mwangalizi
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 842
- 512
Hapana, Wakati wa Tanganyika hayakuwepo hayo. Madhila ya nchi hii yalianza baada ya kuwa Tanzania na to be precise yameanza baada ya kutangazwa na Nyerere Azimio la Arusha mwaka 1967.
OK. Tuseme labda madhila yalianza baada ya kuwa na Azimio la Arusha (unahitaji kunichambulia kwa kina); kisha unieleze vizuri ni mazuri yapi yametokana na azimio la Zanzibar (lililopiga chini misingi ya azimio la Arusha).
1. Je, kwako jambo zuri na jema na ambalo linakupa usingizi murua ni viongozi kuwa na hisa kwenye makampuni ya kibepari na majumba (siku hizi MAKASRI) ya kupanga?
2. Je, ni kweli kwamba huoni athari za mambo haya ya zanzibar? Ni kweli kwamba hujamsikia mzee wa vijesenti? Ni kweli kwamba hukumsikia mzee wa richmond, aliyehujumu uzalishali wa umeme ili kila siku iendayo kwa Mungu awe anatengeneza zaidi ya 150m? Akaunti za vigogo (japo vigogo vya udongo maana hawatadumu) huko uswisi wewe hujasikia? Mahoteli makubwa makubwa ndani na nje ya nchi kutokana na fedha chafu, za wizi, dhuluma na damu za watanzania hujui? Ndiyo mambo yanayokupa usingizi murua dada Faidha Foxy?
3. Unachukizwa na kauli ya kwamba IKULU SI PANGO LA WANYANG'ANYI? ama KUTOKUCHANGANYA BIASHARA NA UONGOZI? Lakini ndivyo ilivyo, unataka ama hutaki! Yasipozingatiwa haya madhila yatazidi kuongezeka. Na yanapoongezeka utambue ya kwamba UKOMBOZI upo karibu! Mjusi ukimfukuza sana hugeuka kuwa NYOKA! Siyo yangu haya, ni historia tu, na historia hujirudia. Kuna watu humu nchini itafika wakati hata ndevu hawatanyoa! Maana watakuwa wanawindwa kama wanyama! Ukipata bahati ya kukutana na Gadaffi atakupa mkanda mzuri. Ama wadhani viongozi wetu wametutenda mambo mazuri kuliko Gadaffi?