Elections 2010 Wazee wamgeuka Malecela - Wanataka Asigombee Ubunge

Anastahili aibu hiyo. Tatizo viongozi wetu kulewa madaraka na kujiona kuwa wataendelea kuwepo kwenye nyadhifa zao milele. Nadhani ni fundisho kwa wengine wenye mawazo kama hayo.
 
Sijui kwanini watu wanadhani kuwa kutopata kura za kutosha kwenye uchaguzi wa kura za maoni ni kushindwa uchaguzi katika jimbo lake.

Bado anayo nafasi ya kuteuliwa kutetea kiti chake. Anaweza kupendekezwa kuwa mgombea wa Jimbo hilo na chama chake, na mshindi wa kura za maoni akawekwa pembeni.

Si imewahi kutokea?
 
Vipi Mzee akiamua kugombea kupitia CUF! I am trying to think out of the Pandora box
 
Leo nilikuwa nafuatilia News kutoka Gazeti letu THE CITIZEN.. nikaona picha kuuubwa ya muheshimiwa sana John Malecela. na kuona maandishi makubwa yakiandika MALECELA'S FALL: WHT IT MEANS.. " it could be an indication that people are tired, not only with old faces, but also CCM as a Party'

nikaendelea kutafuta Informations nikaona kwenye Blog moja inasema "Mkongwe wa siasa Tanzania na mbunge wa zaidi ya miaka 35 John Malecela amebwagwa katika Jimbo la Mtera na Kijana mdogo ambaye anaweza kuwa ni kama mtoto wake.

Sasa hii siaibu hii?

Silver
Mwache mzee akapumzika.
Amelitumika taifa lake kwa heshima zote na sasa mwaache apumzike na sio wa kumcheka.
 
Sijui kwanini watu wanadhani kuwa kutopata kura za kutosha kwenye uchaguzi wa kura za maoni ni kushindwa uchaguzi katika jimbo lake.

Bado anayo nafasi ya kuteuliwa kutetea kiti chake. Anaweza kupendekezwa kuwa mgombea wa Jimbo hilo na chama chake, na mshindi wa kura za maoni akawekwa pembeni.

Si imewahi kutokea?

I agree, its not over yet. Watasema mambo hayawezi kwenda bila ushauri wa wazee!!!
 
Leo nilikuwa nafuatilia News kutoka Gazeti letu THE CITIZEN.. nikaona picha kuuubwa ya muheshimiwa sana John Malecela. na kuona maandishi makubwa yakiandika MALECELA'S FALL: WHT IT MEANS.. " it could be an indication that people are tired, not only with old faces, but also CCM as a Party'

nikaendelea kutafuta Informations nikaona kwenye Blog moja inasema "Mkongwe wa siasa Tanzania na mbunge wa zaidi ya miaka 35 John Malecela amebwagwa katika Jimbo la Mtera na Kijana mdogo ambaye anaweza kuwa ni kama mtoto wake.

Sasa hii siaibu hii?

Silver

Aibu kivipi nyie watu mbona mna mambo ya ajabu??? siasa ni kijiti kupokezana yaani lazima kuna kushinda na kushindwa!
Kwamba hakusoma alama za nyakati si kweli! kwani ameshindwa kwa kura chache sana hii inaonyesha bado wana mtera walikuwa wanamuhitaji hajabwagwa kama kina shelukindo na selelii! (najua kwa kuwataja hawa nimechafua hali ya hewa ila jamani ni mfano tu)
Binafsi namouna kama shujaa kwani anajiamini kuwa na nguvu za kutumikia nchi yake bila kujali umri wake....asingependa kucheza na wajukuu zake miaka 5 ijayo illihali ana uwezo wa kusimama na kujenga hoja bungeni KAMA AMBAVYO WENGI WALITAMANI AFANYE HIVYO. Anguko lake ni anguko la mwanasiasa yeyote hapa duniani jamani
......slaaa au jk wakianguka mtasema hawakusoma alama za nyakati? nyakati nini by the way!
Hongera kwa kukubali matokeo mzee malecela nategemea utakumbukwa tu baada ya october 31 'mshauri wa rais ......,
mix with yours
 
Mzee hataki kujifunza kwa wazee wenzake kama kina Msuya, Warioba, Salim A nk. Sasa kustaafishwa na watu ni tofauti na kustaafu mwenyewe kwa hiari. Maana raha ya kustaafu kwa hiari unabakia na sifa za kuwa mshauri ila ukistaafishwa kama John hata ukapewa nafasi ya kuwa mshauri hiyo inanabaki kuwa unapakwa mafuta kwa mgogo wa chupa. Labda tuseme tingatinga halisikii maumivu haraka maana tinga hili liliwahi kupigwa minyundo na Jk Nyerere ikaonekana kana kwamba JKN anampigia mbuzi gitaa asiyewezakuelewa tofauti za sauti ili acheze. Na kweli hakucheza. Na kwa hili sii ajabu akashinikiza kaupendeleo ka kuteuliwa na mheshimiwi ili nae akauchape pale mjengoni kama mzee Kinje.
 
