Waziri Kigwangalla amwaga baiskeli Nzega

Mwanasiasa anajali sifa na sio kuinua watu,
Kipi muhimu Kati ya hizo baiskeli au vizalisha uchumi
MZEE WA NJE YA BOX AMENIANGUSHA KABISA HAPA.

Na Thadei Ole Mushi.

Hebu tuachane na wanaolalamika Kigwangala kuanza kampeni mapema. Twende kwa hesabu ndogo tu hapa halafu tutajadili baadaye.

Kigwangala katoa baiskeli 780 ambazo ni sawa na shilingi milioni 156,000,000 (Milioni Mia Moja Hamsini na sita) Kama atauziwa kwa Bei ya chini kabisa ya Laki mbili kwa kila baiskeli.

Katoa pikipiki aina ya Boxer 40 Kama atakuwa kauziwa milioni mbili kila Moja atakuwa katumia milioni 80,000,000 (Milioni themanini)

Roughly atakuwa katumia milioni 236,000,000 (Milioni Mia Mbili thelathini na sita). Twendeni tu sawa, hapa kalipa tu dukani bado hajasafirisha, wajumbe Kama walikunywa soda na Chakula hayo Ni Mengine tusiyaweke hapa.

Kwa gharama za Kati katika tukio hili si chini ya Milioni Mia tatu. Narudia Tena kwa gharama za Kati kwa maana gharama hizi kwa jicho la kikampeni zitakuwa zimezidi.

Narudia twende sawa hapa.

1. Nzega vijiji tujiulize Kama Mbunge Ni vijana wangapi hawana Ajira amewawezesha hata kuwanunulilia pump za kuvuta maji za Laki na nusu zile ndogo kabisa?

2. Ni viwanda vingapi vya Kati kabisa alivyoweza kuvijenga hapa kwa ajili ya kupanua wigo wa vijana KUJIAJIRI?

3. Angeliamu Kununua Mashine za kukamulia alizeti kwa milioni 300,000,000 alizotumia Jana angeliweza Kununua Mashine 60 za milioni 5 kila mmoja ambazo Zina uwezo wa kuwaondoa vijana 360 Nyumbani kila siku asubuhi kwenda kazini. Labda Nzega vijiji Hakuna tatizo la Ajira.

4. Angeliamua tu kuanzisha vikundi vya kina mama kwa kuvipa tu milioni 5 kila kikundi tungekuwa na vikundi vipya 60 pale Nzega ambavyo vinagusa mamia ya wanafamilia.

Sitaki kujua fedha hizi kazitoa wapi Ila CCM ina hitaji Sana wabunge wanaowaza kwa maono. Viongozi ambao wataisaidia Serikali kuwaza namna ya kupunguza Umaskini, kupunguza tatizo la Ajira nk.

Tungepeleka hizi milioni 300 kwenye Elimu impact yake ni kubwa kiasi gani? Kwenye afya impact yake Ni kubwa kiasi gani?

Dr. Hamisi A. Kigwangalla Ni kiongozi kijana sikufikiria anaweza kufikiria kwa kiwango hiki.

Hebu tujiulize kwa mtoto wa mkulima pale Nzega vijijini anayetaka kugombea Ubunge anaweza kukivuka kizingiti hiki? Au huku ndio kutumia dola kubaki kwenye Dola?

Sijui Ila bado CCM Kuna kazi kubwa Sana ya kutenganisha uwezo wa Fikra na uwezo wa kifedha. Otherwise tuendelee tu hivyo hivyo....hebu tupime pikipiki hizi na baiskeli za wajumbe wa CCM Nzega zinawagusaje kina mama na Vijana.

Ole Mushi
0712702602.
 
Back
Top Bottom