Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Mkuu Crown iliopiga mzinga Dodoma recently watu wanne walikufa hapo hapo. Alipona mmoja abiria alikaa mbele.
My point ukipiga kishindo heavy na lori au bus kupona ni majaliwa uwe mbele au nyuma.
Ilikuwa nyeupe sio? Kama 2 weeks ago? Nilipita alfajiri nilikuwa naenda Moro, nikaiona imewekwa pembeni imeisha vibaya mno nikajisemea wamekufa watu bila shaka maana imebonyea mpaka nyuma.

Aliipiga wapi ile gari?
 
Jana usiku kabla ya Kabuku kuna mwenye lori ilikuwa atuue. Ingekuwa nimewahi sekunde tano tu leo nisingekuwa hapa naandika haya.
Ilikuwa kwenye kona na kwasababu giza lilishaingia nilikuwa mwendo fulani mdogo around 80kph nikaipita bodaboda inatembea pembeni.
Mbele kidogo naibuka kwenye kona naona Mita kadhaa mbele malori mawili yanaligi yananijia moja imejaa kwangu ilikuwa head-on collision! Nikawahi kufunga breki kali Lori linakuja tu nikaitoa gari pembeni ya barabara natizama bonde. Mwenye lori alikuja hadi Mita kama mbili tu akamlazimisha mwenzie akamchomekea kunikwepa mimi.
Wakati nahangaika hivi bodaboda nyuma yangu hajui nini kinaendelea akaniovateki akakutana na lori ikabidi yeye na abiria wake waingie kwenye bonde! Lori likaendelea na safari. Bodaboda waliinuka ila waliumia maana niliona wanachechemea huku wakijishika viuno! Mungu mkubwa.
Ila Bongo kwa kweli Mungu huwa anatuongoza tu nyakati nyingine, na hizi alama zetu za majani barabarani tena wakati mwingine wayakuta ndani ya umbali mfupi kweli kufikia kilipo kicheche/tatizo mmmh. Moja nishaikutaga Bwawani pale usiku kama saa 5 na ushee hivi nimepandisha tu kuelekea Moro jamaa ndio wametoka kupasuana luckily kuna waliokua barabarani kutahadharisha madereva wengine kwa tochi ili wapunguze mwendo ilisaidia sana ile maana pale wengi huwa wanapanda nayo nzima nzima aisee. By the way nimejifunza nafikiri pia ni muhimu sana kuwa na tochi ya tahadhari kwenye gari aisee sio nyakati zote tochi ya kwenye simu itafaa.
Usiku + Vicheche ni combination moja hatari sana.

Last trip nilikuwa nimeiva usiku kwenye saa 4 naitafuta Sekenke, hakuna gari mbele yangu, ukatokea msururu wa magari kutoka upande wa pili tupishane nao, wa mbele akawa ananiflashia high beam constantly japo nilishazima high beams, nikaanza kupunguza mwendo na kuwa attentive.

Kumbe kuna kicheche mbele yangu, yeye alikotoka amekiona anajaribu kunishtua, sasa kinyume chake yale mataa yake yakawa yananitoa kwenye focus kuangalia mbele yangu naishia kuhangaika na flashes zake, kuja kushtuka majani haya hapa! Bahati nzuri nakaaga katikati ya barabara so nikayakwepa na niliyavaa kiaina nikawa nasikia harufu yake ndani ya gari.

Kunisaidia angeflash mara moja na kuzima taa nione vizuri. Kumflash mtu mara kumi kumi kwamba kuna kicheche mbele ndio kabisa unamzuia kukiona.

Kupishana usiku at high speed ni sanaa ya aina yake
 
Kuna vicheche vinaachwa kwenye mazingira hatarishi sana, giza likiingia barabara zetu hizi ni hatari sana. Kuna Mzee wa usiku Kwa usiku simuoni humu
East Wind
 
Nafikiri anawalenga wasio na uzoefu wa udereva hasa kwa kuangalia nguvu na wepesi wa magari husika. Umiliki kama gari ya kwanza kwa dereva mzoefu ni heri tu wala si jambo

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Kwani unafikiri wanaonyooshwa na ni hizo gari wanaangukia kundi gani? Vijana au wamiliki wa Kwanza. Wapo watu wazima wengi wana hizo gari ila hutasikia wamepata ajali kama tunazosikia za hao vijana.
 
Back
Top Bottom