Waziri Ghasia aumbuliwa na Mkurugenzi LAPF kwa kumdhalilisha Mbowe kukopa mabilioni ya pesa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250


  • LAPF yakana kumdai Mbowe
  • Yaruka kuwasaidia Msigwa, Mbilinyi

Waziri Ghasia aumbuka SIKU chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kusema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amekopa kiasi cha sh bilioni moja kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Eliud Sanga, amekanusha.

LAPF pia imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini, Peter Msigwa, kama ilivyosemwa bungeni.

Juzi, Ghasia alisema kuwa Mbowe anadaiwa sh bilioni moja na LAPF na ametumiwa waraka wa kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Waziri huyo alisema si kosa kwa wabunge kupewa fedha na LAPF, lakini ni kosa kwa mbunge kutorejesha fedha alizokopeshwa.

Kauli ya LAPF

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Sanga, alibainisha kuwa LAPF haijawahi kumkopesha Mbowe sh bilioni moja, na kwamba mfuko huo hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo.

"Mfuko wa LAPF hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo na wanachofanya ni kutoa mikopo ya wanachama wake kupitia vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na mikopo ya nyumba kwa wanachama wanaokaribia kustaafu," alieleza Sanga.

Alisema shughuli kuu za mfuko huo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, uwekezaji na kulipa mafao.

"Ieleweke kuwa ingawa waheshimiwa wabunge au mtu au taasisi yoyote hazuiliwi kuomba msaada wa kijamii, Mbilinyi na Msigwa hawajawahi kuwasilisha maombi na hawajawahi kupewa msaada wowote na LAPF.

"Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mbalimbali Mei 26 ambapo gazeti mojawapo lilikuwa na kichwa kilichosema ‘Waheshimiwa wabunge ni wasumbufu na kumfanya Mkurugenzi Mkuu asiende bungeni' si za kweli," alisema.

Alibainisha kuwa pamoja na majukumu hayo, mfuko unashiriki katika kuisaidia jamii kupunguza umasikini na kuchochea maendeleo.

"Misaada hii ina lengo la kusaidia jamii yote ya Watanzania yenye mahitaji mbalimbali kwa kutambua kuwa misaada hii itawanufaisha si wanachama wa LAPF tu bali wananchi wote na kwamba imekuwa ikitoa misaada ya kijamii kwa wananchi wote.

"Imekuwa ikitoa misaada ya kijamii katika sekta mbalimbali kama vile sekta ya afya, elimu, vituo vya watoto yatima, kusaidia mashuka, vyandarua na dawa kwa watu wanaokumbwa na maafa," alisema.

Aliongeza kuwa LAPF wamekuwa wakichangia elimu kwa kujenga madarasa, ununuzi wa madawati na vifaa vya maabara.

Hata hivyo, alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 LAPF imetoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na vifaa vya ujenzi katika Chuo cha Madaktari Bugando na Chuo Kikuu Huria (OUT).

Alisema kuwa LAPF haizuii taasisi yoyote kuomba msaada wa kijamii kwa kuwa hutoa misaada mbalimbali kwa kuzingatia mpango wa bajeti iliyoidhinishwa kwa kuzingatia sera ya misaada ya kijamii na maombi yaliyowasilishwa.

Sanga, alisema hata taasisi au mtu hapewi fedha mkononi taslimu, bali LAPF inanunua vifaa na kuwasilisha moja kwa moja kwa wahusika.

Source: Tanzania Daima
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,416
2,000
mbona mh LUKUVI alisema mjengoni kuwa hata yeye amekopa hapo kwahiyo sio jambo la kubishania. inamana yeye nae hadaiwi?
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mbowe anasema alikopa NSSF, huyu naye anasema hajamkopesha?. Aliyekopa anasema amekopa. Hii ni sawa na kusema, mwizi anasema aliiba lakini aliyeibiwa anasema hakuiba!. Hoja ni kwamba, anadaiwa na mifuko ya jamii.

Siwezi kushangaa kama hii habari haijatoka kwenye kitengo cha ofisi ya habari na Uenezi ya CHADEMA A.K.A Tanzania Daima.

Tanzania Daima wanajaribu kumsafisha Mbowe kwa kutumia matope huku wakitufanya tuulize maswali zaidi.

Hili gazeti la Tanzania Daima linawadharau sana wasomaji wake. Nadhani labda wasomaji wake ni wale wanaochukua kila kama dodoki bila kuchanganua na kuchuja.
Mbowe apuuzia hoja za Kabaka,Ghasia

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, amepuuza madai ya mawaziri Gaudencia Kabaka na Hawa Ghasia, kwamba ni mdaiwa sugu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Mbowe amedai kuwa viongozi hao wanafanya kazi ya kuficha uovu unaofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake waliobainika kutumia mifuko kinyume cha maadili kupitia kwa kumchafua kisiasa.

Kabaka ni Waziri wa Kazi na Ajira na Ghasia ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).

Mbowe aliyajibu madai hayo juzi muda mfupi baada ya Kabaka kuliambia Bunge kwamba kuna hati ya kukamatwa ambayo imetolewa kwa ajili ya Mbunge mmoja (hakumtaja jina) kutokana na mkopo aliochukua katika moja ya mifuko hiyo kushindwa kuirejesha.

