Waziri aliyeachwa atoboa siri nzito EPA

Uandishi wa kuambiwa cha kuandika na Bwana Mkubwa toka serikalini ni uandishi tegemezi na ni uandishi ambao siku zote utasimama kwa utegemezi.

Kufanya jambo kwa kutegemea mtu, kikundi au hali fulani ni umasikini wa fikra ambao utatuzi wake, ni kuandika kile ulichokitafiti mwenyewe kwa akili yako na kuijaza akili yako utajiri wa fikra na hekima.

Nasema ni uandishi tegemezi ni umasikini wa fikra kwa sababu akili ya mtu yeyote duniani iliumbwa kujitegemea katika kuwaza na kuamua.

Waandishi wa habari ambao kwa makusudi au kwa kuendekeza njaa zao wanaamua;
kupokea Fedha au vitu vya thamani kama magari au nyumba,kupokea huduma fulani za kukidhi haja kama kulipiwa masomo au gharama za kusafiri nje au kuwekwa kwenye list ya misafara ya viongozi nje na ndani ya nchi,kupokea aina yeyote ya upendeleo utakao wawezesha kupanda chart katika fani zao na mbele za Watanzania, hufanya hivyo huku wakiimarisha jitihada za kujichimbia kaburi wao binafsi na taaruma zao.

Mwandishi wa habari anayefanya kazi yake kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari siku zote atatumika kama Taa katika giza nene,kama Mwavuli wakati wa mvua, kama kiyoo cha kujisafi pia kama Sauti ya Sauti za wanyonge.

Mwandishi wa gazeti huru au TV huru hafungamani na upande wowote kwa sababu kazi yake ya awali ni kutoa maelezo sahihi ya kilicho tokea.

Mwandishi wa chombo kisicho huru na kinachofungamana au kumilikiwa na kundi lenye hisa katika siasa au biashara fulani zaidi ya ile ya habari, siku zote ataandika habari zinazolinda Maslahi ya vyombo vinavyoigusa kazi yake na maslahi yake.

Pamoja na ukweli kwamba mwandishi wa Gazeti au TV hategemewi kuwa mstari wa mbele kuandika habari mbaya juu ya Gazeti lake au TV yake, Vivyo hivyo mwandishi huyu hategemewi kwamba hawezi sita kuandika habari mbaya zinazo husu magazeti mengine au vyombo vingine vya habari.

Uandishi wa habari unajitokeza Tanzania sasa hhivi si mgeni sana, katika duru za uandishi wa habari.Uandishi tegemezi umekuwepo nchini kwa muda mrefu tangu kabla ya ukoloni kung'olewa na baada ya kujitwala kwa miaka mingi.

Zamani Wahariri wa magazeti walilazimishwa kuandika habari za namna fulani tu ili kulinda Maslahi binafsi ya viongozi wa serikali. Viongozi wa serikali walikuwa na uwezo mkubwa wa kidikteta wa kuingilia Uhuru wa vyombo vya habari na kuviamulia nini cha kuandikwa katika kila habari waliyo itoa.

Enzi hizo zimepukutika na kuyoyoma na wakati.
Nisemapo uandishi huu tegemezi si mgeni nina maana kwamba zamani vyombo vya habari vililazimika kuwa tegemezi kwa kibano cha serikali.
Leo hii uandishi tegemezi haujajengwa juu ya kibano cha serikali tu. Uandishi tegemezi umejengwa juu ya tamaa au mvuto wa Fedha chafu zinazo sambazwa na wezi wachache ndani ya Serikali ya SISIEMU ili kuyalazimisha magazeti yaandike kile wao Maharamia wanataka.

MWandishi anapewa vitisho na hata Kubenewa kama hatishiki na wala haogopi kufa basi ataonyeshwa burungutu kubwa la fedha ili kumlegeza. Njaa kiu na hofu ya kesho mara zote hugeuka ndoana ya kumuopoa Mwandishi masikini huyu kutoka kwenye BWawa la maji safi ya haki(sheria).

Fedha za kuhonga hazikosekani hata siku moja.

Kuna hizi za RDC $152,000.00 zinazoingia kila siku. Kuna zaidi ya $1000,0000.00 zinazoibiwa TRA kila siku. kuna $250,000.00 za Utalii maliasili na uvuvi zinazoibiwa kila siku.

Mwandishi akiendelea kugoma kupokea fedha hizo Vitisho vinarudi tena, na safari hii si vitisho ni pamoja na kusakamwa na kuzushiwa kashfa mbali mbali hata zinazohusu Ukilanja kule Mzumbe sekondari na umonita darasa la pili kule Kwiro Primary school.

Mapambano ya kununua waandishiwa habari yanaweza fanikiwa tu endapo Uhuru kama Uhuru utapigwa kitanzi na sisi wana JF tutashonwa midomo na mikono yetu na vibaraka wachache hapa JF.

Uandishi Tegemezi huu utaonja mauti hivi punde.

Kitendo cha Tanzania kuienzi Demokrasia na kuunda sheria ya vyama vingi na kupanua wigo wa kutoa maoni, ni chachu, na ni hamira ndani ya mchanganyiko wa purukushani zote Tanzania ambayo taratibu inaumua ukweli wa mambo na kuupenyeza sambamba na matukio mpaka pale utakapo jaza mabonde ya upungufu na kuenea kila kona na kila penye pengo la ufahamu.

Waandishi wa habari waliotegemea kuandika kwa kuuliza watendaji wa serikali kwanza wanapwelea au wamejitoa jumla katika mbio za uandishi wa habari kwa sababu habari zao zimeshindwa kuwa Gumzo mitaani. Waandishi tegemezi wa enzi ya utawala wa kiimla wanaendelea kushindwa kwa sababu ya kuto kuwa na utamaduni wa kutafuta habari kwa kudadisi na kutaka kujua asili na ukweli wa matukio.

Utgemezi katika habari ni kujichimbia kaburi.

Waandishi wa habari ambao leo hii wameamua kuwa tegemezi kwa sababu za kiuchumi nao nilazima waelewe kwamba utegemezi huo utakufa siku na saa ambayo wao watakuwa wamejiegemeza kwa 100%.

Ni Afadhari uwe mwandishi wa matukio ya vijijini; matukio yanayo husu juhudi za wananchi kujikwamua kiuchumi yasiyo na mvuto kwa wasomaji wengi, kuliko kuwa mwandishi mashuhuri kabisa katika safu zinasomwa na watu wengi lakini huandiki kile unacho kiamini wewe bali kile wanacho kiamini Mabwana walio kutuma.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA NA WAKOMBOZI NI MIMI NA WEWE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom