Waziri aliyeachwa atoboa siri nzito EPA

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
*Adai mtandao uliwazidi ujanja Mkapa, Kikwete mapema
*Uliunda Baraza hewa la Mawaziri miezi 6 kabla ya uchaguzi
*Ulitisha vigogo BoT, wizara na wengine kuahidiwa vyeo

Na Mwandishi Wetu

WIKI chache baada ya kuvunjwa Baraza la Mawaziri na kuundwa jipya kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa kufuatia kashfa ya Richmond, siri nzito katika kashfa ya uporaji wa mabilioni ya pesa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) ndani ya Benki kuu ya Tanzania (BoT),imebainishwa.

Mmoja wa mawaziri aliyetemwa katika Baraza jipya la Rais Jakaya Kikwete, ameliambia gazeti hili kwa sharti la kuhifadhiwa jina kuwa kashfa ya EPA ni nzito na chimbuko lake limejikita baada ya kumalizika mchakato wa kumpata mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mei 2005.

Pamoja na kuunga mkono hoja za wananchi wengi kutaka majina ya mafisadi wanaorejesha fedha kuanikwa hadharani, mwanasiasa huyo alisema jambo hilo ni ngumu kutekelezeka kwa sasa kutokana na misingi iliyojikita ndani ya kashfa hiyo,aliyodai imegusa watu na maeneo nyeti.

"Watu wamejaa jazba, waitazama kashfa ya EPA kama moto uliteketeza mali zao bila kujua chanzo chake na wahusika,"alisema waziri huyo aliteachwa.

Alilitaja kundi la wanamtandao maslahi lililoibuka katika uchaguzi mkuu uliopita na kudai kuwa lilichangia kwa kiasi kikubwa 'kansa ya EPA' ndani ya BoT. Katika mchakato huo, Rais Kikwete,aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga wanachama wenzake 11 waliojitokeza kwenye kinyang'anyoro hicho.

Alidai kundi hilo lililokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Rais Kikwete anashinda mchakato huo,lilikwenda mbali zaidi kwani baada ya uteuzi, lilivuka mipaka na kufanya mambo ya 'ajabu ajabu' kwa siri bila hata mgombea (Rais Kikwete) kujua, wala kuhusishwa.

Alidai kwamba mara tu baada ya kumalizika kwa mchakato huo, wanamtadao maslahi, walipanga safu ya 'Baraza lao la Mawaziri' hadi mabalozi wa nje na kupita huku na kule kutishia na kuahidi nafasi kwa vigogo wengine wa mashirika ya umma na taasisi mbalimbali, zikiwemo za fedha.

"Masikini wakati Rais Kikwete anasimama kwenye majukwaa kuomba kura, watu hawa walifanya vitu vya ajabu sana, bila yeye kujua, walipita huku na kule kutishia watu kwenye nafasi zao huku wakiahidi wengine kuwapa vyeo vikubwa. Walifanya hivyo kama wao ndio wenye nchi, waliunda 'Baraza lao la Mawaziri' miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu uliomuingiza Rais Kikwete madarakani."

"Waalipita maeneo mengi,hata BoT kuwajenga hofu watendaji, hadi mawaziri, makatibu wakuu na vigogo wengine. Hawa walikuwa na wasiwasi kutokana na mageuzi yaliyotarajiwa kutokea baada ya uchaguzi mkuu, wakasikiliza na kutii waliyoambiwa na wanamtandao hao.

" Walijua lazima CCM ingeshinda, wakawa tayari kutekeleza matakwa ya wanamtandao kwa hofu ya kupoteza nafasi zao. Hapo ndipo watu hao wakapata mwanya kuchonga mipango kuanzisha kampuni feki kati ya Mei hadi Januari 2006 kwa lengo la kujinufaisha,"alidai mwanasiasa huyo.

