Wazee wa ‘Road Trip’ mpo?

Ilishawahi nitokea kama hii.

Gari ilikuwa harrier tako la nyani ya mshkaji.

Niliweka mafuta kama ya 50K. Nikajua gauge itapanda mbeleni.

Namrudishia gari akalalamika nimerudisha bila mafuta. Ikabidi nimrushie 50 ingine aweke. Akaenda kuweka mzigo ukaruka mpaka full.

Akajisikia vibaya kinoma. Akataka kurudisha mpunga, nikamwambia akaushe.
 
Sidhani. ...

Tena wa kike ndio laini, sister angu alishamsaundisha traffic wa kike mm nilikuwa sijafunga mkanda na akaeleweka. Traffic aliishia kusema next time asirudie
Traffic wa kike watu poa sana.

Niliwahi mpita traffic wa mmama njia ya moro. Akanisimamisha nikasimama mbele sana. Ikabidi nirudi. Akaniongelesha vizuri sana jinsi ilivyo hatari kukimbiza gari. Nikampa 30 ya kumuonea huruma.

Ndo traffic pekee mpaka sasa aliewahi hata kuongea vizuri na mimi.
 
Duh 30,000 nzima! Kuna mwenzio mwingine humu alitoa 50,000/-. Mimi sometime wananiomba namuachia 5,000/- tu
 
Duh 30,000 nzima! Kuna mwenzio mwingine humu alitoa 50,000/-. Mimi sometime wananiomba namuachia 5,000/- tu
Yule alikuwa mama mtu mzima kidogo.

Nika-assume atakuwa na majukumu ya kifamilia.

Alikuwa porini kidogo halafu peke ake.

Na cha zaidi aliongea na mimi vizuri sana. Kama mama ananipa mawaidha.

30k nikaona hata haikutosha.

Mara nyingi traffic wa kike nawamudu sana. Sijawahi andikiwa faini na traffic wa kike.

Wengine naomba namba kabisa.
 
Oh mashimo yameongezeka? Na usiku kuona mbali ni issue. Mara ya mwisho nilisafiri jioni nikapata msala saa 12 ndio ilikuwa pona yangu vinginevyo ningelala barabarani hadi asubuhi. Sisafiri tena usiku.
Ukisafiri usiku nidhamu ya mwendo inahitajika, ukizoea myendo ya magari ya Ulaya inakuwa tabu kwelikweli.

VW Gt uliiuza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…