Waziri Arcado Ntagazwa ahamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Arcado Ntagazwa ahamia CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwafrika, Aug 8, 2010.

 1. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  WAKATI taarifa za mipango ya wana-CCM wanaolia kuwa wamechezewa rafu kwenye kura za maoni kuhamia upinzani zikizidi kushamiri, waziri wa zamani kwenye serikali za awali ya pili na tatu, Arcado Ntagazwa amehamia Chadema.

  Habari za vigogo wa CCM kufanya mipango ya kujiondoa zilitiwa uzito zaidi na kauli ya mbunge wa zamani wa Maswa, John Shibuda ambaye alikiri kufanya mazungumzo na Chadema pamoja na CUF na UDP, lakini akasema atatangaza maamuzi magumu wiki ijayo.


  Kujiunga kwa Ntagazwa kunaonekana kutazidi kuipa nguvu Chadema, ambayo imefanya kazi kubwa ya kujiimarisha katika kipindi cha miaka mitano huku kutangazwa kwa katibu wake mkuu, Dk Willibrod Slaa kugombea urais kukikifanya chama hicho kuwa tishio jipya kwenye mbio za kwenda Ikulu.


  Ntagazwa, ambaye aliangushwa mwaka 2005 na mwaka huu kwenye kura za maoni, hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, lakini naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliithibitishia Mwananchi Jumapili juu ya kupokolewa kwa mwanachama huyo mpya.


  Kabwe aliliambia gazeti hili jana kuwa mbunge huyo wa zamani wa Kibondo alichukua kadi ya Chadema jana asubuhi wilayani Kibondo mkoani Kigoma.


  Ntagazwa ameitumikia serikali ya awamu ya kwanza akiwa Naibu Waziri wa Fedha (1983-85) na baadaye akashika nafasi hiyo kwenye Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi (1986-87).


  Chini ya uongozi wa Ali Hassan Mwinyi alikuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Maliasili na Utalii (1990-2000) na kuanzia mwaka 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) hadi mwaka 2005 alipoanguka kwenye ubunge.


  "Tunashukuru kwa kumpata Ntagazwa ambaye ana uzoefu mkubwa katika serikali. Tunaamini atatusaidia wakati Chadema inapounda serikali yake," alisema Zitto, mmoja wa wabunge wa Chadema waliokuwa moto bungeni.

  Baada ya kushindwa ubunge mwaka 2005, taarifa zilienea kuwa Ntagazwa ameihama CCM na kujiunga na Chadema lakini baadaye mwanasiasa huyo alijitokeza na kukanusha habari hizo akisema kuwa alikuwa akiwasiliana na mwanasheria wake ili amshtaki mwandishi, gazeti na mchapishaji wake kwa kumdhalilisha.

  Kwa upande wa Shibuda, ambaye alitangaza kwa muda mrefu kuwa angegombea urais kupambana na Jakaya Kikwete ndani ya CCM, uamuzi kamili kuhusu hatua inayofuata kwake utakuwa mapema wiki ijayo.

  Shibuda, mwanasiasa machachari, alisema kati ya jumatano au Alhamisi anatarajia kutangaza maamuzi magumu kutokana na kile alichokiita ni baadhi ya viongozi ndani ya CCM kuamua kutumikia wanyonyaji na mafisadi.

  Mwanasiasa huyo mwenyee kupenda kuzungumza kwa kutumia misemo mbalimbali ya Kiswahili, alisema: "Viongozi wa CCM wa leo ni sawa na jiwe la bahari, halifikiri kiu ya mtende."

  Alifafanua kwamba wanachofikiria viongozi hao kwa kiasi kikubwa ni nafsi zao na wanasahau umasikini na matatizo ya Watanzania walio wengi.


  Shibuda aliongeza kwamba enzi za CCM ya Mwalimu Julius Nyerere, mtu mwenye kusimamia misingi aliitwa rafiki, lakini akaongeza: "Siku hizi mtu anayesimamia misingi ya chama huitwa adui na mtu hatari sana."

  Aliweka bayana kwamba kamwe hafikiri kukata rufaa kupinga matokeo ya kura ya maoni baada ya kushindwa kwa sababu hajawahi kukata rufaa na akatendewa haki.