"Kumbuka kipindi hiki kilikuwa kigumu kwa vigogo ambao hawakuwa kwenye kundi la mtandao, walihofia nafasi zao. Kitendo cha kufuatwa na wanamtandao hao, kilifanya wajione kama abiria ambao hawakuwa na tiketi za kusafiri kwa basi la mtandao, sasa wameletewa mlangoni. Wakawa tayari kutekeleza yote waliyotakiwa kufanya, hapa ndipo tatizo lilianzia," kilidokeza chanzo hicho.

Aliendelea kusema" Watu hao (wanamtandao maslahi) wakapanga timu ya kampeni, hawakuiamini ile ya Mangula (Philip, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM). Wakati huo Mkapa (Rais mstaafu, Benjamini) alibaki kama nyoka asiye na sumu, nguvu yake iliporwa na wanamtandao hao bila yeye wala Rais Kikwete kujua.

Chanzo hicho kilifafanua kwamba huenda Rais Mkapa alifikwa na hali hiyo kutokana na matokea ambayo hakuyategemea kwenye mchakato huo.

" Kumbuka Mkapa alipata mapigo mazito mawili baada ya mchakato, kwanza alijikuta ameshindwa 'kumshika mkono'msaidizi wake mkuu upande wa chama, Mzee Malecela (John, aliyekuwa Makamu wake), hali hiyo ikamtokea pia kwa msaidizi wake mkuu upande wa serikali,Bw.Sumaye
( Frederick, aliyekuwa Waziri Mkuu ) ambao wote waligombea na akashindwa kuwabeba. Matokeo hayo yalimchanganya Rais Mkapa, miezi sita ya mwisho ya utawala alikuwa kama ameiweka nchi rehani kwa wanamtandao, walifanya waliyotaka," alidai.

Aliendelea kufafanua" Baada ya kumalizika mchakato na mgombea kupatikana, Rais Mkapa alikosa 'control,' nchi ikawa kama 'imetekwa' na wanamtandao maslahi. Wakati mgombea (Rais Kikwete) anazunguka mikoani kwa nia njema ya kuomba kura, bila kujua hili wala lile,kundi hilo lilisaka pesa kwa nguvu, likapanga pesa za 'material' ya kampeni na zikarudi mifukoni mwao," alidai.

Aliendelea kudai "Kama mawaziri walitishwa, wakawa wadogo zaidi ya wanamtandao, kwanini vigogo wa BOT wasitishwe na kuachia mianya kwenye EPA? Hiyo bilioni 133 ni pesa ya akaunti moja tu (EPA) iliyochunguzwa, usishangae kukuta zaidi ya sh. bilioni 800 zimechotwa pale !" alisema.

Kwa mujibu wa mwenendo wa kampeni za mwaka 2005 mwanasiasa huyo alidokeza kuwa ulimshangaza Rais Kikwete ndio maana baada ya kushinda na kuapishwa kuongoza Awamu ya Nne, katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge, alibainisha kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye chaguzi bila kujulikana zinapotoka na kuahidi kwamba katika uongozi wake atahakikisha kila senti inayotumika kwenye kampeni, inajulikana ilikotoka.

Sambamba na hilo Rais Kikwete alisimama kidete na kubainisha wazi kuwa serikali yake haina ubia na mtu zaidi ya Makamu wake, Dkt. Mohamed Shein, kauli iliyotafsiriwa kubaini hila za wanamtandao hao kujikweza ndani ya serikali yake

Source: Gazeti Majira
 
Hii Ni Kali Ngoja Tutafakari Na Nimeanza Kuamini Ile Kauli Ya Dr Slaa Ya Kuwa "siyo Hizo Tu Ni Zaidi Ya Hizo" Ewe Muumba Utusaidie.
 