Hata hivyo, aliposimama kuchangia, Ghasia alisema hakuna haja ya Kabaka kumficha kiongozi huyo na kwamba mhusika wake ni Mbowe.

Lakini akijibu hoja hiyo, Mbowe alisema kampuni zake zilikopa Sh milioni 15 kutoka NPF takribani miaka 25 iliyopita (kabla haijawa NSSF) na kwamba mkopo huo ulishalipwa.

Mbowe alisema kinachodaiwa ni riba inayotokana na serikali kukosea hesabukiasi cha kutojua wanadai kiasi gani, ingawa ameshalipa zaidi ya shilingi milioni 80 zikiwa ni mkopo na riba.

Mbowe, alisema mawaziri hao wameshindwa kujibu hoja ya msingi iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyewaita na kuwataja kwa majina baadhi ya mawaziri na `wabunge ombaomba' katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alisema, "wakaulize kwa wenye kampuni, wakatafute ukweli wa jambo hilo, na vile vile mikataba ya kukopeshana na kukopa ina utaratibu wa kumaliza migogoro inapotokea, basi wakamalize migogoro kwa mujibu wa mkataba."

CHANZO:Nipashe

http://www.ippmedia.com/frontend/?l=68318
 

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225


  • LAPF yakana kumdai Mbowe
  • Yaruka kuwasaidia Msigwa, Mbilinyi

SIKU chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kusema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amekopa kiasi cha sh bilioni moja kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Eliud Sanga, amekanusha.


LAPF pia imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini, Peter Msigwa, kama ilivyosemwa bungeni. Juzi, Ghasia alisema kuwa Mbowe anadaiwa sh bilioni moja na LAPF na ametumiwa waraka wa kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waziri huyo alisema si kosa kwa wabunge kupewa fedha na LAPF, lakini ni kosa kwa mbunge kutorejesha fedha alizokopeshwa.


Kauli ya LAPF
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Sanga, alibainisha kuwa LAPF haijawahi kumkopesha Mbowe sh bilioni moja, na kwamba mfuko huo hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo.


"Mfuko wa LAPF hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo na wanachofanya ni kutoa mikopo ya wanachama wake kupitia vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na mikopo ya nyumba kwa wanachama wanaokaribia kustaafu," alieleza Sanga.


Alisema shughuli kuu za mfuko huo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, uwekezaji na kulipa mafao. "Ieleweke kuwa ingawa waheshimiwa wabunge au mtu au taasisi yoyote hazuiliwi kuomba msaada wa kijamii, Mbilinyi na Msigwa hawajawahi kuwasilisha maombi na hawajawahi kupewa msaada wowote na LAPF.
Mawaziri , Wabunge , Watawala wa CCM wamekuwa wanatafuta huruma ya Wananchi:
1.Wanafuatilia Maisha ya Mbowe na kuijaribu kumfungulia kesi huku wakiacha wizi wa 200Bils BOT
2.Wanafuatilia Safari za Askof Kakobe Marekani huku wakiacha Safari za Kikwete anayesafiri kila kukicha na kuhujumu kodi
3.Wanapiga marufuku Mikutano ya Ukawa huku wakiruhusu mikutano ya CCM
4.Wanapinga ushirikiano wa CHADEMA NA CUF wakati wao wana serikali ya umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Yapo Mengi lakini hawa viongozi ni wanafiki wakubwa na mdo wao wa kutawala umekwisha!!
 

J Mbungi

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
235
225
Mheshimiwa..Inaongelewa LAPF siyo NSSF usichanganye mambo hapo...! Kama kuna mkopo alichukua NSSF fungua uzi mpya tujadili mkuu!
Mbowe anasema alikopa NSSF, huyu naye anasema hajamkopesha?. Aliyekopa anasema amekopa. Hii ni sawa na kusema, mwizi anasema aliiba lakini aliyeibiwa anasema hakuiba!.

Siwezi kushangaa kama hii habari haijatoka kwenye kitengo cha ofisi ya habari na Uenezi ya CHADEMA A.K.A Tanzania Daima.

Tanzania Daima wanajaribu kumsafisha Mbowe kwa kutumia matope huku wakitufanya tuulize maswali zaidi.
 

MoudyBoka

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
909
1,000
Hawa Ghasia hasitahili kuwa Waziri wala mbunge bali alipaswa kuwa Muimbaji wa taarabu pale Magomeni sema huo ushemeji Shemeji ndio unatupa watu hovyo!!
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mheshimiwa..Inaongelewa LAPF siyo NSSF usichanganye mambo hapo...! Kama kuna mkopo alichukua NSSF fungua uzi mpya tujadili mkuu!
Ndugu, ninaongea kitu ambacho nina uhakika nacho. Soma alichokisema Mh. Mbowe.
Lakini akijibu hoja hiyo, Mbowe alisema kampuni zake zilikopa Sh milioni 15 kutoka NPF takribani miaka 25 iliyopita (kabla haijawa NSSF) na kwamba mkopo huo ulishalipwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom