Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara

Nilishawahi kuandika hapa huyu Magufuli ni bomu tu kutokana na maamuzi yake mbali mbali hasa katika awamu ya tatu na hii pia. Afadhali nawe umeona hivyo. Inaelekea hakuna aliyeiba password yako. Napenda kusoma michango ya huyu Mwiba mpya na siyo yule wa zamani aliyekuwa anapigia debe uozo wa Chama Cha Mafisadi/Majambazi. Hongera sana kwa kuamua kubadilika.
 
Nakumbuka msemo wa kikwetu usemao "...Ukimsifu mgema tembo hulitia maji...! Magufuli amesema yale majumba ya shirika la umeme yanayoleta mandhari ya aina yake hapa jijini yaliyojengwa kwa mabilioni ya shilingi ni lazima yavunjwe eti yamejengwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya kupita barabara.

Huyu mtu kama hana wazimu atakuwa na kitu gani hivi anafikiria hela iliyotumika ni hela ya serikali, ? Au ya shirika la umeme ,akili za watu wengine zinakuwa za ajabu ajabu ,anachotaka ni kuwapa tanesco eneo jingine wajenge upya ,kwa maana kwa dau hilo hela ingine itapatikana na wajanja kupata chao.

Mtu huyu alikuwa wapi wakati majumba hayo yakijengwa ?Serikali ilikuwa wapi ?
Tanescobuild.jpg
Unaenda kuvunja mijumba hiyo kwenye nchi ambayo uchumi wake ni wa kubahatisha au wakuu mnataka na kutafuta njia mbadala ya kufanya ufisadi,
Huyo jamaa sijui!
 
Mnatoka mapovu tu,hao watu wa mipango miji waliruhusu vipi hilo jengo kujengwa hapo wakat mji unatanuka??basi nawashauri wabomoe kote na watupe mahema tuanza kujenga upya
 
Pascal Mayalla naona unasogeza kisu kwenye mfupa na kufanya chanuo lichome. Kila kitu kina ubaya na uzuri wake! Zama hizi za kupimana mikojo na matamko kama watu wana undugu na mumiani, haya mambo hayawezekani hata kwa kuota ndoto tu (Kama Lema).
 
Nakumbuka msemo wa kikwetu usemao "...Ukimsifu mgema tembo hulitia maji...! Magufuli amesema yale majumba ya shirika la umeme yanayoleta mandhari ya aina yake hapa jijini yaliyojengwa kwa mabilioni ya shilingi ni lazima yavunjwe eti yamejengwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya kupita barabara.

Huyu mtu kama hana wazimu atakuwa na kitu gani hivi anafikiria hela iliyotumika ni hela ya serikali, ? Au ya shirika la umeme ,akili za watu wengine zinakuwa za ajabu ajabu ,anachotaka ni kuwapa tanesco eneo jingine wajenge upya ,kwa maana kwa dau hilo hela ingine itapatikana na wajanja kupata chao.

Mtu huyu alikuwa wapi wakati majumba hayo yakijengwa ?Serikali ilikuwa wapi ?
Tanescobuild.jpg
Unaenda kuvunja mijumba hiyo kwenye nchi ambayo uchumi wake ni wa kubahatisha au wakuu mnataka na kutafuta njia mbadala ya kufanya ufisadi,

Jamani huyu mpumbavu wa wapi au Lofa
 
Sasa sijui anasubiria nini kuiporomosha hilo jengo kama anavyo vunja za wengine
 
Sio kwa majumba yaliyojengwa kwa fedha ya wananchi.Tena majumba yenyewe yanajionyesha ni ya bei au gharama kubwa sana. Unaweza kufanya quantity survey hapo au just estimation ni shilingi ngapi za kiTanzania zilitumika.
Inawezekana CCM wapo kwenye mikakati ya kuipa shida serikali itakayokuja badala yao.

Hela, za, wananchi zimejenga tanesco ila nyumba za billion moja za, mama kawa wa mbezi kibanda cha mkaa ni za, shetani
 
Hifadhi ya Barabara ni kwa sababu ya public services and utilities ikiwema; umeme, maji, simu, internet, mobile toilets, e.t.c. Jengo la TANESCO ni public services kwa maana kwamba wameamua badala ya kuweka nguzo za umeme waweke sehemu ya ofisi yao ili kurahisisha public service, sasa mzee Pombe atuambia anataka kuondoa public service and utilities ili public ipate wapi huduma?
Kwa hiyo kwenye road reserve ukijenga zahanati hapana maneno!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akivunja hili jengo nitamwona punguani!
Kuna tatizo gani hiyo barabara ikikwepeswa? Kama ana ubavu Ajenge ipite chini au juu. kama ni lazima ipite hapo.
Sheria ni msimeno. Zimevunjwa nyumba za walala hoi walio zijenga kwa jasho lao hadi wengine wamefariki kwa mishtuko, na nyumba zao zilikuwa kwenye maeneo SAHIHI bila ya kuvunja Sheria lakini hamkupiga kelele Leo watu wamejenga NYUMBA bila kwa jasho letu na bado wana Majumba mengine na wana Bima kubwa kwa Majumba yao. Kama Shelia imevunjwa basi itumike Sheria hiyo hiyo kuweka usahihi unaotakiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sure mkuu, nilisikia kuna wasaidizi wa kikwete wanafurahia wananchi wakiichukia serikali yao, magufuli amepiga x hata kwenye nyumba zilizofuatwa na barabara na inasemekana hazitalipwa. Joto bado si dogo sasa mh magufuli analiongeza hata kwa wananchi waliokuwa kimya. vijijini nyumba zimepigwa x na wameambiwa ndani ya mwezi na hakuna malipo
Hiyo "inasemekana hazotalipwa" kasema nani au umbea wako na fitna??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom