Wazee wamgeuka Malecela - Wanataka Asigombee Ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazee wamgeuka Malecela - Wanataka Asigombee Ubunge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Regia Mtema, May 7, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Habari nilizosikia asubuhi hii toka ndani ya udondozi wa magazeti katika gazeti la Nipashe ni kuwa John Malecela-Mbunge wa Mtera ameshauriwa kutogombea Ubunge tena katika uchaguzi wa mwaka huu.

  Habari zinadai kuwa Wazee hao wa CCM wamesema kuwa Malecela amekuwa Mbunge kwa muda mrefu hviyo inatosha ni vyema akaacha kugombea mwaka huu na kubaki kuwa mshauri muhimu.

  Wazee hao wameenda mbele na kudai kuwa pamoja na kuongoza kwa muda mrefu lakini bado jimbo hilo halina maendeleo ya kuridhisha.

  Haya wazee ndio wamechachamaa.

  Habari zaidi baadaye baada ya Nipashe kuwa mtandaoni.
   
 2. w

  wasp JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu amekuwa Professional Member of Parliament for the last 35 years and would like to continue being a Member of Parliament for life and enjoy a hefty salary plus other fringe benefits associated with the post.
   
 3. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Miaka 35 kama MP ameachieve nini kwa manufaa ya wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla? Je anataka kugombea tena ili akakamilishe yepi kwa manufaa ya wengi ambayo hakuweza kwa miongo zaidi ya 3 na nusu aliyodumu kama MP?
   
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  waende waachie vijana he? kwani walizaliwa kuwa wabunge hadi wafe?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mimi nashauri Malecela apewe ubunge wa heshima. Akae mle mjengo mpaka kufa kwake. Si huwa wanafanya hivyo hata kwenye chama chao kwa nia ya kuwaenzi huwa wanawakaribisha ndani ya vikao?
  Kumbukeni hata hivyo alisema mbinu za ushindi anazo zaidi ya 1000 hivyo lazima arudi bungeni kwa kuchaguliwa na hao wagogo.
   
 6. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Wazee 48 kweli ndiyo kielelezo cha kusema kuwa wazee wa Mtera wanataka mzee Malaecela asigombee ubunge?Wazee 48 wanawasemea wazee zaidi ya ma elfu wa Mtera jamani?Kikao gani ambacho kitajumuisha wazee hadi wa CCM then watamke na kumteua kijana wa CHADEMA agombee ili amtoe Mzee Malecela?

  kweli wazee wa CCM-mtera sasa wamemchoka malecela hadi waipishe CHADEMA?hii haiingii akilini na tumtendee haki mzee wetu huyu na kwa haraka haraka mm nahisi wazee hao ni wa Chadema na hawahusiani hata kidogo na mchakato wa ccm kumpata mgombea ubunge wa Mtera!
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Malafyale usipende kujenga hoja kwa kutumia hisia.Kwanini udhani kuwa wazee hao ni CHADEMA wakati Nipashe limetamka wazi ni wazee wa CCM na ukumbuke kuwa gazeti Nipashe lina mahusiano mazuri na Malecela na Kilango wake.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Malafyale

  Hivi pale Diamond Jubilee kulikuwa na wazee wangapi kuwakilisha watanzania mil.40 sijakusikia ukisema haiwezekani Rais aongee na watu 800 tu halafu aseme wamewakilisha taifa zima, halafu hawa ni wazee wa CCM si wa upinzani kama ulivyokariri.
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee inawezekana ana matatizo fulani haiwezekani uwe wewe tu unapendwa siku zote, mtu anazaliwa anakukuta mbunge anaoa anazaa bado wewe mbunge anakaribia kupata wajukuu wewe bado mbunge na bado unasema eti watu wanakupenda ueendelee i think something is wrong upstairs hata ukomunist haukuwa hivyo, wewe hadi wazee wenzako wanakuchoka awe basi na ile aibu ya kawaida.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Luteni hapa umenikuna.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Malafyale nadhani ingekuwa busara kama ungeelekeza ushauri na nguvu zako huko kwenu kwani wenzako wamekuandalia bajeti ya kuwafanya wasokile wakuondoe mjengoni!! Usishangae, habari ndio hiyo; utajistukia umekufa kifo cha mende!!
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Operesheni sangara tu hali hiyo...!watu wa Mtera msimkatae Malecela tu, yeye si tatizo saaana, chama chake ndiyo hakikufaeni tena...chagueni mtu mwingine kutoka chama chengine mbadala na CCM aliyokuwakilisheni Malecela kwa mda mrefu bila ya faida yoyote zaidi ya tumbo lake.
   
 13. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Nukuru toka Gazeti la Majira/Mtanzania 5-6-2010""Wazee hao waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika baa maarufu ya Kibarua eneo la Uhindini mjini Dodoma walijitambulisha kuwa wanachama wa CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Tanzania Labour Party (TLP) walisema Malecela ambaye amekuwa bungeni kwa miaka 35 sasa amechoka kiakili na kimbinu""

  Hapo mimi ndipo nimechoka;ina mana sasa vyama jimboni Mtera ikiwemo CCM vimeungana kutaka kumng'oa Malecela wa CCM?Ni hulka ya CCM kwa wanachama wake hasa wazee kuungana na upinzani kumng'oa Mbunge wao?Tuwe makini jamani kwani hili ni changa la macho kwa asilimia zote!
   
 14. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Bulesi ina maana huamini utafiti wa REDET waliosema jimboni kwangu Mbunge wangu yupo safe?
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Malyafale

  Kwani ni dhambi au uhaini kwa wazee wa CCM kuungana na wa upinzani kutetea masilahi yao, toa mawazo ya kiuhasama hujasikia mtu na mke wake wanatoka vyama tofauti, halafu inaonekana wewe ni mzanzibari maana nasikia huko walikuwa hata hawazikani lakini hata hivyo siku hizi nao wameelimika hawana uhasama tena naona umebaki wewe lakini kwavile uko humu JF taratibu nawe utaelimika.
   
 16. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wazee hao waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika baa maarufu ya Kibarua eneo la Uhindini mjini Dodoma walijitambulisha kuwa wanachama wa CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Tanzania Labour Party (TLP) walisema Malecela ambaye amekuwa bungeni kwa miaka 35 sasa amechoka kiakili na kimbinu.

  Wazee hao walikwenda mbali na kumuomba mmoja wa makada wa CHADEMA anayejulikana kwa jina la John Lameck kujitokeza na kugombea nafasi hiyo.

  Kwa mujibu wa wazee hao walioonekana wakiwa na ajenda ya kumuunga mkono Lameck ambaye ni mtu mwenye msimamo tofauti na viongozi wengine ambao wamekuwa wakiyumbishwa kwa tamaa zao na kujikuta wanawasaliti waliowaweka madarakani na kuwafanya kuwa maskini wa kutupwa.

  My take:

  Ni wazi kuwa hawa ni wazee wanaomuunga mkono/kumfanyia kampeni Mr. Lameck wa CHADEMA; wanamsimamo dhabiti katika hilo au waliwezeshwa tu-ukizingatia ni bar na baada ya kuongea na waandishi wa habari walijipongeza kwa kinywaji?wataendelea kumuunga mkono mpaka wakati wa uchaguzi?wanaushawishi gani kwa wana mtera?...time will tell, but dont be too quick to trust.
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hakuna sababu ya kujipa matumaini hewa operation sangara ilishapoteza makali, kimsingi Chadema ilikuwa na momentum kubwa sana kuanzia pale Bunge lilipoboronga kwenye suala la Buzwagi na endapo momentum ile ingeendelezwa vizuri Chadema ingekuwa na nafasi nzuri sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Lakini tukiwa wakweli na nafsi na fikra zetu momentum ile ilikufa mwaka jana na kwa sasa haina ushawishi iliyokuwa nao 2007/2008 na ndio maana Kikwete ameweza kusema aliyoyasema wiki iliyopita bila hofu, kushindwa kuliona hilo na kulifanyia kazi ili kuleta mwamko mpya katika chama na kurejesha upya imani iliyokufa itakuwa ni sababu ya kifo cha Chadema.
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  May 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Jifariji baba.Unajidanganya unazungumza vitu vya kufikirika.
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  kwahiyo, nawewe unataka kujidanganya kuwa CHADEMA inaubavu wa kulitoa tingatinga Mtera?
   
 20. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijaandika hayo kwa kuitakia mabaya Chadema bali kwa hali halisi on ground inayokatisha tamaa sana, shine your eyes....
   
Loading...