Elections 2010 Wazee wamgeuka Malecela - Wanataka Asigombee Ubunge

Wazee hao waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika baa maarufu ya Kibarua eneo la Uhindini mjini Dodoma walijitambulisha kuwa wanachama wa CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Tanzania Labour Party (TLP) walisema Malecela ambaye amekuwa bungeni kwa miaka 35 sasa amechoka kiakili na kimbinu.

Wazee hao walikwenda mbali na kumuomba mmoja wa makada wa CHADEMA anayejulikana kwa jina la John Lameck kujitokeza na kugombea nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa wazee hao walioonekana wakiwa na ajenda ya kumuunga mkono Lameck ambaye ni mtu mwenye msimamo tofauti na viongozi wengine ambao wamekuwa wakiyumbishwa kwa tamaa zao na kujikuta wanawasaliti waliowaweka madarakani na kuwafanya kuwa maskini wa kutupwa.

My take:

Ni wazi kuwa hawa ni wazee wanaomuunga mkono/kumfanyia kampeni Mr. Lameck wa CHADEMA; wanamsimamo dhabiti katika hilo au waliwezeshwa tu-ukizingatia ni bar na baada ya kuongea na waandishi wa habari walijipongeza kwa kinywaji?wataendelea kumuunga mkono mpaka wakati wa uchaguzi?wanaushawishi gani kwa wana mtera?...time will tell, but dont be too quick to trust.
So what kama wazee wa vyama vyote hivi including CCM yenyewe wanamuunga mkono Lameck then it is obvoius kwamba jamaa anakubalika.We shida yako ni kwani?mbona unatfutafata sana.Ulishachemsha CHADEMA then fanya mambo mengine..Unajipa presha bureeee,kupambna na chama kubwa kama CHADEMA,utawezaaaaaaa.
 
Ushauri peke yake hautoshi, Kama kweli hawa wazee wamemchoka mzee malecela asiwe mbunge wao watuonyeshe kwenye uchaguzi wa oct, kwa nini tuandikie mate na wino upo!!
 
Wazee 48 kweli ndiyo kielelezo cha kusema kuwa wazee wa Mtera wanataka mzee Malaecela asigombee ubunge?Wazee 48 wanawasemea wazee zaidi ya ma elfu wa Mtera jamani?Kikao gani ambacho kitajumuisha wazee hadi wa CCM then watamke na kumteua kijana wa CHADEMA agombee ili amtoe Mzee Malecela?

kweli wazee wa CCM-mtera sasa wamemchoka malecela hadi waipishe CHADEMA?hii haiingii akilini na tumtendee haki mzee wetu huyu na kwa haraka haraka mm nahisi wazee hao ni wa Chadema na hawahusiani hata kidogo na mchakato wa ccm kumpata mgombea ubunge wa Mtera!

Nadhani thread hii imejibiwa kwa vitendo na "wazee" wa mtera
 
So what kama wazee wa vyama vyote hivi including CCM yenyewe wanamuunga mkono Lameck then it is obvoius kwamba jamaa anakubalika.We shida yako ni kwani?mbona unatfutafata sana.Ulishachemsha CHADEMA then fanya mambo mengine..Unajipa presha bureeee,kupambna na chama kubwa kama CHADEMA,utawezaaaaaaa.
mbunge wangu, punguza kidogo lugha hizi wewe sasa ni public figure usijisahau sana
 
mbunge wangu, punguza kidogo lugha hizi wewe sasa ni public figure usijisahau sana
Anajishusha hadhi huyu dada, kesha anza kuchemsha chemsha na lugha za mtaani. Kaamua kujianika jina lake, inampa umaarufu lakini pia inakuja na gharama ya kujiheshimu.

Saa nyingine huwa nawaza, hivi msalie mtume Dr. Slaa akishinda urais, CHADEMA wataunda serikali na kina nani, watu kama huyu dada, na Sugu, na Mnyika, na Nakaaya Sumari?
 
Sawa Mkuu hayo ni mawazo yako.Umesoma vizuri au unadandia gari kwa nyuma?unaelewa maana ya kujishusha wewe?hivi kwani kiongozi hana moyo jamani?hebu acheni kuwa wanafiki,kwa bahati mbaya sana huwa siwezi kuwa mnafiki hata kidogo.Eti nikasirike halafu nisionyeshe kukasirika kwangu kisa eti public figure,ooh no.Hebu kuweni practical jamani tuache UNAFIKI.
 
Yesu na Mariaaa!

Hiyo ndio maana ya kutafuta ofisi za umma. Hujajifunza kwa Shy-Rose, sasa hivi wewe hata ukiambiwa unatafuta mume unatakiwa usirushe ngumi, kibao kitakugeukia wewe!

Tena kwa wewe inabidi ufanye kazi mara mbili, ukiwakawaka wanaume wa mfumo dume wa kwetu watasema aah, hawa wanawake mtima ndio zao. Huwezi kujiingiza kwenye mipasho mipasho halafu watu wakakuchukulia kama mtu makini. Moja ya sababu kubwa Obama (hata Kikwete pia) kushinda ni kwa vile alionekana hana hulka ya kuwaka waka ovyo. Tuliza boli. Madongo utakayopigwa yatakusaidia.

Na kumbuka CCM hawajaanza "vita" bado, wamo humu, Makamba atachapisha kurasa zako unazo waka waka atasema ni watoto wa mtandaoni hawa hawana lolote zaidi ya mipasho. Isitoshe bado mtandao wa Tanzania uko chini ya wingu la Utamu, watatujumlisha. Unacheza na chama chenye uzoefu toka walipoanza kuhangaika na Waingereza 1929?
 
mmmh yangu macho. NAONA KAMPENI ZIMEANZA, CHA MUHIMU TUSITOANE MACHO, TUBISHANE KWA HOJA:doh::bowl::yield:NADHANI NIMEELEWEKA
 
Mimi nashauri Malecela apewe ubunge wa heshima. Akae mle mjengo mpaka kufa kwake. Si huwa wanafanya hivyo hata kwenye chama chao kwa nia ya kuwaenzi huwa wanawakaribisha ndani ya vikao?
Kumbukeni hata hivyo alisema mbinu za ushindi anazo zaidi ya 1000 hivyo lazima arudi bungeni kwa kuchaguliwa na hao wagogo.
Ameikosa hiyo heshima maana hata kama akipewa ni baada ya kugaragazwa. Hilo ndio tatizo la kukosa hekima ya kusoma alama za nyakati. Kwangu mimi TingaTinga bado ana heshima kubwa. Ila amekosea kutoona au kuamua kudharau ukweli kuwa wazee wakae pembeni badala ya kuendelea kuwa political machinery mpaka dakika za mwisho.
 
Leo nilikuwa nafuatilia News kutoka Gazeti letu THE CITIZEN.. nikaona picha kuuubwa ya muheshimiwa sana John Malecela. na kuona maandishi makubwa yakiandika MALECELA'S FALL: WHT IT MEANS.. " it could be an indication that people are tired, not only with old faces, but also CCM as a Party'

nikaendelea kutafuta Informations nikaona kwenye Blog moja inasema "Mkongwe wa siasa Tanzania na mbunge wa zaidi ya miaka 35 John Malecela amebwagwa katika Jimbo la Mtera na Kijana mdogo ambaye anaweza kuwa ni kama mtoto wake.

Sasa hii siaibu hii?

Silver
 
Aibu kubwa mno, tatizo hawezi kusoma alama za nyakati. mbona wakina mzindakaya waliamua kuachia mapema maana walishaona upepo umebadili uelekeo.
 
Kwenye kugombea kuna kushinda na kushindwa.....mbona Matumla sasa hivi watu wanamdunda tu na hataki kustaafu....ndio hivo tena
 
Ndio tatizo la wanasiasa wetu wa nchi hii,wanataka wazeekee Bungeni bila kujali kuwa kuna watu wengine hasa vijana ambao wana uwezo mkubwa tu wa kuwawakilisha wananchi.
Natumai mpaka sasa bado ch..... inambana na haamini kilichotokea.
 
Back
Top Bottom