  "Msimamo wangu uko wazi; sitakata rufaa CCM kupinga matokeo. Kwa sababu historia iko bayana. Katika siku zote nilizokata rufaa ndani ya chama sijawahi kusikilizwa wala kutendewa haki," alifafanua Shibuda.

  "Niliwahi kukata rufa kupinga mambo mbalimbali kuanzia Nec hadi uongozi wa Jumuiya ya Wazazi, lakini sijawahi kusikilizwa. Nilikata rufaa uenyekiti Jumuiya ya Wazazi, lakini mzee wangu (rais wa awamu ya tatu, Benjamin) Mkapa alinishughulikia kwa sababu nilikuwa nahoji kwenye Nec."

  Alisema kutokana na mtiririko huo wa matukio ya kutomtendea haki ndani ya CCM, ameamua kufanya maamuzi magumu na sasa anaanza kuagana na kupata ushauri wa mwisho kwa watu anaowaheshimu ndani ya chama hicho.

  Shibuda alisisitiza kwamba anajiandaa kuhama na kufanya maamuzi hayo huku akiweka bayana kuwa "wanamapinduzi wengi walipotaka kujipanga kufanya maamuzi magumu ya kutetea, haki walikimbia kwao kidogo."

  "Samora Machel alikimbilia nchini Tanzania, hata akina Augustino Neto wa MPLA Angola, akina Sam Nujoma wa Namibia wote walifanya hivyo, kisha wakarudi kukomboa watu wao," alifafanua.

  Alisema CCM kama chama kina misingi mizuri isipokuwa kimejaa watu ambao hawataki ukweli, hasa unapokosoa utendaji mbovu, ndipo huonekana ni msaliti, adui na mtu hatari kabisa.

  "Tanzania bila malaria inawezekana lakini Tanzania bila mafisadi na wanyonyaji haiwezekani. Sasa hivi CCM ni chama cha walowezi, wale ambao tuliwaita wanyonyaji sawa na makaburu ndiyo wameshika chama," alisisitiza.


  Alisema msimamo wake hadi sasa ni kutumikia Watanzania katika misingi ambayo nchi ilirithi kutoka TANU.
  "Ndiyo maana nataka nikwambie kaka, ukihama msikiti hujagombana na msahafu. Kwa hiyo kama nitahama sitagombana na Watanzania kwani lengo ni kuwatumikia wao," alisisitiza.

  Habari zaidi zinasema kuwa vigogo wengine kadhaa wa CCM wako njiani kujiunga na Chadema baada ya kushindwa kwenye kura za maoni ambazo wanaamini zilijaa rushwa, rafu na ukiukwaji wa taratibu.

  Habari zimeeleza kuwa mazungumzo hayo yanawashikirikisha wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo baadhi ya waliokuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi.

  Taarifa za kiuchunguzi zimeeleza kuwa hadi sasa Chadema kimefanya mazungumzo na wabunge wengi wa CCM.


  Alipoulizwa kuhusu Chadema kuwasiliana na wanasiasa hayo, Zitto Kabwe chama hicho kinawakaribisha wote wanaotaka kujiunga.

  Zitto alifafanua kwamba kwa kuwa Chadema ni chama cha upinzani chenye malengo ya kushika dola, kinahitaji watu makini kutoka CCM lakini akasema"hakuna taarifa rasmi ya makubaliano hadi sasa".
  Zitto, ambaye atatetea ubunge kwenye jimbo lake la Kigoma Kaskazini, alisema suala la kufanya mazungumzo na wana-CCM hao si tatizo.

  Hata hivyo, habari ambazo Mwananchi imezipata zinawataja baadhi ya wabunge wa zamani walioongea na Chadema kuwa ni pamoja na Lucas Selelii wa Nzega ambaye, hata hivyo, alisema bado hajakubali kujiunga na chama hicho wala kujiondoa CCM.


  "Ni kweli nilifanya mazungumzo na Chadema lakini nimekataa kwa sababu ukigombana na shehe siyo kugombana na Uislam. Siwezi kuhama CCM kwa sababu tu ya watu wachache mafisadi," alifafanua.

  "Tutabanana humu humu, hakuna kukimbia wala siwezi kuwaachia waendelee kutamba, kukimbia itakuwa ni kosa kwangu. Siwezi kuwaachia waendelee kutamba wao wenyewe."

  Selelii alisema uamuzi wa kuihama CCM haujaufikiria kwa sasa kwani bado anaamini chama hicho ni chake na hivyo hawezi kuondoka kwa sababu ya kufanyiwa mchezo mchafu na baadhi ya watu waovu.


  Alisema hata wakati wa mchakato wa kura za maoni yupo mmoja wa watuhumiwa wakubwa wa ufisadi nchini, ambaye alipiga kambi siku hiyo kuhakikisha anamng'oa.

  "Unafikiri ilikuwa mchezo alikwepo .....(jina tunalo) siku ya kupiga kura alihakikisha ananing'oa. Si unajua akiwepo, pesa anazomwaga hakuna mtu anayeweza kupona."

  Selelii alifafanua kwamba katika uchagugzi huo alinyanyasika na kuzomewa, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kumfanya afikirie kujitoa CCM labda baada ya kufanya tathimini ya kina.


  Kigogo mwingine wa CCM ambaye inasemekana alifanya mazungumzo na Chadema ni mbunge wa Iramba Mashariki, Mgana Msindai, ambaye pia ameshindwa kwenye kura za maoni.

  Msindai na Dk Slaa kwa muda wote wamekuwa pamoja kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na ameng'olewa kwenye kiti hicho baada ya kukaa bungeni kwa muda mrefu.

  Katika hatua nyingine baadhi ya wabunge na vigogo wa CCM walioshindwa kwenye kura za maoni wameuponda utaratibu mpya wa ulioanzishwa na chama hicho wa kuwapata viongozi wa dola kupitia kura za maoni za wanachama wote kwa madai kuwa unachangia rushwa.

  Aliyekuwa mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alisema utaratibu huo ni mbovu kwa kuwa unachochea rushwa kutokana na ukweli kuwa wanachama wengi wanakuwa hawana ufahamu wa kutosha na elimu ya uraia.

  Hata hivyo, Kimaro aliapa kuwa hatasita kulipua mabomu ya ufisadi nchini hata akiwa nje ya bunge kwa kuwa yapo majukwaa mengi ya kufanyia mambo hayo na kwamba safari yake ya kisiasa haijafika mwisho.

  "Si unajua ukifungulia milango wanaingia hadi inzi. Sasa hata huu utaratibu umeruhusu wengine wa ajabu kuingia ndani ya chama... ni sawa na unapofungua mlango kutaka hewa iingie, lakini badala yake hadi nge wataingia," alisema.

  Mpambanaji huyo wa ufisadi alifafanua kwamba, kuna watu walimchezea mchezo mchafu wakifikiri ndiyo kummaliza, lakini akasisitiza kwamba yapo majukwaa mbalimbali ya kuweza kufikisha ujumbe huo.


  "Tutaendelea kubanana tu, wala sitakaa kimya. Ila moyo wangu uko safi kabisa na naamini nitaendelea kutoa mchango wangu kwa taifa," alifafanua Kimaro.

  Alisema utaratibu huo wa kura za maoni kama utaachiwa kama ulivyo bila usimamizi makini, basi utakuwa hauna maana na hautafaa kutumiwa na chama.

  Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi aliupongeza utaratibu huo, lakini alikiri kwamba rushwa kwa sasa inashuka chini kutoka ngazi ya juu.


  Karamagi, ambaye alijiuzulu uwaziri kutokana na kashfa ya Richmond, aliweka bayana kwamba kukosekana elimu ya uraia na vyombo vya kusimamia utekelezaji wa utaratibu huo na sheria ya gharama za uchaguzi, ni hatari kwa ustawi wa jamii.

  "Kwa ujumla, nadharia ni nzuri sana, lakini kutokana na ukosefu wa vyombo vya usimamizi, hiyo imechangia ku-expand (kutanua) mianya ya rushwa kutoka ngazi ya juu kuja chini," alifafanua Karamagi.


  "Lakini kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya uraia, watu hawakuwa wakichagua bali walijua hiki ni kipindi cha mavuno tu kujiingizia fedha basi. Hii ni hatari sana kwa nchi."

  Dk Zainabu Gama ambaye aligombea jimbo la Kibaha Mjini, naye alisifia utaratibu huo lakini akakosoa kwamba hakukuwa na maandalizi mazuri katika utekelezaji.

  Kwa mujibu wa Dk Gama, utaratibu huo unawezesha wanachama wengi kushiriki kupata viongozi wa dola lakini tatizo ni elimu ya uraia kitu ambacho kiliwafanya wengi wasijue nani ni nani.


  Alisema ukosefu wa elimu ya uraia kwa wanachama, kulifanya baadhi yao wafikiri uchaguzi umekuwa ni fursa ya kupata fedha badala ya kuchagua viongozi bora.

  Gama alisema kwamba athari ya tatizo hilo ni kuchochea rushwa kutoka ngazi ya taifa hadi chini kitu ambacho alikiita kwamba ni cha hatari kwa mustakabali wa baadaye wa taifa na chama.


  Hata hivyo, alisema hafikirii kuhama CCM na lakini akadokeza: "Chama hakikujiandaa vizuri, watu walikuwa na kadi mpya nyingi tu na waliwezaa kuzifanyia modification (marekebisho) ya tarehe tu."

  "Kukosekana kwa umakini katika usimamizi, kumechangia kuongeza loopholes (mianya) ya rushwa katika kupata viongozi wa dola. Lakini, nashukuru mimi kazi nzuri," alifafanua.

  Siraju Kaboyonga, ambaye alikuwa mbunge wa Tabora Mjini, alisema tatizo kubwa ni ukosefu wa vyombo vya usimamizi kuanzia ndani ya chama, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hadi Takukuru.


  Kaboyonga alisema hadi sasa Takukuru haijaweza kujitanua katika maeneo yote nchini ndiyo maana pamoja na juhudi zake, bado ilimezwa na watoa rushwa.

  Mbunge huyo alisema hatua ya Takukuru kuzidiwa nguvu pia ilitokana na msimamizi wa sheria ya gharama za uchaguzi ambayo ni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa dhaifu.


  Alifafanua kwamba jukumu hilo lilipaswa kuwa chini ya ofisi ya vyama vya siasa wakati yenyewe haina ofisi katika maeneo mengi nchini, jambo ambalo liliifanya Takukuru kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.


  Reinard Mrope wa jimbo la Masasi, alifafanua kwamba utaratibu huo ni mzuri lakini tatizo kubwa ni utekelezaji.

  Source mwanachi 07/08/2010
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  huko NTAGAZWA aliposhindwa...aliyeshinda ndiye mwenye tuhuma za kumiliki,kushiriki & kuhusika katika matukio ya kialifu ya utekaji magari na ujambazi.....kwa stahili hii.....WEMA WATATOKA ...WABAYA WATAINGIA........!
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Safari ni safari, safari moja huongeza nyingine mwaka huu hadi raha somo lazima lieleweke hakuna kufeli.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii ni habari nzuri. Wanachama woote wa CCM wanaopigwa chini kwa kuonewa kwa Rushwa au ukiritimba wa CCM, kwa sasa wanaweza kabisa kubadili chama na kuingia CHADEMA hasa kwa bara. Kuingia kwa Dr. Slaa kwenye kugombea cheo cha Urais, kumeanza kuleta mwanga kwa watu wengi. Watu wameanza kujenga imani kwa Chadema kama chama Mbadala. Kama si Dr. Slaa kuingia kwenye kinyang'amyiro hicho, sidhani kama watu hawa wangelihama. Wangejikalia pembeni tu huku wakilia machozi ya samaki kwa kuogopa Weapon Of Opositions Destruction ya CCM isije ikawapitia na kuwaharibuharibu kabisa na kuwamaliza.

  Tunamsubiri Mangula na Malecela sasa waje waongeze nguvu Chadema hata kama Washauri. Hawa wanaifahamu CCM kwa ndani na wakija basi watamwaga siri zote. Naanza kuona mwisho wa CCM kwa mbaali. Mwaka 2015 ndiyo watauwana hasa maana Kikwete akiondoka, huo msuguano utakaotokea, mama weee......

