Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Halafu wabongo wengi hawafahamu matumizi ya hizi led bulbs kwa ajili ya high beams. Wengi wanatumia bulbs ambazo siyo public road-legal. Matokeo yake ndiyo hayo ya kuumiza macho madereva wengine na hata kusababisha ajali.
Hizi taa hazifai kabisa. Kuna kipindi walikuwa wanakamata magari yenye hizi taa sijui operation imeishia wapi?
 
Shida ni limited vision. Watu wanasema taa nzuri ila trust me ukipishana na gari kuna few seconds unakuwa blind hapo kama kuna kichanja mbele unajificha mvua.
Sasa Sisi wazee wa 150+ Hali hii si salama hata kidogo
kesho saa sita usiku naanza safari, juma nne asubuhi saa mbili nina kikao.. ndio raha ya usiku kikao kikisha nalalaaa weweee.. usingizi ukiisha naanza safari tena..
 
Mimi hii trip ya juzi nilipasua tairi ya nyuma kulia kilomita chache baada ya mzani wa dumila.

Hiyo ilikuwa usiku mishale ya saa 6 kasoro na nilikuwa mwenyewe, spidi ndogo tu maybe 120 kuna kashimo nilikaona kadogo kumbe kana kingo kali.
Kuingiza mguu hapo ulitoka mlio nikajisemea sidhani kama tairi zimepona. Sekunde chache baadae nikapata matokeo yangu nyuma kumelala.

Tatizo la pale barabara nyembamba mno, hamna nafasi ukingoni kusema usogeze gari. Hata ule mstari wa njano wa kingo ya barabara hamna. Istoshe kuna majani marefu yameota mpaka lami inapoanzia, na kuna bonde ukingoni... nadhani mtakuwa mmevuta picha. Yani kusogeza gari pembeni ya barabara haikuwa option.

Japo niliweka triangle mbali kidogo na kuwasha hazard, nilipokuwa nikiweka spea nikiona gari inakuja nanyanyuka kwanza maana mwili wangu ulikuwa barabarani kabisa.

Tairi ilikufa ile aisee maana nilitembea nayo ikiwa imelala kama mita 100 kutafuta parking. Huwezi amini nilizunguka maduka kibao Dodoma kutafuta 225/55R17 hawakuwa nazo. Nilikuja kuipata mchana japo nimeifunga kishingo upande maana haina rating ya treadwear, traction na temperature
Dodoma bado sana, sehemu za uhakika ni Mwanza na Dar es Salaan
 
Safari njema.
P10506-113508.jpg
 
Asante Mungu ni mwema sikupata shida, nikabadilishiwa ball joint, weka spare tyre na baada ya masaa kadhaa safari ikaendelea...

Kuna wakati pia maeneo ya Iringa, nilikuwa nafanya ligi na jamaa mmoja hivi usiku yule mtu anatembea kama anawahisha gazeti...

Nipo kwenye kimteremko fulani kikali, gari imewaka na mshale wa speed hauna mahali zaidi pa kwenda...nikasikia kishindo puuuuu, tairi ya nyuma imeivaa na ishaita inarusha rusha mapande tu...

Kilichobaki hapo ni kubalance gari itulie na ikasimame yenyewe bondeni...

Sent using Jamii Forums mobile app

Aaiseeeh, polee.

Mungu aniepushie mbali yasinikute.

Ila kuwa mwanamke raha, nakumbuka ilikuwa mida ya saa 11 jioni nakaribia mataa ya tegeta wazo way tairi ika pancha, nakumbuka alitokea kaka hata simfahamu akaniombea chance nikatoka upande wa kulia na kupaki karibu nanile sheli. Akaniambia spea tairi iko vizuri nikamwambia ndio, lete spana jeki...

Keshaleta mawe kaweka kwenye tairi huyo ndani ya dakika 5 tayari. Nikawa naogopa ntamlipa shilingi ngapi maana hatukuoatana bei, alipomaliza nikamwambia unandai shilingi ngapi akakataa akavuka barabara huyoo akaondoka.

Sikuamini kuwa amenisaidia hivi hivi tuu, nikaendelea njia nzima natabasamu hadi nyumbani.

Sijui kama wanaume wanasaidiaga wanaume wenzao bila kiwachaji.
 
Back
Top Bottom