Tanzania yakopa Tsh. Bilioni 32 Kutoka Saudi Arabia wakati wezi wakiiba mabilioni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,063
49,749
Mambo mengine yanatia aibu sana kuyasikia.

Wakati Wezi wakiiba mabilioni ya pesa,tukilipa mabilioni kwenye riba na mikataba mibovu eti Leo hii Nchi inakopa Bilioni 32.

Viongozi wa Serikali muwe mnaona aibu wakati mwingine na ikibidi kumbe msitangaze Wala kupiga mapicha mnakera sana.

Sipingi Mikopo ila nashangaa kukopa vihela vidogo kama hiyo,sidhani kama tumefikia hapo.

Nilitegemea Nchi ikope mabilioni ya miradi mikubwa ya kimkakati sio huyo tubilikni 32.Tanzania sio Burundi au Malawi kukopa hela ya chumvi.

---
Tanz
Kwa mujibu wa Mkataba uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Mkopo huo unatoka Mfuko wa Maendeleo wa Saudi utakaotumika kuendeleza ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme kutoka Benaco hadi Kyaka mkoa wa Kagera
-
Akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa mradi, Dkt. Mwamba amesema, Fedha zitawezesha kujengwa njia ya Msongo WA umeme wa Kilovolti 220 yenye urefu wa kilometa 167 pamoja na kuboresha eneo la Benaco - Kyaka na kujenga kituo kipya eneo la Benaco na huduma za ushauri.

“Mradi huo chini ya mkataba tuliosaini unatekeleza Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2025/26 na ni sehemu ya ajenda kuu ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayolenga kujenga uchumi shindani wa viwanda na vipaumbele kwa maendeleo ya watu kupitia mikakati mbalimbali,” alisema Dkt. Mwamba.

Dkt. Mwamba alisema mradi wa Kyaka- Benaco umekuwa ukitekelezwa kwa msaada wa fedha kutoka katika Muungano wa nchi zinazouza mafuta/petroli (OPEC) ambao umechangia dola milioni 60, Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu dola milioni 30 na Serikali ya Tanzania dola milioni 2.4.

Alisema kuwa mkopo uliosainiwa ni moja ya mikopo inayotolewa na mfuko huo katika kutekeleza miradi mbalimbali, ambapo Tanzania imenufaika na mfuko huo hasa katika sekta za maji, miundombinu ya Barabara na afya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kuwa Serikali imekusudia kuongeza na kusaidia uchumi na maendeleo ya jamii nchini kwa kuwezesha sekta ya nishati na kuwapatia watu wake shughuli mbalimbali za kufanya zinazotekelezwa na mradi huo.

Aidha aliongeza kuwa Mfuko huo utabaki kuwa mbia mkubwa kwa Tanzania katika kusaidia kukuza Maendeleo ya taifa na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Mfuko huo kuendeleza mahusiano ya maendeleo.

View: https://twitter.com/Hakingowi/status/1722626407359263096?t=f4jH-TZbrc6NTtDmirBLEg&s=19

Mradi mmja umekopewa mikopo kibao.Soma hapa 👇
 
Mambo mengine yanatia aibu sana kuyasikia.

Wakati Wezi wakiiba mabilioni ya pesa,tukilipa mabilioni kwenye riba na mikataba mibovu eti Leo hii Nchi inakopa Bilioni 32...
Hakuna ubaya wowote mtu, taasisi au nchi kukopa popote as long as mkopo huo una justification, ya ni mkopo wa fedha za kufanya nini na umekopwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, una masharti nafuu, hata Marekani japo ni tajiri number moja duniani, inakopa tena inakopa kutoka China.
P
 
Tuwe wakweli;
Mama must go,
Mwigulu must go,
CCM at all must go.
Bila ya hivyo yatatokea yale aliyosema Job Ndugai ya nchi kuuzwa kufidia madeni yasiyo na lazima. Yaani ukiona watu wazima (Rais na waziri wake wa fedha) wanajisifia hadharani eti wanauwezo wa kukopa na wanakopesheka huku hawakemei zinavyo ibiwa ujue hapo hakuna kitu.
 
hawa wote must go na wasikumbukwe kabisa hata kwenye vitabu vya historia ya Tanzania. wanafanya maigizo tu.
 
Hakuna ubaya wowote mtu, taasisi au nchi kukopa popote as long as mkopo huo una justification, ya ni mkopo wa fedha za kufanya nini na umekopwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, una masharti nafuu, hata Marekani japo ni tajiri number moja duniani, inakopa tena inakopa kutoka China.
P
Sijasema Nchi isikope ila hoja yangu ni value ya Mkopo unokopwa ni vihela vidogo ,ilistahili Burundi au Malawi ndio wakope vihela vidogo vidogo.

Unakopaje bil.32 wakati unayekeleza miradi mikubwa ya mabilioni Kwa pesa ya ndani?

Tukope Kwa miradi mikubwa kama hii hapa 👇
20231109_070911.jpg
 
Tuwe wakweli;
Mama must go,
Mwigulu must go,
CCM at all must go.
Bila ya hivyo yatatokea yale aliyosema Job Ndugai ya nchi kuuzwa kufidia madeni yasiyo na lazima. Yaani ukiona watu wazima (Rais na waziri wake wa fedha) wanajisifia hadharani eti wanauwezo wa kukopa na wanakopesheka huku hawakemei zinavyo ibiwa ujue hapo hakuna kitu.
Kukopa sio hoja yangu, naunga mkono mikopo ya miradi.

Hoja yangu ni kwamba Tanzania hatujagikia kukopa vihela vidogo kama hivyo.
 
Back
Top Bottom