Interesting old known story. Lakini tunasikia tu wana mtandao lakini hawa jamaa hawawekwi wazi, demage waliyosababisha ni kubwa sana. Nadhani wanawapa mwanya wa kuendelea kuinfluence mambo, wakitajwa wazi itakuwa vizuri zaidi!
 
eti wanamtandao wajue kinachoendelea halafu Mwanamtandao Mkuu asijue kinachoendelea, eti hata Mkapa aliyekuwa amiri jeshi Mkuu na bosi Mkuu wa taasisi nyeti ya usalama wa taifa asijue kinachoendelea.

hii ni katika kujaribu kuspin., ili kumsafisha Muungwana na BMW,
halafu wanajifanya eti source ni waziri aliyetemwa(lengo ni kuongeza uzito wa chanzo cha habari).

Watanzania hatutakubali kudanganywa na vyombo vya habari kama hivi,
 
Nikisoma taarifa hii bila kuchanganya ubongo ni kwamba huyo Waziri alikuwa na nia njema kukiweka chama tawala bafuni kioge kiwe safi. Lakini ukichanganya ubongo unakuta ni jasusi la chama tawala limetumwa kutudanganya wana JF kwamba chama tawala kimesukumizwa katika matope. Haiwezekani na haiingii akilini kwamba Mkapa hakujua kilichoendelea yaani ukombaji wa fedha za BoT alijua sana na ndiyo maana alikuwa akijigamba kwamba chama tawala kitashinda ni dhahiri alijua kwamba atatumia pesa. Haiingii alikini kabisa kwamba Mkapa hakujua je matanuzi yote hayo hakujua pesa zinatoka wapi kwasababu chama tawala hakina chanzo chochote cha mapato zaidi ya BoT. Kwa kuwa huyu Zee la Shamba katumwa kuturubuni wana JF kwa kigezo cha he darely speaks openly, let him reveal his mind to us, but what he says he seems to be a puppet. Puppet ishia hapo hapo usitudnganye sisi tuna akili ya utambuzi. Go back to your sender.
 
Makala hii ina janja ya kumengua MH JM Kikwete kwenye so la EPA.

Mimi siukubali utetezi huo na ninaomba wote tuukatae utetezi muflisi huu.

Kikwete ameshiriki kwenye huu uchafu wa EPA kikamilifu, hizi ni juhudi za mtandao wao kumwosha kwa maji ya tope wakitegemea kumtakasa na kumnusuru na jinamizi la EPA.

Hii ni serikali ya Maharamia,Wahuni na wababaishaji ambao lengo lao ni moja tu; Kudumaza na kudhoofisha maendeleo ya Watanzania na kutengeneza tabaka la viongozi watakao ongoza nchi kwa kupokezana.

Kuna dalili nyingi za watendaji wa serikali kujaribu kumwepusha Kikwete na Majnga ya kujitakia na kumuenzi hata pale asipo sitahili.

Ni kikwete huyu huyu alijaribu kujiosha kwa waumini wa Kikrsto kwamba yeye hana mkono na ahadi za SISIEMU katika ilani yake ya uchaguzi za kuunda aMahakama ya Kadhi na kudai asili ya wazo hilo ni MH Mrema.

Huu nimwaka 2008 Mrema bado yupo SISIEMU?
Tuchukulie kwamba bado yupo SISIEMU, Mrema ana nguvu gani ya kuinfluensi hoja hiyo?
Bila kusita naweza kusema watu wanaojaribu kumwosha rais kutoka kwenye lundo la Uchafu wa SISIEMU ni walevi wa madaraka na ni watu wasio jari matokeo ya uchambuzi wa ushauri wao.

Kikwete mwenyewe anaonyesha udhaifu mkubwa wa upeo wa kushindwa kutathmini mambo mengi yanayo mkabiri yawe ni yake binafsi au ya kitaifa.
Uwezo wake wa kufikiri na kutafakari nadhani ulisha gusa Glass Ceiling siku nyingi zilizo pita. Kazi tuliyomkabidhi iko juu mno ya uwezo wake wa kufikiri, kiasi kwamba ili afikiri na kuamua nini cha kufanya wazembe na maopportunists wengi wanaomzunguka ndio hujitwalia kazi hiyo inayoachwa wazi na uwezo wake kugusa Glass Ceiling limit.

