Waziri Dkt. Ndumbaro Aweka Mikakati ya Wananchi Kunufaika na Utamaduni, Sanaa na Michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili ofisini Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Mhe. Dkt.Damas Ndumbaro ameanza kazi Wizarani hapo kwa kukutana na kuzungumza na watumishi na viongozi wa Idara ya Utamaduni, Sanaa, Utawala, Sera na Mipango na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kwa lengo la kufahamiana na Watumishi wa Idara hizo, kupata ufafanuzi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwahudumia wananchi ili waendelee kunufaika zaidi na Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Mhe. Dkt. Ndumbaro alipokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Yakubu kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa furaha kwa wananchi ikiwemo kuwa na Matamasha ambayo yanatoa fursa ya ya ushiriki wa wananchi katika michezo na kujiongezea kipato.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Sekta hizo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza Idara ya Utamaduni kuongeza bidii katika kusimamia na kuelimisha jamii kuhusu maadili mema, Utamaduni, Mila pamoja na Desturi njema, kuhakikisha vazi la Taifa linapatikana kwa kuwashirikisha wabunifu kwa kuandaa shindano la wabunifu wa mavazi yatakayopigiwa kura huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mkakati wa kutangaza Lugha ya Kiswahili Kimataifa.

Aidha, ameitaka Idara ya Sanaa ianzishe Dawati ndani ya Idara la kusimamia Mashirikisho ya Sanaa ili kuleta ufanisi wa utendaji wa Mashirikisho hayo na namna yanavyosaidia wasanii wao, kuhakikisha inaanzisha utaratibu maalumu utakaotoa mwongozo wa uendeshaji na uendelezaji wa mashirikisho hayo pamoja na kuweka mikakati ya namna Sekta hiyo inavyoweza kuongeza ajira kupitia uibuaji na uendelezaji wa vipaji vya vijana kwa kushirikiana na Sekta binafsi.

IMG-20230905-WA0129.jpg
255762089225_status_0ae1d15a81bf4cdeb90b099dc96d6ebb.jpg
255762089225_status_20212d52e76b40e69ead5f5ecc3d768c.jpg
 
WAZIRI DKT. NDUMBARO AKUTANA NA IDARA NNE, AWEKA MIKAKATI YA WANANCHI KUNUFAIKA NA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili ofisini Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Damas Ndumbaro ameanza kazi Wizarani hapo kwa kukutana na kuzungumza na watumishi na viongozi wa Idara ya Utamaduni, Sanaa, Utawala, Sera na Mipango na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kwa lengo la kufahamiana na Watumishi wa Idara hizo, kupata ufafanuzi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwahudumia wananchi ili waendelee kunufaika zaidi na Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Mhe. Dkt. Ndumbaro alipokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Yakubu kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa furaha kwa wananchi ikiwemo kuwa na Matamasha ambayo yanatoa fursa ya ya ushiriki wa wananchi katika michezo na kujiongezea kipato.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Sekta hizo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza Idara ya Utamaduni kuongeza bidii katika kusimamia na kuelimisha jamii kuhusu maadili mema, Utamaduni, Mila pamoja na Desturi njema, kuhakikisha vazi la Taifa linapatikana kwa kuwashirikisha wabunifu kwa kuandaa shindano la wabunifu wa mavazi yatakayopigiwa kura huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mkakati wa kutangaza Lugha ya Kiswahili Kimataifa.

Aidha, ameitaka Idara ya Sanaa ianzishe Dawati ndani ya Idara la kusimamia Mashirikisho ya Sanaa ili kuleta ufanisi wa utendaji wa Mashirikisho hayo na namna yanavyosaidia wasanii wao, kuhakikisha inaanzisha utaratibu maalumu utakaotoa mwongozo wa uendeshaji na uendelezaji wa mashirikisho hayo pamoja na kuweka mikakati ya namna Sekta hiyo inavyoweza kuongeza ajira kupitia uibuaji na uendelezaji wa vipaji vya vijana kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.06.jpeg
    35.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.05(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.05(1).jpeg
    35.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.05.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.05.jpeg
    37.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.06(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.06(1).jpeg
    74.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.07.jpeg
    54.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.09.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-05 at 21.23.09.jpeg
    50 KB · Views: 1
Ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili ofisini Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Mhe. Dkt.Damas Ndumbaro ameanza kazi Wizarani hapo kwa kukutana na kuzungumza na watumishi na viongozi wa Idara ya Utamaduni, Sanaa, Utawala, Sera na Mipango na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kwa lengo la kufahamiana na Watumishi wa Idara hizo, kupata ufafanuzi na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwahudumia wananchi ili waendelee kunufaika zaidi na Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Mhe. Dkt. Ndumbaro alipokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Yakubu kuwa, wizara hiyo inaendelea kutoa furaha kwa wananchi ikiwemo kuwa na Matamasha ambayo yanatoa fursa ya ya ushiriki wa wananchi katika michezo na kujiongezea kipato.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Sekta hizo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameagiza Idara ya Utamaduni kuongeza bidii katika kusimamia na kuelimisha jamii kuhusu maadili mema, Utamaduni, Mila pamoja na Desturi njema, kuhakikisha vazi la Taifa linapatikana kwa kuwashirikisha wabunifu kwa kuandaa shindano la wabunifu wa mavazi yatakayopigiwa kura huku akisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mkakati wa kutangaza Lugha ya Kiswahili Kimataifa.

Aidha, ameitaka Idara ya Sanaa ianzishe Dawati ndani ya Idara la kusimamia Mashirikisho ya Sanaa ili kuleta ufanisi wa utendaji wa Mashirikisho hayo na namna yanavyosaidia wasanii wao, kuhakikisha inaanzisha utaratibu maalumu utakaotoa mwongozo wa uendeshaji na uendelezaji wa mashirikisho hayo pamoja na kuweka mikakati ya namna Sekta hiyo inavyoweza kuongeza ajira kupitia uibuaji na uendelezaji wa vipaji vya vijana kwa kushirikiana na Sekta binafsi.

View attachment 2740298View attachment 2740300View attachment 2740299

Ogopa tapeli.
 
Back
Top Bottom