Waziri Dkt. Ashatu Kijaji - Tanzania, China, Uturuki na Indonesia Kuendeleza Ushirikiano wa Kibiashara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Indonesia na Balozi wa Indonesia nchini Mhe. Tri Yogo Jatmiko Septemba 9, 2023 katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam..

Waziri Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania iko tayali kuendeleza ushirikiani baina ya nchi hizo na iko tayari kuwezesha miradi ya uwekezaji hususani katika sekta ya kilimo hasa katika uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao ambayo nchi hiyo imepanga kuyaendeleza kama vile karafuu ili kuongeza ajira na kipato kwa wanzania.

Aidha, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kuzungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Uturuki na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Güllüoğlu 11/09/ 2023 katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam

Vilevile, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kuzungumza kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na China hususan uchakataji wa mazao ya kilimo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 11/09/2023.

F5xZwxYXwAAPyoy.jpg
F5xhZLhXcAAp56X.jpg
F5xhZLkWgAErZGz.jpg
F5xZwxWXsAA0LqE.jpg
F5xZwxVXsAAa3Sg.jpg
F5xhZLhXcAAp56X.jpg
F5xlEgtWUAAjivC.jpg
F5xlEgoWYAAfzaM.jpg
F5xl10pXAAAzjuS.jpg
F5xl10nWUAAx6P4.jpg
 
Back
Top Bottom