Sikubaliani na maneno ya waziri asiye tajwa katika harakatui zake za kujifanya anafichua siri na katika juhudi zake zilizo msingi wa hoja za kumengua Rais Kikwete kutoka kwenye Uoza wa serikali na chama chake.
 
Hivi ndani ya EPA kuna nini????

Mtiririko wa matukio kuhusiana na EPA yanaifanya EPA liwe ni dubwasha la kutisha ambalo kila mtu analiogopa.

EL na Meghji wakiwa bado wanashikilia nyadhifa zao za zamani waliahidi kuipeleka Bungeni Report ya Uchunguzi wa EPA pindi itakapokuwa tayari. Kikao kilichopita Mama akasoma Press Release ya Mzee Luhanjo ambayo wabunge wote walikuwa nayo tayari.

Kwenye kikao kilichopita Mzee wa Standard (Mh. Sam Six) akadai kwamba majadiliano yanaendelea kati ya ofisi yake na serikali ili waone kama EPA itashushwa Bungeni. Mara akapata safari ya dharura kwenda kwa Bush na kumuagiza Naibu wake asikurupuke kujadili EPA na Richmond, hayo yamsubiri kwa kuwa ni muhimu awepo kwa kuwa ni mazito sana.

Wiki iliyopita Mwanyika akagoma kutaja majina ya mafisadi waliorudisha fedha kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea. (Baada ya hapo nikasema hii ndiyo imetoka, hata Bungeni wataambiwa kwamba Kamati ya Uchunguzi ya Bwana Mwanyika haijakamilisha kazi yake kwa hiyo haifai kuwasilishwa Bungeni).

Leo nimesoma kwenye gazeti Mzee Sam Six anasema "busara ya kamati ya uongozi itatumika kuona kama inafaa EPA ishushwe Bungeni ama wasubiri mpaka uchunguzi ukamilike". Hapo naona alikuwa anawaandaa watu kisaikolojia kwamba kwa kuwa swala linachunguzwa na Kamati ya Rais, subirini kwamba uchunguzi ukamilike ndipo EPA itashushwa bungeni na kujadiliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Swali langu, huu mtiririko wote unaenda sambamba na jinsi Richmond ilivyopingwa danadana kwa miaka 2 na hatimaye bomu likalipuka. Kauli ya Sam Six kwamba EPA na Richmond ni mazito na hivyo mjadala wake lazima awepo Bungeni kunaashiria kwamba kuna bomu fulani. Huko kwenye EPA kuna nini? Kwanini wanazidi kutuongezea longolongo nyingi ambazo nadhani hata watoto wadogo wanaweza kushituka kwamba hapa tunafanyiwa kiini macho na serikali ya CCM. Hakuna mzawa yeyote aliyebahatika kuona hilo dubwasha linaitwa EPA atuwekee hapa japo tujifariji na kujua ni akina nani waliotafuna keki ya taifa bila huruma??????
 
*Adai mtandao uliwazidi ujanja Mkapa, Kikwete mapema
*Uliunda Baraza hewa la Mawaziri miezi 6 kabla ya uchaguzi
*Ulitisha vigogo BoT, wizara na wengine kuahidiwa vyeo

Na Mwandishi Wetu

WIKI chache baada ya kuvunjwa Baraza la Mawaziri na kuundwa jipya kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa kufuatia kashfa ya Richmond, siri nzito katika kashfa ya uporaji wa mabilioni ya pesa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) ndani ya Benki kuu ya Tanzania (BoT),imebainishwa.

