Waziri Kagasheki ajiuzulu; David Mathayo, Nchimbi na Nahodha watimuliwa na Rais Kikwete!

Wizara ya mambo ya Ndani chini ya nchimbi mauaji mengi ya kisiasa yalitokea akiwa WAZIRI. NCHI ZENYE UWAJIBIKAJI HUYU ALITAKIWA AENDE JELA NA KAZI NGUMU. HUYU KATIBU MKUU WA ZAMANI WA UVCCM KAMA SIJAKOSEA. ALIKUWA ANAFANYA KAZI ZA MAGAMBA KUTESA/KUUMIZA WOTE WALIOKUWA WANA MAWAZO TOFAUTI NA WATAWALA. HATA MAUAJI YA MWANGOSI YEYE NDIE ALIKUWA WAZIRI HUSIKA. SOWETO/MVUNGI. LAANA YA DAMU ZA WATZ ZILIMWAGIKA ZITAKUTAFUNA KOKOTE UENDAKO. KAMA ULIJUA AU KUSHIRIKI. ALICHELEWA SANA KUFUKUZWA.
 
Ina maana huwa hawajui kinachoendelea mpaka kwa style ya ushabiki ndio tunaona uwajibishwaji
 
Sasa kama yako moyoni mwake wewe umeyajuaje ama Shehe Yahya wewe?
 
Dar es Salaam/Dodoma. Rais Jakaya Kikwete leo ametengua uteuzi wa mawaziri wanne kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.

Mawaziri waliopoteza ajira zao usiku huu ni pamoja na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT).

Akizungumza Bungeni Dodoma usiku huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kulikuwa na matatizo makubwa katika usimamizi wa zoezi hilo.

“Tulifanya operesheni kwa nia nzuri,” alisema Waziri Mkuu Pinda. “Tatizo ni namna operesheni hiyo ilivyotekelezwa.”

Katika mdahalo uliogusa nyoyo za wabunge na wachambuzi mbalimbali wa siasa leo, wabunge waliueleza umma jinsi ambavyo Operesheni hiyo ilitumika kutesa, kunyanyasa na kuua raia wasio na hatia na kuwadhulumu mali zao.

Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi.

SOURCE:MWANANCHI
 
TUMEFIKA HAPA, NA TUTAENDELEA KUVUNA HASARA NA VIFO KWA SABABU YA UDHAIFU WA JK.... AWAMU YA NNE HII SASA NCHI INANINGIA HASARA TU

JK NI TATIZO.. HUWEZI KUCHAGUA WATU KWA USWAHIBA USHWAHIBA.. TAZAMA YA MULUGO?? TAZAMA MAMBO YA KAWAMBWA... USANII WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA,,,...?? ANGALIA MAGUMASHI YA WIZARA YA ARDHI.. HADI LEO VIWANJA VYA WAZI VINAUZWA UZWA TU.. NO SERA NO WHAT??

KUJIUZURU NI JAMBO MOJA,.. JE HASARA NA MAUTI NA VILEMA WALIVYOWASABISHIA WATANZANIA INAKUWAJE??


hawa watetea uovu wa Lumumba sijui wako wapi leo... Cc. Faiza foxy, taswira , wingu, simiyu yetu, msalani.. Ritz.. et al...

Ngoja niwatumie summons wasijekusema kuwa hawakualikwa...Cc.FaizaFoxy, Taswira , Wingu, Simiyu Yetu, MSALANI.. Ritz.. et al..
 
Wakati waziri Hamisi kagasheki alipotangaza kujiuzuru leo bungeni, mawaziri wengine wanne ambao ni Emannueli Nchimbi, Mathayo David, wafukuzwa kazi rasmi na rais.

source. startv
 
Mkuu hili nalo ni bonge la zigo. Sijui kama mipango yake ya kugombea urais wa Tanganyika bado iko pale pale au atakuwa amebadili mawazo. Kama kuna wanasiasa waliokosa mvuto nchi hii nadhani huyu chakubimbi anaongoza.
 
Ndio maana naipenda CCM na nitaendelea kuipenda Daima kwani
wiki mbili zijazo mkuu wa kaya na yule mkuu wa mawaziri
nao watatangaza kujiuzulu, nafikiri huu utakuwa uwajibikaji mkubwa zaidi kuwahi
kutokea.
 
Back
Top Bottom