyway, kama kwetu sisi ni sawa basi tuendelee.
 
He is really great teacher na kama ndiyo ilivyo alikuwa makini sana maana siku zote ni makini sana katika ufanyaji wa kazi
 
Hongera Magu ,uko tofauti na wale waheshimiwa waliofungiwa kwenye chumba special wakati wakifanya mitihani pale Openi Univasiti pale biafra
 
Jamani Dr. Magufuli sina shaka na kuipata PhD yake. Nilikuwa naye akimaliza Masters yake, na immediately baada ya Masters akagombea Ubunge na moja kwa moja kupata Uwaziri. In fact kugombea ubunge alikuwa akiongelea kwenye corridors za pale Hall IV na watani wake tukawa tunamwambia utapata kura moja tu - ya kwako. He is serious and hard working. Na kumbukeni kwamba PhD mtu anaweza kuendeleza research yake ya Masters na ikafanya apate PhD kwa muda mfupi sana. Wapo ma-genius kama kina Prof. Mwandosya ambao Masters zao zilipandishwa na kufanywa PhD kwa sababu zilionekana kuvuka kiwango cha Masters, na kufanya wapate PhD kwa muda mfupi. Na uzingatie kwamba hiyo PhD ya Prof. Mwandosya ilitolewa na Waingereza ambao wanajulikana kwa ukali wa shule. Kwa hiyo si razima PhD iwe minimum 3 years, na yes, PhD ukiwa Mkamba au Kipanga utaimaliza chini ya hiyo miaka mitatu.
 
Msomi mmoja maarufu alisema hivi, kama mvua inanyesha na haionyeshi kama imenyesha basi hakuna maana ya mvua hiyo kwepo.

Mhe. Magufuli siyo tu kwamba anajua anachokifanya bali kila anapopita anaacha "ATHALI HASI" Mfano:

1. Alipokuwa Waziri wa Ujenzi - Kajenga Nyumba ngapi ambazo Mawaziri wengine wala hawakuthubutu hata kuzifanyia Ukarabati zile zile zilizopo. BaraX2 ngapi amezisimamia na siyo hilo tu bali hata kujua urefu wake na maendeleo yake ya kazi yanavyoendelea.

2. Alipokuwa Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi, Tazama NHC ilivyobadilika kiutendaji hata Ofisi zao zilianza kubadilika.

3. Kapelekwa Mifugo na Uvuvi- Vile vyuo vyote vya Mifugo amevifufua, zile Ranchi zote za Taifa amezifufua.

Mimi sijuwi wengine wanashindwa Nini.

Waziri Magufuli namfahanisha na Mhe. Celina Kombani - Waziri wa Serikali za Mitaa kuna mengi ameyafanya katika Serikali za Mitaa tangu alipokuwa Mhe. Naibu Waziri na hadi sasa kuwa Waziri kamili. hao ndiyo watendaji tunaowataka.

No no no!Nasema no!Kumlinganisha Dr. John Pombe Magufli na Celina Kombani ni kumshusha hadhi John. Huyo Kombani tayari harufu za ufisadi zinamwandama katika sakata la Muro. No, No!John yuko Juu!
 
Back
Top Bottom