  Ila lazima tuhakikishe CCM haifi maana kama ikifa, basi CHADEMA ndiyo itakuwa CCM ya leo. Hapa itabidi Dr. Slaa ahakikishe Tanzania kunaundwa vyama viwili vikubwa vya Siasa na iwe kama Simba na Yanga. Hii itafanya milele kuwe na uwiano kwa chama tawala na chama cha upinzani.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Aug 8, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  WanaCCM msisubiri mfanyiwe rafu na kukosa "ulaji" ndio mhame Chama, mnanitia wasiwasi sana na hiyo motive mliyo nayo! Na mkihama mnakimbilia kuomba nafasi za ubunge chapchap, kwa namna hiyo nchi hii tutafika wandugu?
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nafikiri watu kama wakina Ntagazwa wanahitajika kwani uzoefu wao serikalini ni muhimu kwa sasa , hivyo sioni kama kuna taabu watu hao kujiunga na CHADEMA kwa wakati huu.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu mama Zainabu Gama aliyekuwa mbunge wa Kibaha mjini nae ameangushwa kwenye kura a maoni? Kama ni hivyo, tafadhali mwenye matokeo ya Kibaha mjini atubandikie hapa kwani kwenye thread ile ya matokeo ya CCM sikuona!!
   
 8. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hizo ndio rangi halisi za chama cha mapinduzi! Sisi wajanja tulisha shitukia zamani! Nashukuru mmeanza kuziona!
   
 9. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Bulesi katika kura za awali za Ubunge,Jimbo la Kibaha mjini aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Dr.Zaynab Gama aliangushwa na Kamanda wa UVCCM wa Wilaya hiyo Bw.Sylivester Koka.Katika imbo hilo kulikuwa kuna Wagombea sita ambao ni Prof.Samwel Wangwe,Dr.Rose Mkonyi,Ret.Col.Hussein Vuon,Dr.Zaynab Gama,Hamis Kilinge na Sylivester Koka.

  Majibu ya matokeo ya Uchaguzi guo ilikuwa Sylivester Koka kura 4303 akifuatiwa na Pro.Samwel Wangwe kura 2570 na Mbunge wa sasa Dr.Zaynab Gama kura 1243 na alichukua nafasi ya tatu.
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hawa wengine weshajiozeaozea...haya tu tena...!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Aug 8, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Nadhani CHADEMA wako makini vya kutosha, watajua namna ya kuwatumia hao waliojiozea badala ya kuwaacha wao ndio waitumie CHADEMA.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kocha Mzuri huwatumia hawa UOZO na kutengeneza timu bora.

  Murinho akifundisha timu nzuri, anaoza. Akienda kwenye vitimu vya ovyo, anatesa.

  Binadamu ni watu ambao huwa wanacheza kutokana na unavyopiga mziki.
   
 13. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaaaaaaziiiiiz kwelikweli
   
 14. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Parapatataaa, Shibuda kikulacho ki nguoni mwako baba na muosha huoshwa jamani,umesahau kuwa ulitaka kupingana na JK uraisi mwaka huu wakakunote kuwa wewe si mwenzao na sasa wamekuchana mbaya?, hiki ndicho chama cha mafisadi (CCM) bana so watetezi wa haki na ustawi wa wananchi ni sumu kali ndani ya hiki chama.Shibuda na wengineo karibuni CHADEMA mpate raha na kuendeleza mapambano juu ya ufisadi.Mwaka huu yetu macho.:A S 100:
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mkuu Sikonge Umenena, nasubiri kwa hamu sana kumwona Mzee Mangula anakuja CHADEMA, tena sijui yuko wapi kwa sasa, kapotea sana ktk anga za siasa.
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu Ntagazwa amejichokea, Chadema wangekuwa makini kutopokea wanasiasa wachovu ambao tulitegemea watangaze kustaafu siasa. Huyu bwana alikuwa waziri tangu enzi za Mwalimu!
   
 17. M

  Mswahela Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tamaa nyingi na njaa kubwa
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Hapana wacha waje waseme mbinu walizokuwa wanazitumia....usisahau One Man's Garbage is another Man's Treasure
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,124
  Trophy Points: 280
  Tunawataka hao wakongwe acha waje.
   
 20. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anahaha njaa huyo Mkatoliki Ntagazwa. Anadhani kampeni za makanisani zitaisaidia Chadema. Watu makini kama Mangula hawawezi kujiunga na chama kinachoongozwa na DJ.
   
Loading...