Waziri aliyeachwa atoboa siri nzito EPA

Yet another attempt to try remove the president and mkapa from these allegations, wanadhani watu wajinga na hawafahamu ukweli. Those two are in it from the start, anyone remember the dramatic u-turn of mkapa when he gave the speech supporting JK for president, i wonder how much of the EPA money had he received by then to make him do that...
 
JK tangia mwanzo nilijua ni archtec wa EPA.He knew well baada ya kwenfa Paris Club na akajua wapi pa kuchotea .Hakuna wa kuondolewa kwenye hili .Kama ni kweli wayasemayo na yeye hakujua basi awakamate maana ushahidi upo na kesi iende Mahakamani kuna shida gani na yeye ndite Amiri Jeshi mkuu ?
 
Kama hii habari ni kweli, JK kama kweli yeye ni kiongozi safi basi anabidi ajiuzuru kwa kuwa kaingia madarakani kwa pesa za wizi.Tena baada ya kuwaibia watanzania. Kuendelea kukaa madarakani ni kutokuona tatizo na kuhalalisha njia zilizotumika kumuingiza madarakani nim chafu. Hata kama hakujua huko mwanzo mbinu hii haisaidii kumsafisha. Zaidi tunammulika kuangalia uadilifu wake
 
What goes around comes around.

Hii EPA inaweza ikafa na mtu siku moja subirini tuu muone mnafikiri RICHMOND atakufa mwenyewe?
 
Asante sana Waziri uliachwa, kwa haya mambo ambayo inawezekana ni ya kweli kabisa!
Lakini huyu Mwanasiasa si mpiganaji wa wananchi wake na ninaweza kumuita ni mnafiki, kwa sababu haya yote aliyajua toka hata kabla ya uchaguzi, na ameingia madarakani na kukaa miaka miwili bila kuyaeleza haya, lakini leo hii kaachwa kwenye uwaziri ndo anatueleza, huu ni ujinga tena sana
Tunashukuru na kama Kawaida ya JF linafanyiwa kazi, lakini muwe na moyo wa kupigania nchi yenu na kukosoa mambo yote pale yanapotokea, sio baada ya kukosa ulaji ndo mnasema

Ngoja tuone sasa kuhusu hili pia

Huyu waziri kachemsha na wala sio mwanaharakati katika kulikomboa taifa hili linalodidimia kila siku.Angekua na uchungu na TZ hata ule uwaziri angeukataa na kuyasema haya alionayo na sio kusema wakati ambao ameondolewa madarakani.

Je ktk miaka miwili ya uwaziri nini alichoifanyia TZ au sisi WATZ tutamkumbuka kwa lipi.

Lakini kwa utamaduni tuliouzoea wa WATZ,ni kwamba mtu akitemeshwa nafasi za juu ndio wanaanza kutoa siri za nchi,huu ni unafiki wa hali ya juu ambao sio wa kujenga bali kubomoa.Huyu bwana alishindwa kupiga kelele wakati huo akae kimya mnafiki mkubwa.
 
Mjinga hapa ni huyo mwandishi na gazeti waliyoamua kuripoti uchuro kama huo uncritically. Hawa waandishi ndio waliwalisha sumu watanzania kwamba JK alikuwa a special offer direct from the Almighty himself, na ndio haohao wanaohangaika kuhakikisha wanamnyoa JK na madhambi yote yanayoendelea katika ile nchi. Wanatuona sisi ni wajinga kiasi cha kuamini kwamba unaweza ukapita katikati ya tanuru la moto na bado usiungue. Kibaya zaidi kuna watanzania wengi wanaoelekea kukubaliana na huu ujinga, sasa cha kujiuliza mjinga ni hawa waandishi au sisi tuliokubali kudanganywa?
 
Wana JF...

Naomba tunapo tizama uhusika wa JK juu ya EPA tuangalie mambo mawili:

1) Faida gani atakazozipata JK kwenye kujiongezea maadui katika CHAMA - hususan wanamtandao wenzake (ambao wengine amewaua au anakaribia kuwaua kisiasa) ambapo sote tunakubali kua ndio walio changia sehemu kubwa kwa yeye kuweko madarakani.

2) Naomba pia tuangalie namna ambayo EPA na Richmond maamuzi yake alivyoyafanya.

Baada ya kutizama hayo masuali mengine MATATU yanajitokeza:

1) Je JK ni KATILI kiasi kwamba wezi wenziwe wakisha maliza kazi ( hufanya kama ili michezo ya zamani ya kitaliano - ukisha iba uwa wenzio wote mali ule pekeyako) awasafishe?

2) Je JK amekubali walichokifanya na wenziwe kuwa ni kibaya na kwahiyo ameamua kujisafisha yeye kwa kuwatosa wenziwe?

3) Je JK aliambiwa wewe tulia sisi tutafanya kazi yote - wewe kwa upande wako jitayarishe kua The next Raisi wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania?

Kwa mawazo yangu hili la 3 naweza kulipa 80% kua ndicho kilicho tokea - kwa mtazamo wa mambo yanavyo kwenye hivi sasa hapa Tanzania.
 
Mie nafikiri huyu WAZIRI MUACHWA anajikosha ingawa hakupendwa jina lake liwekwe public kwa sababu anaamini kuwa nafasi bado zipo na anaweza kuangaliwa kwa mara nyingine pale anapojitahidi kumsafisha Muungwana. Kwa nini aseme sasa hivi baada ya kutemwa????
Anyway, nafikiri litakuwa jambo la BUSARA kama ACCOUNT zingine za EPA zitakapofanyiwa uchunguzi. Hiki ni Kizunguzungu Macho, naamini ni pesa nyingi imelambwa tu na wanatuzuga kwa Bilioni 133. Hapa tunatakiwa kuwabana wabunge wote ili WAKOMAE huko bungeni kama walivyofanya kwenye ripoti ya Mwakyembe ili kila kitu kiwekwe hadharani
.
 
jamani mbona tunasahau zile ajenda 21,hawa ndio waandishi wanafiki na waliobobea ktk ufisadi. sasa wanatunga hadithi ambazo azinakichwa wala miguuu,kwa kuunganisha hizi habari kutoka hapa hapa jf
 
BAADA YA HUU UJINGA ULIOLETWA HAPA TUNAWEZA KU-PREDICT NINI KITALETWA TENA NEXT.NAFIKIRI KICHWA CHA HABARI KITAKUWA: MKAPA HAKUSHIRIKI KUNYAKUA KIWIRA..AU KIKWETE HAKUSHIRIKI MKATABA WA IPTL NA UTUMBO MWINGINE KAMA HUO.
Nafikiri ndugu yangu umekosea kufikiri hadhira yote ya JF wana vichwa vikubwa lakini ubongo kiduchu.
Hayo yote uliyoeleza hapo hakuna jipya mengi ni nyepesi nyepesi ambazo umeweka kwa makusudi katika jitihada za kupotosha ukweli na kuwasafisha watu waliokutuma.Hakuna asiyejua Mkapa na Kikwete ndio nguzo ya wizi wa BoT na ufisadi wote uliopita,uliopo na unaondelea ndo maana mpaka sasa pamoja na ushahidi wote uliopo hawajathubutu kuacha sheria zifanye kazi kwa sababu wanajua wao hawatakwepa makali yake.
Nakutakia kila la kheri ndugu na wenzio wote katika harakati zako
 
Yaaani article zingine bwana, wakuu JF sasa tunahitaji kuwa macho maana tumeingiliwa, hawa waandishi uchwara sasa ni kuwapiga mawe tu waende an article zao za vichochoroni,

Ukweli ni kwamba sasa hivi bongo kuna kaazi kweli kweli, naiskia viongozi karibu wote wananunua waandishi, kila kona kuna vikundi vya kisiasa vinapigana vita, sasa ni wajibu wetu wananchi kuwa macho on what is ours kwenye hivi vita vyao, ama sivyo tutaishia kua victim wa tusichoelewa, I mean how low can it go?

hizi article za namna hii sasa zimekosa hata pa kuziweka, wanajaribu kuzileta huku, dawa ni kuwapiga mawe, kama kuna waziri ana uchungu na taifa basi aseme yeye ni nani sio asitajwe jina halafu wanaturushia pumba hapa, I mean thanx kwa waliotangulia kwa kuweka hii ishu inapotakiwa.
 
Jamani huyu jamaa mbona anatufanya wana JF wajinga?. Hivi kweli huyo Jakaya Kikwete alifanya kampeni ya nguvu na kifahari bila kujua pesa za kampeni zilitoka wapi na akina nani walimpa pesa hizo?.
Jakaya lazima alijua pesa za kampeni zilitoka wapi na akina nani walitoa pesa hizo. Na bila shaka pesa za EPA ndizo zilizofanya kampeni ya CCM sababu kwanini wahusika katika uchafu huu wanatandikiwa carpet jekundu na kuombwa kwa heshima na taadhima ili warudishe pesa hizo na bila kutajwa majina?. Mpaka sasa kwanini aliyekuwa gavana wa BOT Mr Balali amefichwa?.

Na pia inaonesha kabisa zilizochotwa hapo BOT ni zaidi ya sh bil 133 hivyo watanzania tungeomba uchunguzi ufanywe tena na kwa makini zaidi.
 
Gazeti lililoandika habari hiyo ni MAJIRA la tarehe 17.03.2008.

Mmoja wa wakurugenzi/Waasisi wake ni Mhe. Mbunge wa Mbeya (CCM).
 
Jamani huyu jamaa mbona anatufanya wana JF wajinga?. Hivi kweli huyo Jakaya Kikwete alifanya kampeni ya nguvu na kifahari bila kujua pesa za kampeni zilitoka wapi na akina nani walimpa pesa hizo?.
Jakaya lazima alijua pesa za kampeni zilitoka wapi na akina nani walitoa pesa hizo. Na bila shaka pesa za EPA ndizo zilizofanya kampeni ya CCM sababu kwanini wahusika katika uchafu huu wanatandikiwa carpet jekundu na kuombwa kwa heshima na taadhima ili warudishe pesa hizo na bila kutajwa majina?. Mpaka sasa kwanini aliyekuwa gavana wa BOT Mr Balali amefichwa?.

Na pia inaonesha kabisa zilizochotwa hapo BOT ni zaidi ya sh bil 133 hivyo watanzania tungeomba uchunguzi ufanywe tena na kwa makini zaidi.

Gazeti la Rostam Azizi, kuweni makini kwenye kuliangalia hili, kuna kitu kinatafutwa ama kinasafishwa....Balile upoooo
 
Yaaani article zingine bwana, wakuu JF sasa tunahitaji kuwa macho maana tumeingiliwa, hawa waandishi uchwara sasa ni kuwapiga mawe tu waende an article zao za vichochoroni,

Ukweli ni kwamba sasa hivi bongo kuna kaazi kweli kweli, naiskia viongozi karibu wote wananunua waandishi, kila kona kuna vikundi vya kisiasa vinapigana vita, sasa ni wajibu wetu wananchi kuwa macho on what is ours kwenye hivi vita vyao, ama sivyo tutaishia kua victim wa tusichoelewa, I mean how low can it go?

hizi article za namna hii sasa zimekosa hata pa kuziweka, wanajaribu kuzileta huku, dawa ni kuwapiga mawe, kama kuna waziri ana uchungu na taifa basi aseme yeye ni nani sio asitajwe jina halafu wanaturushia pumba hapa, I mean thanx kwa waliotangulia kwa kuweka hii ishu inapotakiwa.

Mkuu ES,

Hio ndio maana ya Cheque Book Journalism!

Na kwa hali ya TZ sasa hivi baadhi ya waandishi ni matarishi tu.

Uandishi wao ni uliojaa ubabaishaji, udaku na sasa kwa mimi nimeondoa "credibility" kwao.
 
..kuna tabia ya ajabu sana ya uongo-uongo inajengeka miongoni mwa waandishi wa habari na watumishi wa serikali.

..hii inanikumbusha ile habari iliyotoka Ikulu kwamba Kikwete amesitisha ziara ya Raisi wa Uturuki.

..WHY? Kama waandishi hawana la kuandikia ni bora wakae kimya kuliko kutunga mambo ya uongo kama haya.
 
JK fisadi,Mbowe Fisani!Kila kiongozi nchi hii fisadi!tume laaniwa?

Viongozi kuwa Mafisadi si laana ya nchi ni laana yao Viongozi.
Endapo Wananchi wote tu Mafisadi,jambo ambalo haliwezekani, ni kweli nitaikubali hiyo laana.

Dawa ya kuumaliza Ufisadi wa viongozi ni kutumia haki zetu kama raia wa Tanzania (KURA)kuwanyima madaraka ya kuongoza nchi na kuwa diminish personality zao mpaka level iliyochini ya heshima waliyonayo Wafungwa.

Kwa maana hiyo, naomba mimi na wenzangu kadhaa tunao kesha tukitafakari mambo ya Tanzani,kukataa rasmi hiyo laana na kuwaachia ninyi mnao tetea Viongozi waliojaa mawazo yenye Uoza na Udumavu mjivishe kama Joho la heshima.
 
Yaaani article zingine bwana, wakuu JF sasa tunahitaji kuwa macho maana tumeingiliwa, hawa waandishi uchwara sasa ni kuwapiga mawe tu waende an article zao za vichochoroni,

Ukweli ni kwamba sasa hivi bongo kuna kaazi kweli kweli, naiskia viongozi karibu wote wananunua waandishi, kila kona kuna vikundi vya kisiasa vinapigana vita, sasa ni wajibu wetu wananchi kuwa macho on what is ours kwenye hivi vita vyao, ama sivyo tutaishia kua victim wa tusichoelewa, I mean how low can it go?

hizi article za namna hii sasa zimekosa hata pa kuziweka, wanajaribu kuzileta huku, dawa ni kuwapiga mawe, kama kuna waziri ana uchungu na taifa basi aseme yeye ni nani sio asitajwe jina halafu wanaturushia pumba hapa, I mean thanx kwa waliotangulia kwa kuweka hii ishu inapotakiwa.

Mkuu es mwambie jamaa huyu aende kule Darhotwire kama utabahatika kumuona .Hapa habari kama hizo haziuziki maana kwanza sie wenyewe tuna andaia very investugative info kuliko zao na kwa kifupi sana .
 
Makala hii ina janja ya kumengua MH JM Kikwete kwenye so la EPA.

Mimi siukubali utetezi huo na ninaomba wote tuukatae utetezi muflisi huu.

Kikwete ameshiriki kwenye huu uchafu wa EPA kikamilifu, hizi ni juhudi za mtandao wao kumwosha kwa maji ya tope wakitegemea kumtakasa na kumnusuru na jinamizi la EPA.

Hii ni serikali ya Maharamia,Wahuni na wababaishaji ambao lengo lao ni moja tu; Kudumaza na kudhoofisha maendeleo ya Watanzania na kutengeneza tabaka la viongozi watakao ongoza nchi kwa kupokezana.

Kuna dalili nyingi za watendaji wa serikali kujaribu kumwepusha Kikwete na Majnga ya kujitakia na kumuenzi hata pale asipo sitahili.

Ni kikwete huyu huyu alijaribu kujiosha kwa waumini wa Kikrsto kwamba yeye hana mkono na ahadi za SISIEMU katika ilani yake ya uchaguzi za kuunda aMahakama ya Kadhi na kudai asili ya wazo hilo ni MH Mrema.

Huu nimwaka 2008 Mrema bado yupo SISIEMU?
Tuchukulie kwamba bado yupo SISIEMU, Mrema ana nguvu gani ya kuinfluensi hoja hiyo?
Bila kusita naweza kusema watu wanaojaribu kumwosha rais kutoka kwenye lundo la Uchafu wa SISIEMU ni walevi wa madaraka na ni watu wasio jari matokeo ya uchambuzi wa ushauri wao.

Kikwete mwenyewe anaonyesha udhaifu mkubwa wa upeo wa kushindwa kutathmini mambo mengi yanayo mkabiri yawe ni yake binafsi au ya kitaifa.
Uwezo wake wa kufikiri na kutafakari nadhani ulisha gusa Glass Ceiling siku nyingi zilizo pita. Kazi tuliyomkabidhi iko juu mno ya uwezo wake wa kufikiri, kiasi kwamba ili afikiri na kuamua nini cha kufanya wazembe na maopportunists wengi wanaomzunguka ndio hujitwalia kazi hiyo inayoachwa wazi na uwezo wake kugusa Glass Ceiling limit.

Sikubaliani na maneno ya waziri asiye tajwa katika harakatui zake za kujifanya anafichua siri na katika juhudi zake zilizo msingi wa hoja za kumengua Rais Kikwete kutoka kwenye Uoza wa serikali na chama chake.

Mkuu inabidi nikutafute nihesabu mvi kichwani kwako maana inaonesha una akili kama wembe.
They lied to us and the want to wash our brain.... hii haikubaliki
Pia kuhusu EPA naona kuna kamchezo kanafanywa kuikuza ionekane kama dubwashika kuuubwa ili watusahaulishe ripoti kamili ya BOT.
Iletwe ripoti isomwe hapa ili tujue yaliyomo. Waache kudili na vijisenti huku minoti ikiyeyuka ktk vipengele vingine vya ripoti hiyo.
JAMANI CAN WE DEMAND THE WHOLE REPORT?
 
Kama kuna mtu aliingia madarakani kwa kutumia EPA hana budi kungoka kwa EPA, hata kama aliingia amefungwa macho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom