Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

nadhani mleta mada ana matatizo ya ufahamu. Rais hazungumzi na wazee bali analihutubia taifa. Hao wazee ni hadhira ambayo inaweza kuwa kikundi chochote cha watu. Jingine, inashangaza sana unaposhindwa kuona umuhimu wa wazee. Au kwa vile wazee wa chama chako wametopea kwenye uzinifu na kila aina ya kukosa busara?

Hao wazee mpaka sasa hakuna la maaana walilomshauri Rais badala yake wameishia kula chakula cha bure tunacholipia kodi sisi na kupewa posho huku nchi ikienda arijojo.
 
nadhani mleta mada ana matatizo ya ufahamu. Rais hazungumzi na wazee bali analihutubia taifa. Hao wazee ni hadhira ambayo inaweza kuwa kikundi chochote cha watu. Jingine, inashangaza sana unaposhindwa kuona umuhimu wa wazee. Au kwa vile wazee wa chama chako wametopea kwenye uzinifu na kila aina ya kukosa busara?
Utakuwa na homa
 
Hao sio "wazee" wa Dar mkuu.
Ni vibarua na wapagazi waliokuja tu kutoka bara na kuiga mienendo na maisha ya Dar mkuu!
Nyerere pia alikuwa ni wakuja tu, alikaribishwa mjini kabla hajakua kiongozi wa chochote kile na hao wazee.
Ujamaa ni kitu cha juzi tu, ukweli ni wabara wengi walikimbilia jijini na wakarowea. Walikuwa ndio wapagazi na wauza mazao ya ma Alwatan wa jijini.
Wazee ma Alwatan wa Dar na koo zao ni watu kama akina Adulwahid Sykes, John Rupia, Jumbe Tambaza, Aziz Ali nk ambao jiji lilikuwa ni mashamba yao! Koo zao zipo na bado zinajimudu. Cha muhimu zaidi, uungwana na ustaarabu wao hauwezi kushushwa kwa matusi rejereja ya wanyika!
.Asante mkuu kwa ufafanunuzi.inawezekena we ni ndugu,mi myika wa ndolezi.wewe je?
 
Wazee wote wanaoitwa kuongea na Jk ni wenye mtindio wa ubongo na mazuzu tu na hawana msaada kwa Taifa letu.
 
Huu uzi umewafanya ikulu kufanya madiliko makubwa kuwaalika Hao wanaoitwa wazee wa Daresalam.

Nimesikia kwenye vyombo vya Habari ikulu imesema wazee watakaohudhuria ni wale tu walioalikwa "wazee wengine wabaki tu majumbani hotuba ya Rais wataifatilia wakiwa majumbani mwao"

Hii ni baada ya wadau Hapa kuhoji sifa za wazee wanaoalikwa, maana wengi wao huwa wanasinzia tu na kupiga makofi hata sehemu anayouliza maswali.

Leo tutarajie sare za CCM kupungua au kutokuepo kabisa.
 
Mhe. Rais wa JMT ndio anaingia Ukumbini sasa!Nasikiliza kupitia TBC FM 87.5
 
Kikwete ataongea na wazee kuwakata ngebe za wale wanaotaka mawaziri wake wafukuzwe au awafukue au awaondoe. Hii sio nchi ya kiimla. Hakuna namna yoyote Rais atatoa tangazo la kuwaondoa mawaziri kwenye mkutano kama huo. Kwa maoni yangu ni kuwa kama alivyoachia mambo ya katiba mpya yakazungumzwa mpaka akapokea rasimu ya kati na akaja kugeuka ndivyo hivyo ameacha hili la escrow limezungumzwa mpaka mwisho. Atakachosema kuhusu escrow (ikiwa tu atalizungumzia) mtakushangaa. Ni maoni yangu kuwa hatamwondoa mtu kazini siku hiyo.

Niliyasema haya 20.12.2014 saa 13.13
 
Ni kwenye mkutano wa Jk pale diamond jubilee
1419261786373.jpg
 
Back
Top Bottom