Damas Ndumbaro: Zaidi ya nusu ya Watanzania hawaifahamu Katiba

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Tayari Bunge limepitisha bajeti ya Sh9 bilioni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mchakato wa Katiba mpya. Hata hivyo, haijulikani ni mchakato huo utafikia tamati na nchi kupata Katiba mpya.

Wizara ya Katiba na Sheria, imewakutanisha pamoja mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wastaafu na waliopo madarakani katika kikao chenye lengo la maoni yao kuhusu mchakato kupata Katiba mpya.
Waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika leo Agosti 28, 2023 jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akiwa kama Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, Joseph Warioba na Mizengo Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Dk Damas Ndumbaro amesema wameamua kukutana na viongozi hao ili kupata uzoefu wao kwa kuwa waliwahi kufanya kazi katika wizara hiyo, hivyo wana ufahamu na uelewa wa kutosha katika mchakato wa Katiba mpya.

"Tunaamini uzoefu mliokuwa nao katika wizara hii na katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ambao ulikoma mwaka 2014, mna mengi ya kutushauri ili tuwe na mchakato mahsusi. Tunaamini tutajufunza mengi kutoka kwenu," amesema Dk Ndumbaro.

Waziri huyo amebainisha kwamba wizara yake imeamua kuliweka kama kipaumbele namba moja suala la elimu ya Katiba kwa wananchi kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba, wengine hawajawahi hata kuiona.

Amesema ulichukulia umuhimu wa Katiba katika taifa lolote, wana wajibu wa kuhakikisha kwamba hiyo asiliamia 50 ya Watanzania wanaifahamu Katiba. Amesema wasipoifahamu, hatari ni kwamba wataamini hata upotoshaji unaofanya huko mitaani.

Chanzo: Mwananchi
 
Nawapongeza sana hao Watanzania zaidi ya nusu kutoifahamu hiyo Katiba. Maana haikuandaliwa kwa manufaa ya Wananchi wote! Isipokuwa iliandaliwa kwa manufaa ya kikundi cha watu wachache tu wanaojiita ccm.

Siku tukifanikiwa kama nchi kuwa na Katiba yenye maslahi kwa nchi, badala ya kikundi cha watu wachache pekee, kila Mwananchi ataitafuta ili aisome na kuilewa.
 
28 August 2023

"Wanataka KATIBA MPYA Walikimbia Mchakato BUNGENI "Dkt Ndumbaro Mbele ya Mawaziri wa Sheria

View: https://m.youtube.com/watch?v=ur0Th8eNHu0

Huku Dr. Ndumbaro akisikilizwa na kufuatiliwa kwa umakini na viongozi wazito ambao ni Makamu wa kwanza wa Rais SMZ Othman Masoud Othman ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Na mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, jaji Joseph Warioba na Mizengo Peter Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Dr. Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dr. Harrison Mwakyembe na Dr. George Simbachawene....
 
Tayari Bunge limepitisha bajeti ya Sh9 bilioni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mchakato wa Katiba mpya. Hata hivyo, haijulikani ni mchakato huo utafikia tamati na nchi kupata Katiba mpya.

Wizara ya Katiba na Sheria, imewakutanisha pamoja mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wastaafu na waliopo madarakani katika kikao chenye lengo la maoni yao kuhusu mchakato kupata Katiba mpya.
Waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika leo Agosti 28, 2023 jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akiwa kama Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela, Joseph Warioba na Mizengo Pinda. Pia, wapo mawaziri wa zamani wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwemo Mary Nagu, Balozi Mathias Chikawe, Profesa Palamagamba Kabudi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk George Simbachawene ambaye pia ni Waziri wa Utumishi na Utawala Bora.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Dk Damas Ndumbaro amesema wameamua kukutana na viongozi hao ili kupata uzoefu wao kwa kuwa waliwahi kufanya kazi katika wizara hiyo, hivyo wana ufahamu na uelewa wa kutosha katika mchakato wa Katiba mpya.

"Tunaamini uzoefu mliokuwa nao katika wizara hii na katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ambao ulikoma mwaka 2014, mna mengi ya kutushauri ili tuwe na mchakato mahsusi. Tunaamini tutajufunza mengi kutoka kwenu," amesema Dk Ndumbaro.

Waziri huyo amebainisha kwamba wizara yake imeamua kuliweka kama kipaumbele namba moja suala la elimu ya Katiba kwa wananchi kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba, wengine hawajawahi hata kuiona.

Amesema ulichukulia umuhimu wa Katiba katika taifa lolote, wana wajibu wa kuhakikisha kwamba hiyo asiliamia 50 ya Watanzania wanaifahamu Katiba. Amesema wasipoifahamu, hatari ni kwamba wataamini hata upotoshaji unaofanya huko mitaani.

Chanzo: Mwananchi
wale jamaa waliopinga takwimu za TEC, hawajamuuliza Ndumbaro amepata wapi hizo takwimu,
au anawapotosha wale jamaa waliouliza TEC walipata wapi takwimu kua wananchi wingi hawapendi mkataba wa bandari?
 
Back
Top Bottom