Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri John Magufuli hili la kuvunja jengo la TANESCO Ubungo tumia busara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Mar 1, 2011.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka msemo wa kikwetu usemao "...Ukimsifu mgema tembo hulitia maji...! Magufuli amesema yale majumba ya shirika la umeme yanayoleta mandhari ya aina yake hapa jijini yaliyojengwa kwa mabilioni ya shilingi ni lazima yavunjwe eti yamejengwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya kupita barabara.

  Huyu mtu kama hana wazimu atakuwa na kitu gani hivi anafikiria hela iliyotumika ni hela ya serikali, ? Au ya shirika la umeme ,akili za watu wengine zinakuwa za ajabu ajabu ,anachotaka ni kuwapa tanesco eneo jingine wajenge upya ,kwa maana kwa dau hilo hela ingine itapatikana na wajanja kupata chao.

  Mtu huyu alikuwa wapi wakati majumba hayo yakijengwa ?Serikali ilikuwa wapi ?
  [​IMG]Unaenda kuvunja mijumba hiyo kwenye nchi ambayo uchumi wake ni wa kubahatisha au wakuu mnataka na kutafuta njia mbadala ya kufanya ufisadi,
   
 2. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijaluelewa mkuu, unajaribu kusema kwamba nikitumia pesa nyingi sana kuvunja sheria inabidi sheria itupwe ili mimi nisiwe nimepata hasara kwa kuvunja kwangu sheria?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sio kwa majumba yaliyojengwa kwa fedha ya wananchi.Tena majumba yenyewe yanajionyesha ni ya bei au gharama kubwa sana. Unaweza kufanya quantity survey hapo au just estimation ni shilingi ngapi za kiTanzania zilitumika.
  Inawezekana CCM wapo kwenye mikakati ya kuipa shida serikali itakayokuja badala yao.
   
 4. w

  warea JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Akivunja hili jengo nitamwona punguani!
  Kuna tatizo gani hiyo barabara ikikwepeswa? Kama ana ubavu Ajenge ipite chini au juu. kama ni lazima ipite hapo.
   
 5. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa ana wazimu sio kidogo, hao wazembe wa serikali waliopitisha ujenzi wa hilo jengo wako wapi? Wamechukuliwa hatua gani?

  Au kwakuwa hayo majengo yamejengwa na kodi ya mwananchi basi inakuwa ni rahisi kuyavunja? Akavunje nyumba zake huko chato na dar..hili swala ni zito sana,badala ya serikali kufikiria maendeleo ya kujenga flyover eti wao wanafikiria kuvunja! Nasema siku atakapoamua kuvunja lile jengo kwa huo wazifa wake wa muda,atakuja kujutia maisha yake yote..I mean it.
   
 6. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hifadhi ya Barabara ni kwa sababu ya public services and utilities ikiwema; umeme, maji, simu, internet, mobile toilets, e.t.c. Jengo la TANESCO ni public services kwa maana kwamba wameamua badala ya kuweka nguzo za umeme waweke sehemu ya ofisi yao ili kurahisisha public service, sasa mzee Pombe atuambia anataka kuondoa public service and utilities ili public ipate wapi huduma?
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ama umekwepa kujibu swali langu au ni swali gumu kidogo kwako
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyie mbona mnadiscuss ujinga? mnalijua lile gorofa la masaki lililobomolewa kwa kuwa kule hakukutakiwa kuwepo jengo lefu kama lile? mnajua gharama za jengo lile? Nyie ni wafuasi wa serikali ambayo inawaonea wananchi na nyie mmekubali. Sheria haijalishi serikali au mtu binafsi. Unaponibomolea kijumba changu kidogo ni sawa na yule unayembomolea gorofa. Mmeshafanya projection in twenty five years mahitaji ya ile bara bara yatakuwaje?
  Magufuli yuko sawa myie ndio mmepotoka
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa kwa kina ila jibu langu limekupita.
  Huwezi kusema sheria imevunjwa wakati kwa kujengwa Jumba hilo ,bia ya shaka yeyote ile hizo landmark za zinjia au hiyo master plan ilikuwepo kabla ya jumba hilo au sio ? Kama ni hivyo majengo hayo ni lazima yapitie katika idara kwa kupasishwa na kama kuna kizingiti chochote kile ,ujengaji huwa hauruhusiwi ,kumbuka tu aliejenga hapo si mwananchi anaekaa karibu na mipaka ya njia badala ya kuona kwa muda mrefu barabara haijajengwa akaamua kujenga,pengine na alama za upitishaji njia akazing'oa,majumba hayo yamejengwa kwa baraka zote za serikali iliopo madarakani,iweje leo hukohumo ndani ya serikali azuke mtu aseme ni lazima majumba hayo yavunjwe? Hivi serikali yeti ina uwezo gani wa kuyafanya hayo yote ?
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mwiba Mozambique hawajambo?
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kama yanakiuka sheria za mabarabara hayana budi kuvunjwa.sheria ni msumeno inakata kotekote.nyie ndo wale mnaosema kwa kuwa mabango ya barabarani yanaingiza fedha basi yaachwe hata kama yanakiuka sheria na ushauri wa kitaalamu.
  Songa mbele magufuli fuata sheria.
  Work as a binary system...0 or 1
   
 12. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  sure mkuu, nilisikia kuna wasaidizi wa kikwete wanafurahia wananchi wakiichukia serikali yao, magufuli amepiga x hata kwenye nyumba zilizofuatwa na barabara na inasemekana hazitalipwa. Joto bado si dogo sasa mh magufuli analiongeza hata kwa wananchi waliokuwa kimya. vijijini nyumba zimepigwa x na wameambiwa ndani ya mwezi na hakuna malipo
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Strategically, kama majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe.