Mmoja wa mawaziri aliyetemwa katika Baraza jipya la Rais Jakaya Kikwete, ameliambia gazeti hili kwa sharti la kuhifadhiwa jina kuwa kashfa ya EPA ni nzito na chimbuko lake limejikita baada ya kumalizika mchakato wa kumpata mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mei 2005.

Pamoja na kuunga mkono hoja za wananchi wengi kutaka majina ya mafisadi wanaorejesha fedha kuanikwa hadharani, mwanasiasa huyo alisema jambo hilo ni ngumu kutekelezeka kwa sasa kutokana na misingi iliyojikita ndani ya kashfa hiyo,aliyodai imegusa watu na maeneo nyeti.

"Watu wamejaa jazba, waitazama kashfa ya EPA kama moto uliteketeza mali zao bila kujua chanzo chake na wahusika,"alisema waziri huyo aliteachwa.

Alilitaja kundi la wanamtandao maslahi lililoibuka katika uchaguzi mkuu uliopita na kudai kuwa lilichangia kwa kiasi kikubwa 'kansa ya EPA' ndani ya BoT. Katika mchakato huo, Rais Kikwete,aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga wanachama wenzake 11 waliojitokeza kwenye kinyang'anyoro hicho.

Alidai kundi hilo lililokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Rais Kikwete anashinda mchakato huo,lilikwenda mbali zaidi kwani baada ya uteuzi, lilivuka mipaka na kufanya mambo ya 'ajabu ajabu' kwa siri bila hata mgombea (Rais Kikwete) kujua, wala kuhusishwa.

Alidai kwamba mara tu baada ya kumalizika kwa mchakato huo, wanamtadao maslahi, walipanga safu ya 'Baraza lao la Mawaziri' hadi mabalozi wa nje na kupita huku na kule kutishia na kuahidi nafasi kwa vigogo wengine wa mashirika ya umma na taasisi mbalimbali, zikiwemo za fedha.

"Masikini wakati Rais Kikwete anasimama kwenye majukwaa kuomba kura, watu hawa walifanya vitu vya ajabu sana, bila yeye kujua, walipita huku na kule kutishia watu kwenye nafasi zao huku wakiahidi wengine kuwapa vyeo vikubwa. Walifanya hivyo kama wao ndio wenye nchi, waliunda 'Baraza lao la Mawaziri' miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu uliomuingiza Rais Kikwete madarakani."

"Waalipita maeneo mengi,hata BoT kuwajenga hofu watendaji, hadi mawaziri, makatibu wakuu na vigogo wengine. Hawa walikuwa na wasiwasi kutokana na mageuzi yaliyotarajiwa kutokea baada ya uchaguzi mkuu, wakasikiliza na kutii waliyoambiwa na wanamtandao hao.

" Walijua lazima CCM ingeshinda, wakawa tayari kutekeleza matakwa ya wanamtandao kwa hofu ya kupoteza nafasi zao. Hapo ndipo watu hao wakapata mwanya kuchonga mipango kuanzisha kampuni feki kati ya Mei hadi Januari 2006 kwa lengo la kujinufaisha,"alidai mwanasiasa huyo.

"Kumbuka kipindi hiki kilikuwa kigumu kwa vigogo ambao hawakuwa kwenye kundi la mtandao, walihofia nafasi zao. Kitendo cha kufuatwa na wanamtandao hao, kilifanya wajione kama abiria ambao hawakuwa na tiketi za kusafiri kwa basi la mtandao, sasa wameletewa mlangoni. Wakawa tayari kutekeleza yote waliyotakiwa kufanya, hapa ndipo tatizo lilianzia," kilidokeza chanzo hicho.

Aliendelea kusema" Watu hao (wanamtandao maslahi) wakapanga timu ya kampeni, hawakuiamini ile ya Mangula (Philip, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM). Wakati huo Mkapa (Rais mstaafu, Benjamini) alibaki kama nyoka asiye na sumu, nguvu yake iliporwa na wanamtandao hao bila yeye wala Rais Kikwete kujua.