Nadhani CCM wanapaswa kujifunza kutokana na anguko la mzee Cigwiyemisi J. S. M, kwamba wananchi wakidhamiria, hakuna mbuyu wala tingatinga litakaloshindikana kuangushwa..., not even CCM itself.
 
Sijui kwanini watu wanadhani kuwa kutopata kura za kutosha kwenye uchaguzi wa kura za maoni ni kushindwa uchaguzi katika jimbo lake.

Bado anayo nafasi ya kuteuliwa kutetea kiti chake. Anaweza kupendekezwa kuwa mgombea wa Jimbo hilo na chama chake, na mshindi wa kura za maoni akawekwa pembeni.

Si imewahi kutokea?

Kwavile kazi imekwisha huko Mtera nadhani Field Marshall sasa atarudi ili atupashe vitu vilivyomsibu babu!! Ingawa baada ya kushindwa chances za kurudi mjengoni ni very slim lakini bado atakuwemo mjengoni kwani mama kapeta kule Same; ilimradi mama asije akabadilisha mwelekeo kwa vile mzee kalost!!
 
[COLOR="blueMtazamo wangu mimi ni kuwa Mzee Chigwiyemisi atarudi mjengoni kupitia kapu la Rais. Hawa watu hawatupani kihivyo. Pamoja na kuwa kuna wakati alikuwa akienda tofauti na JK lakini ukizingatia historia ya mzee huyo sio rahisi wamtose kihivihivi tu. Huyo mzee amesha save post karibu zote za siasa ndani ya nchi yetu ukiacha hiyo tu ya Urais. Amekuwemo kwenye kamati ya ulinzi na usalama kwa muda mrefu saana labda kushinda wengine wote katika CCm, so anayajua mengi mazuri na mabaya ya CCM. Hivyo ni rahisi kwao kumvumilia ili kulinda siri zao kuliko kumtosa akatoa siri nzito."][/COLOR]. Mama Chigwiye misi ameshajeruhiwa, amepenya kwenye tundu la sindano. Hivyo ule moto aliokuwa nao kwenye bunge lililopita hautoonekana tena this time kama ataweza kukitetea kiti chake. Maana atakitumia kipindi hicho kujiandaa kuachana na ubunge hapo 2015.
 
Sijui kwanini watu wanadhani kuwa kutopata kura za kutosha kwenye uchaguzi wa kura za maoni ni kushindwa uchaguzi katika jimbo lake.

Bado anayo nafasi ya kuteuliwa kutetea kiti chake. Anaweza kupendekezwa kuwa mgombea wa Jimbo hilo na chama chake, na mshindi wa kura za maoni akawekwa pembeni.

Si imewahi kutokea?
What message CCM would be sending? I don't think they would opt for such a catastrophic decision on our young demecracy. Maana kutakuwa hakuna umuhimu wa kuwahi kuamka ili ukapige kura
 
Inafanya mtu ujiulize maswali mengi.
Mtu umesakuwa PM. Maana utakula na kunywa pesa za walipa kodi mpaka kifo. Lakini bado mtu huyu hataki kumalizia nguvu zake kwa kustaafua na kuwa mfano wa kilimo kwanza kwa wnachi wake.Nguvu zake zote anataka kumalizia kwenye siasa. Mhhhh.

Hivi ni wabunge au mawaziri wangapi wana mashamba ya japo ya hekari mbili ya mifano?

Serikali inahubiri kilimo kwanza wakati wakubwa wenyewe wanachofanya ni mali kwanza. Magari, Viwanja na majumba mijini.
 
Ulevi wa madaraka ndio unaowafanya wadhani kuwa walizaliwa wawe madarakani siku zote na kujikuta wanaadhiriwa bila hodi. Ulevi huo huo ndio ilio nao CCM, na hivyo itaadhirika kwa mtindo huo huo.

Kumbuka somo la katuni hii hapa iliyotoka mwezi wa tatu mwaka huu.

attachment.php

Katuni+March+28.jpg
 
Back
Top Bottom