  Kabla ya kumwona Magufuli hana akili ni lazima wote mnaopinga uamuzi wa Magufuli kujiuliza maswali.

  Hivi ni nani aliyeamuru ujenzi wa majengo haya ya mabilioni bila kukaa chini na kupanga kila kitu kikamilifu??
  Master plan ionyeshayo eneo la Barabara ilichorwa mwaka gani?
  Kama Master plan ilikuwepo kabla ya ujenzi wa barabara ni kwa nini Tanesco iliendelea na ujenzi katika eneo la barbara? Ni kwa nini serikali haikuizuia Tanesci kujenga akatika eneo la barbara?

  Eneo la Ubungo ni Entrence na Exit kuu ya jiji la Dar, kama kwa namna yeyote ile majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe kupisha upanuzi wowote wa barabara uiliopangwa hapo awali. Comparatively thamani ya majengo hayo ni ndogo sana ukilinganisha na hasara itakayosababishwa ya kuzuia upanuzi wa barabara.


  Kama kwa akili zenu mnamuona Magufuli ni Punguani kwa kushikiria msimamo wake wa kubomoa majengo yote yaliyomo katika eneo la barabara! Mnamuonaje na mtamwita jina gani mtu aliyeng'ang'ania kujenga majengo ya thamani kubwa katika eneo la barabara?

  Kulikuwa na Busara gani kujenga majengo hayo ndani yana eneo la barabara??

  Ni nani aliyekuwa Waziri wa wizara husika wakati wa ujenzi huo?? Na ninani aliyekuwa Bosi wa Tanesco wakati huo??

  Serikali ya CCM ilikuwa wapi na mastar plan yake wakati Tanesco wakijenga katika eneo la barabara??

  Kipimo na Ujinga,Upunguani Uhuni na Utovu wa Nidhanmu Tanzania ni nini??

  Magufuli ni Punguani, aliyesimama kidete kujenga katika eneo la barabara tutamwitaje??


   
 14. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka huna point pumzika, ungana na mameya wa Dar kufanya uchafu wenu. Kama serikali iliyopita ilifanya makosa lazima sasa yasahihishwe sio yabaki kama yalivyokuwa. Na impact ya hilo jambo ina maana ukiwavunjia wananchi utakuwa ni uonevu mkubwa sana. Magufuli is right, nyie wenye uelewa huo ndio mmepotoka.
   
 15. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa anatakiwa ku focus attention yake kwenye kujenga barabara. Badala yake sasa ana focus attention yake yote kwenye kubomoa majengo ambayo yamekuwepo hapo kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Huu ni wenda wazimu!
   
 16. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka hawa ni wale wenye point nyepesi kama mameya wa Dar, hivi mnasimamia wapi kusema hayo msemayo? Sheria inasemaje kuhusu hilo jambo? ile barabara baada ya miaka kama ishirini kutakuwa na need ya kupanua mpaka kule na bado gari zitakuwa hazitoshi. Mimi namuona magufuli kama ni kiongozi mwenye vision nzui sana katika taifa, hawafikirii nyie tu hapa ila na vizazi vyenu vijavyo
   
 17. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sasa barabara ajenge wapi? hivi nyie mnafikiria kweli? ajenge juu ya majengo?
   
 18. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kwamba ni uendawazimu kubomoa majumba ya gharama kubwa kama lile la Tanesco Ubungo, eti kwa sababu tunataka barabara inyooke. Hata kama majumba hayo yanamilikiwa na watu binafsi, ni hasara kwa taifa kwani yakijengwa mengine gharama za ujenzi zitaongezeka na sisi wananchi tuta-suffer. Mengi ya haya majengo yaliidhinishwa na Serikali hii hii.

  Huku kukurupuka kwa Magufuli na mawaziri wengine wa aina yake, kunadhoofisha uchumi wetu. Hivi Baraza la Mawaziri halijadili mambo kama haya ambayo yanaweza kuongeza gharama kwa taifa?

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mustapha Mkullo ana jukumu la kuhakikisha mipango ya Serikali inatekelezwa kwa namna ya kutokuongeza mzigo usio wa lazima kwa walipa kodi. Tunaomba uwadhibiti wenda wazimu kama Magufuli.
   
 19. coby

  coby JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ile ni mali ya umma aisee, kama ipo barabarani ni lazima ibomolewe aisee ila aliyetoa kibali cha kulisimika pale lazima awajibike aisee kwani ni hela mingi sana ile, approximately 16billion!
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama hilo jumba ni la mtu binafsi hakuna tabu kwani itakuwa ametoa rushwa ili kupata kibali cha ujenzi na haswa ilivyokuwa kuna uhakika wa kutotakiwa majumba marefu,haya majumba ya Tanesco sidhani kama kutakuwa na rushwa zaidi ya ufisadi na kuyavunja na bila ya shaka kutahitajiwa kujengwa tena sehemu nyingine ,hiyo hela hapo ni ya walipa kodi ,Tanzania ni kubwa sana na bara bara na future plan inawezekana kupindishwa kuliko kulitia hasara Taifa, Kama Makufuli anataka kuyavunja hayo majumba basi ni lazima afanye uchunguzi na kulijulisha Taifa ilikwendakwendaje hata majumba hayo ikawezekana kujengwa hapo ili hao wahusika walipe gharama za majengo hayo na gharama za uvunjaji,hii sio nchi ya Magufuli peke yake ,afanye kila kitu vile aonavyo yeye,hilo haliwezekani ,ila ikiwa yeye anamiliki kampuni za uvunjaji majumba,sasa napata wasiwasi kuwa kampuni za kuvunja majumba ni za kwake au hela inayotumika kuvunja majumba na yeye anachota zake na kuwalipa matingatinga hela ya chai.
   
Loading...