Chanzo hicho kilifafanua kwamba huenda Rais Mkapa alifikwa na hali hiyo kutokana na matokea ambayo hakuyategemea kwenye mchakato huo.

" Kumbuka Mkapa alipata mapigo mazito mawili baada ya mchakato, kwanza alijikuta ameshindwa 'kumshika mkono'msaidizi wake mkuu upande wa chama, Mzee Malecela (John, aliyekuwa Makamu wake), hali hiyo ikamtokea pia kwa msaidizi wake mkuu upande wa serikali,Bw.Sumaye
( Frederick, aliyekuwa Waziri Mkuu ) ambao wote waligombea na akashindwa kuwabeba. Matokeo hayo yalimchanganya Rais Mkapa, miezi sita ya mwisho ya utawala alikuwa kama ameiweka nchi rehani kwa wanamtandao, walifanya waliyotaka," alidai.

Aliendelea kufafanua" Baada ya kumalizika mchakato na mgombea kupatikana, Rais Mkapa alikosa 'control,' nchi ikawa kama 'imetekwa' na wanamtandao maslahi. Wakati mgombea (Rais Kikwete) anazunguka mikoani kwa nia njema ya kuomba kura, bila kujua hili wala lile,kundi hilo lilisaka pesa kwa nguvu, likapanga pesa za 'material' ya kampeni na zikarudi mifukoni mwao," alidai.
Aliendelea kudai "Kama mawaziri walitishwa, wakawa wadogo zaidi ya wanamtandao, kwanini vigogo wa BOT wasitishwe na kuachia mianya kwenye EPA? Hiyo bilioni 133 ni pesa ya akaunti moja tu (EPA) iliyochunguzwa, usishangae kukuta zaidi ya sh. bilioni 800 zimechotwa pale !" alisema.

Kwa mujibu wa mwenendo wa kampeni za mwaka 2005 mwanasiasa huyo alidokeza kuwa ulimshangaza Rais Kikwete ndio maana baada ya kushinda na kuapishwa kuongoza Awamu ya Nne, katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge, alibainisha kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye chaguzi bila kujulikana zinapotoka na kuahidi kwamba katika uongozi wake atahakikisha kila senti inayotumika kwenye kampeni, inajulikana ilikotoka.

Sambamba na hilo Rais Kikwete alisimama kidete na kubainisha wazi kuwa serikali yake haina ubia na mtu zaidi ya Makamu wake, Dkt. Mohamed Shein, kauli iliyotafsiriwa kubaini hila za wanamtandao hao kujikweza ndani ya serikali yake
Source: Gazeti Majira

Any thing in Red is Big Fat Lie.[/SIZE]

Any thing Bolded is suspicious
 
Kazi tunayo kweli kweli.....sipati picha bubgeni nini kitatokea especially pale ishu kama hizi nitakapo kataliwa kuwekwa wazi until kamati maalumu ya raisi kukamilisha uchunguzi wa vitu vilivyo wazi. Ikiwa mtu anarudisha pesa na kampuni unazijua moja kwa moja na wamiliki wa companies hizo wanajulikana sasa uchunguzi for six month......hapa kuna mashairi yanaandaliwa na wanajipanga na kutafuta chorus nzuri ili wakianza kughani wadanganyika waimbe chorus. Glory to God for JF Community.
 
waziri huyu anaonekana hana akili ya kupima. anafikiri atakuja hapa kumsafisha kirahisi BWM na JK kwa maneno machache bila ya majina au ushahidi wowote?
kama kikwete hayumo kwenye hili au mkapa, na waitowe ripoti hadharani. na pesa zimeibwa kabla kikwete hajaingia madarakani na zimeendelea kuibwa baada, anakataa tu uchunguzi kufanywa wa accounts nyengine
 
"Watu wamejaa jazba, waitazama kashfa ya EPA kama moto uliteketeza mali zao bila kujua chanzo chake na wahusika[/B],"

Chanzo cha moto walikijua, wahusika wanajulikana na watu waliuona moto ukiwaka na kutekeleza mali zao kwa kasi lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kufanya jitihada zozote za kuuzima!

