Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 3
*Adai mtandao uliwazidi ujanja Mkapa, Kikwete mapema
*Uliunda Baraza hewa la Mawaziri miezi 6 kabla ya uchaguzi
*Ulitisha vigogo BoT, wizara na wengine kuahidiwa vyeo
Na Mwandishi Wetu
WIKI chache baada ya kuvunjwa Baraza la Mawaziri na kuundwa jipya kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa kufuatia kashfa ya Richmond, siri nzito katika kashfa ya uporaji wa mabilioni ya pesa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) ndani ya Benki kuu ya Tanzania (BoT),imebainishwa.
Mmoja wa mawaziri aliyetemwa katika Baraza jipya la Rais Jakaya Kikwete, ameliambia gazeti hili kwa sharti la kuhifadhiwa jina kuwa kashfa ya EPA ni nzito na chimbuko lake limejikita baada ya kumalizika mchakato wa kumpata mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mei 2005.
Pamoja na kuunga mkono hoja za wananchi wengi kutaka majina ya mafisadi wanaorejesha fedha kuanikwa hadharani, mwanasiasa huyo alisema jambo hilo ni ngumu kutekelezeka kwa sasa kutokana na misingi iliyojikita ndani ya kashfa hiyo,aliyodai imegusa watu na maeneo nyeti.
"Watu wamejaa jazba, waitazama kashfa ya EPA kama moto uliteketeza mali zao bila kujua chanzo chake na wahusika,"alisema waziri huyo aliteachwa.
Alilitaja kundi la wanamtandao maslahi lililoibuka katika uchaguzi mkuu uliopita na kudai kuwa lilichangia kwa kiasi kikubwa 'kansa ya EPA' ndani ya BoT. Katika mchakato huo, Rais Kikwete,aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga wanachama wenzake 11 waliojitokeza kwenye kinyang'anyoro hicho.
Alidai kundi hilo lililokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Rais Kikwete anashinda mchakato huo,lilikwenda mbali zaidi kwani baada ya uteuzi, lilivuka mipaka na kufanya mambo ya 'ajabu ajabu' kwa siri bila hata mgombea (Rais Kikwete) kujua, wala kuhusishwa.
Alidai kwamba mara tu baada ya kumalizika kwa mchakato huo, wanamtadao maslahi, walipanga safu ya 'Baraza lao la Mawaziri' hadi mabalozi wa nje na kupita huku na kule kutishia na kuahidi nafasi kwa vigogo wengine wa mashirika ya umma na taasisi mbalimbali, zikiwemo za fedha.
"Masikini wakati Rais Kikwete anasimama kwenye majukwaa kuomba kura, watu hawa walifanya vitu vya ajabu sana, bila yeye kujua, walipita huku na kule kutishia watu kwenye nafasi zao huku wakiahidi wengine kuwapa vyeo vikubwa. Walifanya hivyo kama wao ndio wenye nchi, waliunda 'Baraza lao la Mawaziri' miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu uliomuingiza Rais Kikwete madarakani."
"Waalipita maeneo mengi,hata BoT kuwajenga hofu watendaji, hadi mawaziri, makatibu wakuu na vigogo wengine. Hawa walikuwa na wasiwasi kutokana na mageuzi yaliyotarajiwa kutokea baada ya uchaguzi mkuu, wakasikiliza na kutii waliyoambiwa na wanamtandao hao.
" Walijua lazima CCM ingeshinda, wakawa tayari kutekeleza matakwa ya wanamtandao kwa hofu ya kupoteza nafasi zao. Hapo ndipo watu hao wakapata mwanya kuchonga mipango kuanzisha kampuni feki kati ya Mei hadi Januari 2006 kwa lengo la kujinufaisha,"alidai mwanasiasa huyo.
"Kumbuka kipindi hiki kilikuwa kigumu kwa vigogo ambao hawakuwa kwenye kundi la mtandao, walihofia nafasi zao. Kitendo cha kufuatwa na wanamtandao hao, kilifanya wajione kama abiria ambao hawakuwa na tiketi za kusafiri kwa basi la mtandao, sasa wameletewa mlangoni. Wakawa tayari kutekeleza yote waliyotakiwa kufanya, hapa ndipo tatizo lilianzia," kilidokeza chanzo hicho.
Aliendelea kusema" Watu hao (wanamtandao maslahi) wakapanga timu ya kampeni, hawakuiamini ile ya Mangula (Philip, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM). Wakati huo Mkapa (Rais mstaafu, Benjamini) alibaki kama nyoka asiye na sumu, nguvu yake iliporwa na wanamtandao hao bila yeye wala Rais Kikwete kujua.
Chanzo hicho kilifafanua kwamba huenda Rais Mkapa alifikwa na hali hiyo kutokana na matokea ambayo hakuyategemea kwenye mchakato huo.
" Kumbuka Mkapa alipata mapigo mazito mawili baada ya mchakato, kwanza alijikuta ameshindwa 'kumshika mkono'msaidizi wake mkuu upande wa chama, Mzee Malecela (John, aliyekuwa Makamu wake), hali hiyo ikamtokea pia kwa msaidizi wake mkuu upande wa serikali,Bw.Sumaye
( Frederick, aliyekuwa Waziri Mkuu ) ambao wote waligombea na akashindwa kuwabeba. Matokeo hayo yalimchanganya Rais Mkapa, miezi sita ya mwisho ya utawala alikuwa kama ameiweka nchi rehani kwa wanamtandao, walifanya waliyotaka," alidai.
Aliendelea kufafanua" Baada ya kumalizika mchakato na mgombea kupatikana, Rais Mkapa alikosa 'control,' nchi ikawa kama 'imetekwa' na wanamtandao maslahi. Wakati mgombea (Rais Kikwete) anazunguka mikoani kwa nia njema ya kuomba kura, bila kujua hili wala lile,kundi hilo lilisaka pesa kwa nguvu, likapanga pesa za 'material' ya kampeni na zikarudi mifukoni mwao," alidai.
Aliendelea kudai "Kama mawaziri walitishwa, wakawa wadogo zaidi ya wanamtandao, kwanini vigogo wa BOT wasitishwe na kuachia mianya kwenye EPA? Hiyo bilioni 133 ni pesa ya akaunti moja tu (EPA) iliyochunguzwa, usishangae kukuta zaidi ya sh. bilioni 800 zimechotwa pale !" alisema.
Kwa mujibu wa mwenendo wa kampeni za mwaka 2005 mwanasiasa huyo alidokeza kuwa ulimshangaza Rais Kikwete ndio maana baada ya kushinda na kuapishwa kuongoza Awamu ya Nne, katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge, alibainisha kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye chaguzi bila kujulikana zinapotoka na kuahidi kwamba katika uongozi wake atahakikisha kila senti inayotumika kwenye kampeni, inajulikana ilikotoka.
Sambamba na hilo Rais Kikwete alisimama kidete na kubainisha wazi kuwa serikali yake haina ubia na mtu zaidi ya Makamu wake, Dkt. Mohamed Shein, kauli iliyotafsiriwa kubaini hila za wanamtandao hao kujikweza ndani ya serikali yake
Source: Gazeti Majira