Wazee wa ligi. Dar - Mbeya

Wazee wa ligi. Dar - Mbeya

ligi ipo dar -mwanza pia...ukute Happy Nation, Super Sammy, Enzi hizo pia kulikuwa na Allys wewe acha wewe.....
 
New force ndio balaa wameleta gari mpya ZING TONG tarehe 31 december zilikwenda KAHAMA zinatembea balaa Scania inapitwa kama imesimama kwanza engine kubwa mpaka mizani gari inazidi kilo mia tatu,watu hawazijui hizo gari vizuri.
 
Rekebisha kidogo, hizi basi ni ZHONG TONG, ukitaka kujua balaa la hizi basi,kamuulize omary msigwa mmiliki wa super Feo, ufalme wa super Feo uko mashakani Songea. Super Feo zinatoka stand saa 12:00,new force zinatoka saa 12:30 lakini Yutong za Feo zinachanwa hata kabla ya kufika Njombe! Hawa New Force ujanja waliotumia ni kuchukua Madereva wazoefu wa njia waliokua Ottawa.
 
Mbona madereva wao ni waswahili tu mkuu...hawa wachina walichofanya ni kuwekeza wenyewe nchini na wanashusha mabasi zero kilomita, na yakifikisha kilomita kadhaa wanayapiga sell kwa wamiliki wa kibongo, unadhani hapo kuna basi litatamba barabarani?
 
Zhong Tong Bus ni habari nyingine kabisa, ikikupita iache utapasua injini bure..
 
Attachments

  • 1420620212544.jpg
    1420620212544.jpg
    104 KB · Views: 170
SAIBABA za kusini ni kama daladala zinaokoteza abiria kila mahari njiani. pia anaweza kuondoka stand mda wowote gari likijaa abiria

Mkuu acha kabisa mwaka jana mwezi wa kumi abiria tulitaka kumchapa makofi dereva. Stendi kuu mbeya tumeondoka vizuri akaja kututelekeza stendi ya pili nimeisahau jina kama daladala bhana.
Tulivyoondoka alikimbia kiasi cha kutisha tukawapita wengi ila kufika kwenye kizuizi fulani kikubwa basi likazuiwa na trafiki sababu linakimbia mno. Zuio la dakika kama 20 liliisha baada ya kulipa faini, mpaka tunafika Dsm mabasi yote yameshapoa na injini.
Wapumbavu kabisa hao ni heri nitumie bajaj kwenda Mbeya kuliko huo ujinga...
 
Kuna mashine moja ya Happy Nation nyuma imeandikwa "Voice of Manka". Hicho ni kisu, mwisho wa maneno. Sijajua hiyo scania engine yake ilifanywa nini. Hiyo ndo kiboko ya gari zote za Mbeya, iringa na Songea.
Ipo siku na Mbinguni litawawahisha bila wasiwasi
 
Mbona madereva wao ni waswahili tu mkuu...hawa wachina walichofanya ni kuwekeza wenyewe nchini na wanashusha mabasi zero kilomita, na yakifikisha kilomita kadhaa wanayapiga sell kwa wamiliki wa kibongo, unadhani hapo kuna basi litatamba barabarani?
Hujanielewa mkuu, nilikuwa namaanisha wameajiri madereva waswahili waliokuwa madereva wa mabasi ya Ottawa kampuni ya mabasi ya songea-dar iliyokufa.
 
Hujanielewa mkuu, nilikuwa namaanisha wameajiri madereva waswahili waliokuwa madereva wa mabasi ya Ottawa kampuni ya mabasi ya songea-dar iliyokufa.

Ok nadhani hapo ndipo hatukuwa sawa, ahsante kwa taarifa. Nilidhani ni kutoka ule mji wa nchi za mbele.
 
hiyo ligi ni ya basi mbili tu Happy Nation na Nganga Xpress ....hao ndio wafalme wa njia kwa sasa...uzuri wa nganga ni kuwa madereva wake wako makini sana...na gari zao zina nguvu ajabu hasa ile T413 AVU
 
dah hata sijui yuko wapi yule jamaa... ila kama ulikuwa unamfahamu nadhani unaweza ukawasimulia wanajf kidogo fujo za yule jamaa..... afu alikuwa anautani mwingi sana njiani though nachompendea mimi ni kuwa alikuwa makini..

Mkuu umenikumbusha zamani Giliki yupo alipigwa marufuku kuendesha mabasi alikuwa kwenye malori kakaa sana kwa Mzee Mt huwel Iringa na mara ya mwisho alikuwa kwa Delina group ila wametibuana tena nazani ataenda kwa mtoto wa Huwel anaitwa Abdala.umenikumbusha ligi ya Songea wakati huo yupo Mzee Okala Sele pioni Marehemu John Africa huyu alikuwa anaendesha Special sleeping video coach mzee mambo Lwambo wengine nimewasahau hadi mzuka unipande wakati matrafiki hawana tochi.busi za songea kuna kiswele Special sleeping video coach ikaja mwendowasaa ikaja kilimanjaro mengine nimesahau ila ktk njia zote Tanzania Dar-Songea ndio ngumu sana
 
na wakiwaingiza bondeni au uso kwa uso na semi trailer mje kuwasifia humu!!!
 
Hyo ligi hapo ni happy nation galaxy ndo mwisho wa matatizo,kuna mdau kaitaja" sauti ya manka"hizo zote zina engine scania gia8 then bodi ni ndogo,abiri 60 kwa ukubwa wa engine ile ni kama ipo tupo!!!
 
Back
Top Bottom