Waziri Dkt. Ndumbaro Anufaisha Vikundi 8 na Mfuko wa Jimbo Songea Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

WAZIRI DKT. NDUMBARO ANUFAISHA VIKUNDI 8 NA MFUKO WA JIMBO SONGEA

"Nimekabidhi mashine nane za kutotolesha vifaranga kwa vikundi nane vya Jimbo la Songea Mjini, Kupitia fedha za mfuko wa jimbo kwa lengo la kuwainua wananchi waliojumuika kupitia vikundi vilivyosajliwa kisheria" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

"Nimekabidhi vifaa tiba katika vituo saba vya afya vya Manispaa ya Songea kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Pamoja na viongozi wengine wa vituo hivyo." - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

"Nimeambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini CDE. Mwinyi Msolomi Pamoja na viongozi wengine wa chama. Ugawaji wa Vifaa tiba ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kupitia mfuko wa jimbo. " - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

"Ninatoa wito kwa wananchi wengine kuunda vikundi ili muweze kunufaika na mfuko huu awamu ijayo" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.45.57.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.45.59(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.45.58.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.46.00.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.46.01.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-23 at 13.46.02.jpeg
 
Back
Top Bottom