Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,426
8,240
Your browser is not able to display this video.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewakabidhi magari mapya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kwa maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Majeshi Wastaafu waliokabidhiwa magari ni CDF Mstaafu George Waitara na Robert Mboma na makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi Mtumba Jijini Dodoma


Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.

“Wakuu hawa wa Majeshi Wastaafu walifanya kazi kubwa na iliyotukuka kipindi cha utumishi wao kwa Nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan imewapatia magari na kuwatakia kheri na maisha marefu Majenerali Wastaafu hawa.”


 
Mbona huyu wa juzi kazi Mwamunyange yeye hajakabidhiwa? ama yeye utaratibu wake uko tofauti? ila kwa nchi masikini kama bomgo kuendelea kukumbatia haya mashangingi ambayo ulaya yanamilikiwa na matajiri wakubwa tu ni kuendelea kuwa masikini tena masikini hohehahe.
 
Amina. Aliyenacho......
 
Huwa wanapewa kwa mujibu wa sheria tangu enzi za Mzee Mkapa na hupewa baada ya miaka kadhaa ( kutaja miaka husika ni kosa)

hao wengine tangu wapewe mapya hawajamaliza ule muda wa depreciation kwa mujibu wa sheria
Kutaja miaka ni kosa, hapa una refer to kifungu gani? Kindly share hicho kifungu, au kushare hicho kifungu cha sheria nayo ni kosa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…