Mkulu alishasema yakipungua ukubwa yasiongezwe tena.
Nilifanikiwa kupita njio hiyo wakati ikijengwa kabla lami haijafika Sumbawanga.
Kulikuwa hakuna matuta kama yaliyopo sasa bali kulikuwa na rasta tu, tena zile rasta za kuchimbwa chini, hivyo gari hupita vizuri tu na kutetema kidoogo kuashiria kivuko cha wenda kwa miguu mbele.
Lakini baada ya kukamilia yakawekwa matuta ya kufa mtu.
Eeee, walikuwa na sababu nzuri ya kufanya hivyo, ajali zilikuwa nyingi za magari kuanguka na pia ajali za wanavijiji kugongwa mara kwa mara.
Ni jambo la kawaida sana ukipita hata saa tisa za usiku kukuta wanakijiji wamekaa ama kusimama katikati ya lami wakipiga stori. Yani wamekufa wengi kwa kugongwa.
Ila kwa miaka hii tayari wanavijiji wamejifunza, hivyo hakuna haja ya kuwekwa matuta meeeeengi kama ilivyo bali yaachwe machache tu sehemu muhimu lakini alama na michoro ya barabarani iongezwe.