Hata kama kuna ukweli wowote katika haya anayosema muheshimiwa waziri wa zamani, binafsi namuona ni just another bad loser- why is he saying all this cr.p now? Would he have said these things kama angekuwa amepewa nafasi kwenye hiyo cabinet mpya.Im sure he would have kept his filthy mouth shut as if nothing ever happened!
 
Source ya hii habari ni kwenye gazeti la RA, hv inaingia akilini kumsafisha mkapa at ths stage????? Na huyo JK ndiyo kabisaaaaaa.......... Kwa huu upepo wa EPA kuna kila sababu ya kumuhusisha Ben na JK moja kwa moja.

Hawa waandishi wanaojipendekeza pendekeza sijui watakuja kutuambia nini pale ukweli woote utakapojulikana.

God bless TZ!!!!!!
 
Liars, Liars, Liars, Liars, Liars! U Cant Fool Us Anymore, Si Siye Watoto Wa Chekechea, Hiyo Habari Nahisi Imetoka Kwenye Gazeti La Udaku, Imekaa Ki Ijumaa Ijumaa, Tena Ijumaa Wikienda.
 
Source ya hii habari ni kwenye gazeti la RA, hv inaingia akilini kumsafisha mkapa at ths stage????? Jeeeeeeeeez!!!!! Na huyo JK ndiyo kabisaaaaaa.......... Kwa huu upepo wa EPA kuna kila sababu ya kumuhusisha Ben na JK moja kwa moja. MTANDAO UNGEWEZAJE KUPENETRATE NGOME YA BEN, SUMAYE NA KINA KIGODA BILA WAO KUJUA?????????

MTANDAO AMEKUJA NAO JK NA FULL POWER WAKAIPATA BAADA YA USHINDI WA JK WA 2005.

Hawa waandishi wanaojipendekeza pendekeza sijui watakuja kutuambia nini pale ukweli woote utakapojulikana.

God bless TZ!!!!!!
 
If somebody fool you once it is his mistake, but if he fool you twice it is your mistake. Na sisi hatufanyi makosa kuamini hadithi hii ya shule ya Chekechea - na nisiwavunjie hadhi watoto wetu ni hadithi ya kijendaazimu.

Hili limewakwama mafisadi JK na wenzake, wananchi wameenza kuelewa japo kidogo kidogo - hadi mwisho ujulikane.
 
Haya yote ni mazingaombwe ya Kikwete na mwizi na rafiki yake mkubwa Rostam Azizi wanajaribu kujisafisha hapa. Walianza na kununua wahariri wa habari wameona haitoshi, wakakamata wana JF ili kuua mambo, wameanza kuichafua CHADEMA, na sasa wana hili ambalo hata majina hayatajwi.... huu moto unaofukuta ni kazi sana kwao kuuzima, kununua waandishi wa habari si suluhisho.
 
If somebody fool you once it is his mistake, but if he fool you twice it is your mistake. Na sisi hatufanyi makosa kuamini hadithi hii ya shule ya Chekechea - na nisiwavunjie hadhi watoto wetu ni hadithi ya kijendaazimu.

Hili limewakwama mafisadi JK na wenzake, wananchi wameenza kuelewa japo kidogo kidogo - hadi mwisho ujulikane.

huyu mwendawazimu mtikila ndio maneno yake mmeyapa uzito na kuamini kuwa rostam si raia?

tuzungumzie kuhusu kuhusika na ufisadi wake ni sawa ila kuwa si mtanzania no

kumbukeni kuwa alisema hata mkapa si mtanzania na kiukweli huyu jamaa siku anapenda atajwe tajwe sana magazwtini
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom