Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Usidanganye watu, JK kukutana na wazee ni utamaduni wetu Tanzania wa siku nyingi, nakukumbusha tu kwamba awamu zote tokea ya kwanza ya Mwalimu JK, Mzee Ruksa na Mkapa wote wamekuwa na utamaduni huo wenye heshima. Na sio kwamba wazee hawana akili kumbuka ndio waliopigania Uhuru wa nchi yetu leo tuko huru pamoja na challenges zilizopo.
 
Mtoamada! Shika adabu na adabu ikushike!
Wewe nani ? Utomboke wazee wa Dar hawana akili ?
Mimi sikai Dar, wala sina Mzazi Dar, kilichonigusa ni kuona lugha uliyoitumia haina nguo!
Unadhani ni Jf's members wangapi na nje members wenye wazee wao Dar?
Blood-msondongoma wewe , bendi ya zamani .
Unaongea kwa kutumia firigisi unayoikalia au?
 
Ni utamduni ulioasisiwa na baba wa taifa (wengine hawapendi kumwita hivyo akiwemo Kikwete). Wakati huo ilikuwa Mfumo wa kichama kimoja.
Nyakati zimebadilika na sio wazee wote wapo ccm. Hawa wazee wa Kikwete wanapatikana kwa njia gani?
Wanashangalia kila kitu. Wakati wake Mwl alikuwa na utamduni wa kuongea na wasomi pale Mlimani. Waliofuata wote wanapaona kama mahabusu. Hamna kasuku pale ni hoja tu
 
Mada hii imepitwa na wakati. Ni ya mwaka 2013. Kwani wewe umueshimu babako?
 
Kikwete ataongea na wazee kuwakata ngebe za wale wanaotaka mawaziri wake wafukuzwe au awafukue au awaondoe. Hii sio nchi ya kiimla. Hakuna namna yoyote Rais atatoa tangazo la kuwaondoa mawaziri kwenye mkutano kama huo. Kwa maoni yangu ni kuwa kama alivyoachia mambo ya katiba mpya yakazungumzwa mpaka akapokea rasimu ya kati na akaja kugeuka ndivyo hivyo ameacha hili la escrow limezungumzwa mpaka mwisho. Atakachosema kuhusu escrow (ikiwa tu atalizungumzia) mtakushangaa. Ni maoni yangu kuwa hatamwondoa mtu kazini siku hiyo.
 
Ujumbe Kwa Majid Mjengwa.

Kutumia utashi wako wa uandishi kuzua jambo ambalo nina uhakika unafahamu undani wake, umeonyesha jinsi ulivyopwaya kiakili.
Kama ni mwandishi wa blogu au makala, jinsi ulivyoelekeza hoja na maswali yako, ni wazi ultegemea kuamsha hisia za chuki na ubaradhuli dhidi ya wazee wa Dar.
Lengo lako hasa ilikuwa ni nini?
Wivu? choyo? Kukosa shukurani au kujipandisha kwa kumdhalilisha mwengine?
Ulikuwa na ajenda ambayo kwa kiasi imekamilika. Kupanda mzizi wa kudharau waasisi wa taifa hili na vizazi vyao.
Dar ni mji na ulikaliwa na watu, bila shaka watakuwepo wazee. Vizazi vyao vipo na wameweza kuwakaribisheni wengi waliokuja toka hata Iringa kama wewe.
Tunza heshima na adabu kwa wazee, wako na wa wenzako!

Bw. Mjenga... Utu wa mtu haudharauliwi!
Nataka uombe samahani kwa hili.
 
:smow::smow:MASUALA YA KITAIFA SI YA WAZEE WA CCM DAR, HEBU RAISI AJIFUNZE KUACHANA NA UTENDAJI WA KIMAZOWEA SIKUHIZI NI UTARATIBU:msela::msela::msela:
 
Wazee wa daressalaam ndo wazee pekee wanaoweza kudanganywa kirahisi na kumpigia makofi anayewanganya na jamaa hapo alishaona ndo mahali sahihi pa kupigia porojo zake
 
Kuna wengine wanajiita(UWT)nao ajabu hakuna anayetoka nje ya CCM,ni bora wangebadili jina wakajiita Umoja wa wanawake wa ccm Tanzania.
 
Mkuu umeniwahi,na wengi ya wazee hao ni kutoka Ilala na Temeke,na hasa wa Ilala wao ndio uwa wanajiita wenye jiji,elimu hawana,maisha ya kueleweka hawana,wao ni vijiweni na story za kale tu na story za Simba,Pan na Young,wazee waliostaarabika wako mbali kabisa na hao wazee!
.yes mkuu ni vile vizee vilikimbia vijiji vya ujamaa enzi za nyerere vikaja dar kufanya kazi bandarini,relini nk nk.vingi vinaona aibu kurudi kwao kijijini maana havijaacha hata kibanda vitafikia wapi?wale wanaojitambua wamerudi kijijini wanakula pensheni safi walizowekeza kwa watoto,mashamba,mifugo,majengo nk nk.ni maskini sana wanaokuja kumsikiliza prof vasco da gama
 
.yes mkuu ni vile vizee vilikimbia vijiji vya ujamaa enzi za nyerere vikaja dar kufanya kazi bandarini,relini nk nk.vingi vinaona aibu kurudi kwao kijijini maana havijaacha hata kibanda vitafikia wapi?wale wanaojitambua wamerudi kijijini wanakula pensheni safi walizowekeza kwa watoto,mashamba,mifugo,majengo nk nk.ni maskini sana wanaokuja kumsikiliza prof vasco da gama


Hao sio "wazee" wa Dar mkuu.
Ni vibarua na wapagazi waliokuja tu kutoka bara na kuiga mienendo na maisha ya Dar mkuu!
Nyerere pia alikuwa ni wakuja tu, alikaribishwa mjini kabla hajakua kiongozi wa chochote kile na hao wazee.
Ujamaa ni kitu cha juzi tu, ukweli ni wabara wengi walikimbilia jijini na wakarowea. Walikuwa ndio wapagazi na wauza mazao ya ma Alwatan wa jijini.
Wazee ma Alwatan wa Dar na koo zao ni watu kama akina Adulwahid Sykes, John Rupia, Jumbe Tambaza, Aziz Ali nk ambao jiji lilikuwa ni mashamba yao! Koo zao zipo na bado zinajimudu. Cha muhimu zaidi, uungwana na ustaarabu wao hauwezi kushushwa kwa matusi rejereja ya wanyika!
 
Wazee wa daressalaam ndo wazee pekee wanaoweza kudanganywa kirahisi na kumpigia makofi anayewanganya na jamaa hapo alishaona ndo mahali sahihi pa kupigia porojo zake


Kuna wakati ilipotolewa kauli ya "bora ninyimwe kura kuliko kuongeza mishahara" vizee vingi vilitolewa maeneo ya bagamoyo kuja kusikiliza speech baada ya intelijensia kusikia vile vya city vimeota speech kuwa isingekuwa na mashiko
 
SIFA ZAO. Sifa Ya Kwanza Kabisa Na Ya Muhimu Lazima Uwe ZOMBI AU JUHA KWANZA NDO UTAWEZA KUFANYA WAFANYAYO HAO WAZEE.PILI,Usiwe Na Ajira.3. Uwe Tayari Kupiga Makofi Hata Kama Atajamba TU. UNIFORM ZAO. Kibandiko Kichwani, Kanzu,fulana Au Shati La C.C.M Mkongoja, Kandambili Au Makubazi Yaliyochakaa. Kwa Mwanaume Sifa Ya Ziada Uwe Na Busha.
 
JE Umewahi Kujiuliza Gharama Za Mkutano Huo Zinalipwa Na Nani Kama Siyo Serikali? Je Umewahi Kujiuliza Iweje Wahudhuriaji Wawe Wazee Wa C.C.M Peke Yao Huku Wakivalia Matambala Yao Ya Kijani Utafikiri Mkutano Ni Wa Chama Chao Na Gharama Zimelipwa Na Chama Chao?

Je Umewahi Kujiuliza Ni Gharama Kiasi Gani Zinatumika Kwa Kuendekeza Ufisadi Huo Huku Bohari Kuu Ya Madawa Ikiwa Haijalipwa Pesa Zake Zote,waalim Malimbikizo Hayajalipwa? Na Kwanini Ahutubie Wazee Wa Dar Peke Yao Na Siyo Wa Nzega?

Ni Lini Zamu Ya Vijana? Kuandaa Mkutano Kwa Gharama Za Serikali Halafu Wahudhuriaji Wawe Wazee Wa C.C.M Peke Yao Huo Ni Ufisadi Na Ni Matumizi Mabaya Ya Pesa Za Umma!! Wananchi Tuzinduke Tusiruhusu Hii Hali Ijirudie.
 
JE Umewahi Kujiuliza Gharama Za Mkutano Huo Zinalipwa Na Nani Kama Siyo Serikali? Je Umewahi Kujiuliza Iweje Wahudhuriaji Wawe Wazee Wa C.C.M Peke Yao Huku Wakivalia Matambala Yao Ya Kijani Utafikiri Mkutano Ni Wa Chama Chao Na Gharama Zimelipwa Na Chama Chao? Je Umewahi Kujiuliza Ni Gharama Kiasi Gani Zinatumika Kwa Kuendekeza Ufisadi Huo Huku Bohari Kuu Ya Madawa Ikiwa Haijalipwa Pesa Zake Zote,waalim Malimbikizo Hayajalipwa? Na Kwanini Ahutubie Wazee Wa Dar Peke Yao Na Siyo Wa Nzega? Ni Lini Zamu Ya Vijana? Kuandaa Mkutano Kwa Gharama Za Serikali Halafu Wahudhuriaji Wawe Wazee Wa C.C.M Peke Yao Huo Ni Ufisadi Na Ni Matumizi Mabaya Ya Pesa Za Umma!! Wananchi Tuzinduke Tusiruhusu Hii Hali Ijirudie.

No one cares about your political views in the first place
 
Huo ndio uwezo wake hawezi ongea Na Wanahabari maana watampiga maswali magumu au la Rweyemamu atawaalika wale uhuru tu Na kuwapangia cha kuuliza , hawezi pia kuongea na Intellectuals pale Mlimani au pengine maana anajua wataona chenga zake na hawatompgia makofi huko anajua kuwa lobby tu wampe Honourable PhD tu, aige kwa Obama alichofanya juzi kukata kiu ya WaAmerika kuhusu maswala nyeti ya kitaifa , au Ahmed al Nijad wa Iran alivyokua anafanya. Kesho sitegemei kipya zaidi ya wale wazee wa Lumumba Kupoka bahasha zilizotuna zaidi maana nao wameiskia Escrow. Akireshuffle baraza la mawaziri kwa kuwa piga chini wote kulingana Na maazimio ya bunge atakua kanipa Zawadi ya sikukuu ya Noeli(Christmas) kwa mara kwanza ndani ya miaka yake tisa.
Jumapili njema - Kilele Pori.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom