Wazimbabwe wanamdhihaki Rais wa Tanzania?

Nakupinga sana.JK before being presidaa alikuwa yupo juu sana tuu,nimeona clip fulani akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa akiongea na mabalozi wawakilishi,jamaa kakomaa na lugha ya malkia utadhani anaongea kiswahili tu very relaxed kabisa
Nakumbuka hata Jk alipoingia madarakani alikuwa na Poor English, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda alikuwa ana improve . huyu wameshindwa kumpiga msasa angalau cha kuombea maji tu? Dar hapo kuna wale jamaa wa English Fountain kama wapo, ameshindwa kuwaita kama ameshindwa yeye kwenda angalau jioni?
 
English nzuri waitoe wapi wazimbambwe watu wenyewe 'the' wanatamka 'zeh' wana accent mbovu aijawahi tokea duniani ata ya Magu nzuri.

Mwisho siku liwe somo kwa wahusika wanatakiwa kuchukua precaution measures zote kuakikisha raisi adhiakiwi kwa uzembe wa mipango yao.

I blame Prof Kabudi
Ha ha ha ha ha miafrika huu ndo ugonjwa unaotumaliza mie nikiongea na mzimbabwe ninakuwa agitated kwa accent utadhani wako wanaongea kisauzi . Ati nao wanachonga nafuu yetu watanzania hatuna accent mzito
 
Mimi nadhani tatizo siyo lafudhi; watu wameamua tu kupuuza misingi ya lugha.
Hapana Mkuu, si kweli kuwa ni uamuzi wa hiyari, hapana. Kuna mahali wataalamu wa Kiswahili katika Wizara ya elimu wameacha kutimiza wajibu wao.
Miaka ya 60 na 70 Kiswahili kilitiliwa mkazo sana shuleni. Walimu walifundisha ufasaha wa lugha yenyewe. Kila Mwanafunzi alitakiwa kuzungumza Kiswahili na si Kisukuma au Kizaramo. Leo hii kila mwenye lugha yake anaingiza silabi kwenye Kiswahili.
Mfano: Mkurya hana silabi zenye "l" bali ana "r"
Matokeo yake ni kutumia neno "rara" badala ya "lala"
Halikadhalika Wasukuma hawana "r" bali wana "l," hivyo kwao neno: "Ramadhani" hutamkwa: "Lamadhani." Kuna wachangiaji humu nimeona wanatumia maneno bila kujali athari ya matokeo yake. Mfano neno: "awana" haliwezi kuwa na maana sawa na neno: "hawana."
Mbaya zaidi ni kwamba kundi linalopaswa kulinda "Lugha" kama tunu ya Taifa, kundi la watawala na "elites" (wanataaluma), nalo ndilo haswa halijitambui, linapuyanga tu utafikiri nao ni watu wa mtaani kwetu!!!!
 
Sijui kama wewe ulisoma miaka hiyo unayozungumzia. Wakati huo lugha za nyumbani zilikuwa zinazungumzwa zaidi kuliko hata sasa. Tofauti na sasa ni kwamba wale waliokwenda shule na kufundishwa Kiswahili au kiingereza walijitihadi kuwa tofauti kwa kuzungumza na kuandika lugha hizo kwa ufasaha; hawakupuuzia. Kutokana na umakini huo hata athari za lugha ya mama zilipunguzwa sana. Leo hii umakini umepungua sana. Mwanzoni tulifikiri ni kwenye kiingereza tu kumbe na kiswahili pia. Sidhani kama kuna Mwalimu anafundisha "araka" badala ya haraka au "alafu" badala ya halafu! "Amasa" badala ya hamasa! Vijana wamejiendekeza tu na hatimaye kulemaa na kuharibu lugha.
 
Vema mkuu, japo bado nasisitiza kuwa watawala na wasomi ndio haswa kundi linalopaswa kulinda "Lugha" katika Taifa lolote duniani. Mkiwa na Taifa ambalo viongozi na wasomi wake hawajali namna wanavyoitumia lugha, basi utakuwa unajenga jamii ya watu wasiojali katika kila nyanja.
 
Back
Top Bottom