Wazimbabwe wanamdhihaki Rais wa Tanzania?

Wazimbabwe wanamdhihaki Rais wa Tanzania?

Wamwache katarist wetu watafute chakula chao kwanza walizora kulishwa na wazungu!!! Ila atafutwe mwalimu wa lugha miaka kumi no ingilish ikwulu haipendezi,hatakama anawazo zuri atakaa kimya wanapojadili masuala na mabalozi na wakuu wengine
 
Mkuu samahani lakini naona kama unahamisha magoli, swala la watu kuiba sijajua hapa limefikaje, pili pronunciation ya mtu siyo ishu iliyoko mezani, jiwe/mimi/wewe / mchina hatuwezi kuwa na pronunciation sawa. Ok turudi kwenye ishu ya msingi ambayo ni mtu kuwa na PhD ambayo aliifanya kwa kiingereza lakini mtu huyo huyo hajui hiyo lugha
Kama hiki unachokisema hakiwezekani, namaanisha kuwa na PhD ya kiingereza wakati wewe hujui Kiingereza basi hilo tuwaulize waliompa PhD. Lakini nakuhakikishia taaluma zinatofautiana sana! Ndo maana kuna watu wamefanya PhD za lugha ya kiswahili lakini zimeandikwa kwa kiingereza.
 
Ndio lugha inayofundishwa toka msingi na kukomaa zaidi sekondari hadi chuo na ni lugha rasmi ya nchi kutokuijua ni fedheha kwa usomi wako usiponielewa muulize mkulu
Umejiuliza kwa nini michango ya wana JF ni ya Kiswahili, hata kama Thrd ni ya kiingereza?
 
Kuna English ya kusomea na kujibia mitihani na hii kwa elimu ya Tanzania ni kitu cha kawaida na ndio maana utakuta Mtu ana 1 ya 3 PCM au PCB lkn hawezi jieleza kwa kiingereza kilichonyooka. Advance tumesoma na watu walikua wanapiga sana ngeli na hadi kwenda nje ya nchi coz shule yetu kila mwaka watu walikua wanachaguliwa kwenda Germany. Ingekua kiingereza ndio akili kama unavyowaza basi Wale jamaa wangepiga 1 au pass kali lkn maajabu yake wengi ni ZERO au four mbovu. ELIMU ya Tanzania na habari za kujua kiingereza ni vitu viwili tofauti na nina mifano mingi ktk hili.
Najaribu kuangali wana JF wakongwe huko nyuma wamechangia mara ngapi kwa kiingereza. Ajabu ni kwamba hata thrd za kiingereza wanachomoka kwa kiswahili. Tuna tabia ile ya kuamini Ukishapiga lugha ya kiingereza basi, wewe kiboko. Wengi hapa JF hawanyooshi kiingereza chao lakini hawako tayari kupokonywa digrii zao, tena wanazitaja kwa maringo ya usomi.
 
Umejiuliza kwa nini michango ya wana JF ni ya Kiswahili, hata kama Thrd ni ya kiingereza?

Wengine huchagua kuandika kwa Kiswahili kama mimi binafsi, lakini wengine pia wanakiri hawakwenda shule. Wanasema kwamba hawakwenda shule wakimaanisha kama umesoma utajua kukiongea kwasababu utafundishwa shuleni.
 
Siku zote Kenya watatupiku tu na kuchukua ajira kila kona huku sisi tukiingiza lafudhi na silabi kutoka lugha za mama zetu kwenye hicho tukiitacho: "Kiswahili"

Mimi nadhani tatizo siyo lafudhi; watu wameamua tu kupuuza misingi ya lugha.
 
Unaonekana kilaza kwa sababu Kiingereza ni miongoni mwa lugha zetu rasmi.

Kiswahili ni lugha yetu rasmi ya ndani. Kiingereza ni lugha yetu rasmi ya ndani na kimataifa. Kimataifa tunawasiliana kwa Kiingereza (mataifa mengine wanawasiliana kwa Kifaransa, Kispanish, Kijerumani, Kirusi, Kichina, n.k.). Kwetu sisi kama hujui Kiingereza, katika ngazi ya kimataifa unaonekana wa ajabu maana ni sisi wenyewe tumeeleza kuwa miongoni mwa lugha zetu rasmi, Kiingereza kinapewa nafasi ya kwanza. Tunatumia English, kunafundishia masomo, na ndiyo tunayoitumia katika sheria zetu pia.
Hapa ndipo wanaomtetea wanasahau
 
Acheni ushamba kujua kiingereza sio dili kwanza sikuhizi ni kama zilipendwa miaka ya tisin hiyo walikuwa wanaonekana wajanja kipindi hicho ata ukimuona mzungu njiani unaona kama kitu cha ajabu ni vyema tukosoe vitu vyenye tija vya maendeleo kwa taifa wadau
sasa hayo maendeleo unayapataje kama huwezi kuwasiliana,ungejua hata msosi bado tunaagiza toka huko kwa wanaoongea kiingereza usingetokota hivi
 
msigwa akasema raisi kaongea kingireza yani alikosa chakuripoti kabisaa
kwa sababu wanajua hakijui,hivyo alivyoweza kumwaga hata hiyo broken wakaona mgonjwa anaanza kupata nafuu hivyo ni Bora wawajulishe wadanganyika
 
Kama hiki unachokisema hakiwezekani, namaanisha kuwa na PhD ya kiingereza wakati wewe hujui Kiingereza basi hilo tuwaulize waliompa PhD. Lakini nakuhakikishia taaluma zinatofautiana sana! Ndo maana kuna watu wamefanya PhD za lugha ya kiswahili lakini zimeandikwa kwa kiingereza.

Mkuu toka form one unaitumia hiyo lugha mpaka unapata PhD na bado lugha inakupiga chenga tena chenga kweli kweli afu useme hakuna tatizo hapo??
 
Hivi ni kwanini kwa hapa nyumbani usopojua kiingereza unaonekana kilaza??
Kwa sababu umesoma miaka 3 kwa lugha hiyo ukapata Bachelor's, miwili Masters na miwili PhD ukiacha Secondary na High School. Miaka yote hiyo bado lugha ipige chenga? Kuna walakini lazima!
 
English ni ya wazungu ss chetu kiswahili, ni ujinga na upumbav kumcheka mwafrica asojua kimombo
 
Magu kiingereza hakijawahi mwacha salama hahahaha
Siku chache zilizopita Rais alikutana na Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa. Moja kati ya vitu alivyovitaja ni kuwa yeye ni catalyst katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe.

Tatizo likaja kwenye lafidhi ya matamshi ya Kiingereza. Jinsi alivyolitamka neno catalyst lilisikika kama cataryst sababu iliyopelekea watu kutoa maneno ya mzaha kwenye YouTube. Mtu mmoja alichangia kwa kuandika, "We r waiting to see the effects of the catarist".

View attachment 1114345
 
Back
Top Bottom