Waziri Bashungwa: Diaspora Tusisahau Kuwekeza Nyumbani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WAZIRI BASHUNGWA: “DIASPORA’ TUSISAHAU KUWEKEZA NYUMBANI”

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wazawa wa Kagera wanaoishi nje ya mkoa pamoja na nje ya nchi 'Diaspora' kuja kuwekeza mkoani humo kwani Serikali imeshaweka mazingira wezeshi na rafiki ya Uwekezaji.

Ametoa wito huo tarehe 25 Disemba 2023 katika ibada ya Krismasi katika Parokia ya Bikira Maria Mbarikiwa Bushangaro - Nyakaiga, Karagwe mkoani Kagera iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padri Edward Rwechungura pamoja na Padri Georges Kimonges.

" 'Diaspora' pamoja na Majukumu ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na mikoani lakini tusisahau kuwekeza nyumbani na niwapongeze Wanakagera wanaoendelea kuwekeza katika mkoa wetu” - amesema Bashungwa.

Waziri Bashungwa amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo mkoa Kagera ambao unaendelea kuunganishwa na nchi jirani kwa ujenzi wa barabara za lami.

“Kwa mfano kwetu sisi ukanda wa Bushangaro, mawasiliano ya barabara hayakuwa mazuri lakini barabara zinazidi kuboreshwa na 'Diaspora' mnapokuja mmekuwa mkinipigia kunieleza mambo yalivyobadilika” - amesema Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Kagera kuendelea kumuunga mkono na kumuombea afya njema, Mheshimiwa Ras, Dkt. Samia Suluhu Hassn ili azidi kutenda kazi yake ya kuletea maendeleo ambapo amesema kazi ya kuwahudumia wananchi ni ngumu hivyo inahitaji maombi ambayo yatamlinda na kumsaidia kuzidi kuwa na hekima na busara katika uongozi wake.

Katika Mahubiri, Padri Georges Kimonge amekemea tabia ya vijana kujihusisha na matendo yasiyompendeza Mungu hususan suala la kutoa Mimba ambapo amesema si jambo zuri kuua kiumbe ambacho Mwenyezi Mungu amepanga kukileta duniani kwa sababu maalum.

"Unapotoa mimba unamtoa Rais, unamtoa Waziri Mkuu, unamtoa Mfalme lakini vile vile silaumu akina mama wanaotoa mimba lakini akina Baba ndio mnaowapa hizo mimba akija akikwambia nina mimba unatumia lugha anasema nina mzigo kwa hiyo mama akienda kutoa mimba anaona ametoa mzigo"- amesema Padri Kimonge.
 
Attachments

  • GCL6pOUWsAAn8eK.jpg
    GCL6pOUWsAAn8eK.jpg
    151.5 KB · Views: 3
  • GCL6qR3XQAAervM.jpg
    GCL6qR3XQAAervM.jpg
    331.6 KB · Views: 1
  • GCL6qR3WYAAhT7g.jpg
    GCL6qR3WYAAhT7g.jpg
    313.9 KB · Views: 2
  • GCL6qRwXkAAVau2.jpg
    GCL6qRwXkAAVau2.jpg
    410.3 KB · Views: 2
  • GCL6rUpW8AAisQD.jpg
    GCL6rUpW8AAisQD.jpg
    224.5 KB · Views: 1
  • GCL74OJXgAAjnjC.jpg
    GCL74OJXgAAjnjC.jpg
    289.1 KB · Views: 1

WAZIRI BASHUNGWA: “DIASPORA’ TUSISAHAU KUWEKEZA NYUMBANI”

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wazawa wa Kagera wanaoishi nje ya mkoa pamoja na nje ya nchi 'Diaspora' kuja kuwekeza mkoani humo kwani Serikali imeshaweka mazingira wezeshi na rafiki ya Uwekezaji.

Ametoa wito huo tarehe 25 Disemba 2023 katika ibada ya Krismasi katika Parokia ya Bikira Maria Mbarikiwa Bushangaro - Nyakaiga, Karagwe mkoani Kagera iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padri Edward Rwechungura pamoja na Padri Georges Kimonges.

" 'Diaspora' pamoja na Majukumu ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na mikoani lakini tusisahau kuwekeza nyumbani na niwapongeze Wanakagera wanaoendelea kuwekeza katika mkoa wetu” - amesema Bashungwa.

Waziri Bashungwa amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo mkoa Kagera ambao unaendelea kuunganishwa na nchi jirani kwa ujenzi wa barabara za lami.

“Kwa mfano kwetu sisi ukanda wa Bushangaro, mawasiliano ya barabara hayakuwa mazuri lakini barabara zinazidi kuboreshwa na 'Diaspora' mnapokuja mmekuwa mkinipigia kunieleza mambo yalivyobadilika” - amesema Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Kagera kuendelea kumuunga mkono na kumuombea afya njema, Mheshimiwa Ras, Dkt. Samia Suluhu Hassn ili azidi kutenda kazi yake ya kuletea maendeleo ambapo amesema kazi ya kuwahudumia wananchi ni ngumu hivyo inahitaji maombi ambayo yatamlinda na kumsaidia kuzidi kuwa na hekima na busara katika uongozi wake.

Katika Mahubiri, Padri Georges Kimonge amekemea tabia ya vijana kujihusisha na matendo yasiyompendeza Mungu hususan suala la kutoa Mimba ambapo amesema si jambo zuri kuua kiumbe ambacho Mwenyezi Mungu amepanga kukileta duniani kwa sababu maalum.

"Unapotoa mimba unamtoa Rais, unamtoa Waziri Mkuu, unamtoa Mfalme lakini vile vile silaumu akina mama wanaotoa mimba lakini akina Baba ndio mnaowapa hizo mimba akija akikwambia nina mimba unatumia lugha anasema nina mzigo kwa hiyo mama akienda kutoa mimba anaona ametoa mzigo"- amesema Padri Kimonge.
Wapeni Diaspora Haki zao acheni kumungunya mineno wawekeze wakati haki yao ya uraia hamuithamini!.
 
Kila mwana diaspora anataka kuwekeza kwao tatizo serikali haiwapi haki ya kuwa wamiliki wazawa. Kuna wakati naona wakenya wana huruma sana na raia wao kuliko sisi watanzania serikali haijali wazawa kabisa.
 
Back
Top Bottom